Hoja ya Lisu ni kwamba; Kwa nini sheria ziandikwe kwa kiingereza ikiwa lugha ya taifa ni Kiswahili, wanaotunga sheria (wabunge) hawajui kiingereza na hata wananchi zaidi ya asilimia 95 hawajui.
Kwa hali hii kuna tatizo kubwa!
Sheria ni noble profession bana...hivyo sheria haziwezi kuandikwa kwa Kiswahili.
Wapi Kiranga ....
Taratibu mkuu! Atakutumia mabaunsa wasionekana
Upo sawa kabisa, kwa sie wanananchi tutaona kiswahili kinatumika lakini makabrasha yao yanaandikwa kwa kizungu, nadhani hoja hapa either kuwa na wabunge wenye uweledi wa kiingereza au kiswahili ambacho ni lugha ya taifa kitumike kikamilifu mpaka kwenye makabrasha yao alafu serikali ifanye kazi ya kupeleka kwenye kiingerezaBunge hutumia lugha ya kiswahili kufikisha ujumbe kwa wananchi.
Ni muhimu kumkumbusha Tundu Lisu kuwa hatutumii kisukuma, kindengeleko, kijerumeni wala kiingereza kwenye bunge wala kwenye kampeni za kugombea Ubunge. Na wala si sherti kuwa mbunge LAZIMA AJUE KIINGEREZA kwani wabunge wengi wa Ujerumani, Ufaransa, URUSI n.k hawajui kiingereza.
Ushauri wangu kwa T. Lisu: Kama umeshindwa kufanikisha AJENDA KUU YA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI NI BORA UJIUZULU UBUNGE. HATA SIKU MOJA SITOCHAGUA MBUNGE KWA KIGEZO CHA KIINGEREZA BALI KWA UADILIFU, KUJALI WANANCHI, KUWA MBUNIFU WA UTATUZI WA MATATIZO YA WANANCHI NA KUWA SEHEMU YA WANANCHI.
Nadhani ndio maana akatoa kauli ile ili hoja hapo itumike lugha ambayo inaeleweka alafu serikali irudishe miswada kwa kiingereza mara baada ya kujadiliwa, lakini utaratibu uliopo watu wanabwabwaja kwa kiswahili alafu mambo yanaandikwa kwa kiingerezaMbona yeye Tundu Lisu kwa wakili Msando aliomba Kitumike Kiswahili,baada ya kuchemka Kiingereza
CC
msando
Yule mwanakwaya wa TOT vipi mayai yanapanda au yule mzee wa gombe vipi??????????????????????????.Mkuu, hata prof Kulikoela Kahigi ni aibu tupu
Nakumbuka kijana Albert Msando alivyomtoa nduki Lissu kwenye matumizi ya kugha ya kiingereza wakati wa kesi ya Zitto mpaka Lissu akaomba poo kwa kuomba mahakama itengue matumizi ya lugha ya kiingereza na kutumia kiswahili
Jamaa kasema "Qualification kubwa kabisa ya kuwa mwanasheria ni lazima ujue oral english". Hajasema kwa tz! Kachemka.kwa tz lazima iwe hivyo kwasababu sheria zipo kwa kingereza
huyu usimuonee ni profesa wa kiswahili sasa kiingereza na kiswahili wapi na wapi?mkuu, hata prof kulikoela kahigi ni aibu tupu
Bunge hutumia lugha ya kiswahili kufikisha ujumbe kwa wananchi.
Ni muhimu kumkumbusha Tundu Lisu kuwa hatutumii kisukuma, kindengeleko, kijerumeni wala kiingereza kwenye bunge wala kwenye kampeni za kugombea Ubunge. Na wala si sherti kuwa mbunge LAZIMA AJUE KIINGEREZA kwani wabunge wengi wa Ujerumani, Ufaransa, URUSI n.k hawajui kiingereza.
wewe mwenyewe kiingereza hujui zaidi ya kusema "so called Lema" tunakujua sana wewe Mjinga unaejipachika jina la kihayaTundu Lissu bhana anapenda kuwadanganya watanzania.
Sidhani kama kingereza ni kikwazo kabisa katika shughuli nyingi za wabunge maana asilimia 70% ni kiswahili ndio kina tumika na bado utendaji ni mbovu.
Ni sehemu chache sana zina mlazimu mbunge kujua kingereza tena cha kusoma hasa kwenye mikataba.
Si kweli kingereza ni kikwazo.
Hata yeye tundu lissu aliomba msamaha kitumeke kiswahili kwa kisingizio cha maslahi ya umma kumbe kijana msando alberto alimtoa jasho kwenye lugha ya kigeni.
Ni kweli wabunge wengi wa Ujerumani, Ufaransa, URUSI n.k hawajui lugha ya Kiingereza, lakini serikali zao hazileti bungeni miswada iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza bali kwa lugha zao.