Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,099
- 79,498
MHE. RAIS UNAPOTEZA MUDA WAKO TUU.
Na, Robert Heriel.
Moja ya mambo yanayonisikitisha katika jamii yangu ni pamoja na hili nitakalolisema hivi leo. Ninaumia sana kuona jamii yangu ikiwa katika dhiki kuu. Katika tabu, na umasikini wa aibu isiyoelezeka.
Umri wangu najua bado ni mdogo, lakini sishindwi kusema machache kwa yale niliyoyaona, yasikia au kusoma. Basi kwa vile imenipendeza leo, na nimepata nafasi kuandika, acha niandike kwa faida ya wenye mapenzi mema na jamii yetu, wapendao taifa hili na kizazi kijacho.
Niite Taikon wa Fasihi, Mwanafalsafa katika zama za uharibifu.
Ili tumkabili adui sharti tujue ni wapi alipotuzidia. Wapi adui alipotuzidi. Ni wapi nauliza? Adui anaweza kutuzidi mambo mengi lakini yapo mambo ya msingi ambayo ndio ushindi wake ulipo. Endapo tukilifahamu jambo hili basi ni wazi tunaouwezo wa kumkabili adui huyo.
Taifa hili limepitia Historia kadhaa tangu hapo nyuma. Kabla halijawa taifa lilikuwa na maadui, na hata baada ya kuwa taifa bado lina maadui. Jambo moja la dhahiri ni kuwa taifa letu kamwe halitakosa adui dunia ingalipo. Hii ni kusema, kama hatutajua namna bora ya kukabiliana na adui basi tutatawaliwa milele. Mbinu bora na yalazima ya kumshinda adui kama nilivyokwisha kusema awali ni kuwa, sharti tujue adui ni wapi alipotuzia, hasa mambo ya msingi.
Mara kadhaa nimekuwa nikifuatilia Viongozi wetu namna wanavyojitahidi kutetea jamii zao. Kwa bahati mbaya ni kuwa viongozi wengi hawapo kwa maslahi ya jamii zao bali wapo kwa ajili ya familia zao. Hii sio mbaya ikiwa itafanywa kwa uadilifu lakini kama itafanywa kwa ubinafsi wa kuibia wengine na kujilimbikizia mali inasababisha umasikini zaidi na zaidi.
Andiko hili linalenga kufanya mabadiliko ya msingi katika fikra za viongozi wa taifa hili wakiwakilishwa na kiongozi mkuu ambaye ni Rais John Pombe Magufuli ambaye ndiye anayetawala kwa muda huu wakati andiko hili linaandikwa. Hii ni kusema, Mhe Rais, Magufuli anawakati muhimu wa kuandika historia ya kukumbukwa yenye manufaa kwa vizazi elfu vijavyo ikiwa atafuata baadhi ya mambo niliyoandika kama sehemu ya ushauri wangu na mchango wangu katika taifa hili.
Nafahamu hisia hasi zinaweza kuzuka baada ya andiko hili kutokana na kichwa cha habari cha makala hii. Lakini itaeleweka kwa wenye kufikiri vizuri ni nini nilikuwa nataka kusema hasa, mpaka kufikia hatua ya kuandika kuwa 'Rais anapoteza muda wake. Tafsiri ya waliowengi inaweza kuwa, huenda Rais hana akifanyacho zaidi ya kucheza tuu. Hii inaweza kuwa maana potofu lakini inayokaribia ukweli.
Mhe. Rais, kwa heshima ya cheo chako, umri, elimu na heshima ya utu wako kama binadamu wengine. Niruhusu sasa nizungumze na wewe kupitia andiko hili ambalo linaweza kukufanya kuwa Rais ambaye hatakuja atokee tena katika taifa letu ikiwa utayazingatia na kuyafanya mambo yaliyosemwa humu. Tena naamini ukiyaboresha utakuwa kiongozi ambaye utaifanya nchi hii iwe moja ya nchi kubwa zenye heshima duniani.
Mhe. Rais, bila shaka unajua ni wapi adui zetu walipotuzidi. Lakini kwa heshima yako naomba nidokeze kwa ufupi ni mambo gani ambayo adui ametuzidi ambayo kama hayatashughulikiwa hayo basi utakuwa ni moja ya waliopoteza muda wao, nguvu zao, akili zao katika uongozi kwa nafasi ya Urais.
Adui hajatuzidi maghorofa, wapo wanaodhani kuwa adui zetu wametuzidi majengo marefu katika majiji. Sio kweli. Adui hajatuzidi barabara, reli, viwanja vya ndege, madaraja, miongoni mwa mengine. Wapo wanaodhani hivyo lakini ukweli ni kuwa adui hajatuzidi mambo hayo.
Wapo wanaodhani, adui ametuzidi teknolojia mbalimbali kama mawasiliano, Tiba, mahospitali ya kisasa, magari, ndege, meli, masuala ya Tehama miongoni mwa mengine. Lakini ukweli ni kuwa adui hajatuzidi katika mambo hayo.
Wapo wanaodhani adui ametuzidi silaha, mbinu za kivita, sijui mitambo ya kulinda anga, mitambo ya kudungua ndege vita, meli za kivita, manyambizi miongoni mwa mengine. Lakini ukweli ni kuwa adui yetu hajatuzidi mambo hayo.
Wengi wanaofikiri kwa namna hiyo hutumia akili ndogo kufikiri. Kwani wenye akili ndogo hufikiri mambo wayaonayo pekee yake lakini wenye hekima na werevu sana hufikiri mambo wayaonayo na yale wasiyoyaona. Ninapozungumzia mambo yasiyoonekana simaanishi mambo ya kiimani. Hivyo nisijechukuliwa vibaya.
Ingekuwa adui zetu wametuzidi mambo hayo basi nasi tungepata nafasi ya kusema nasi tumewazidi mambo kama Uwepo wa rasilimali halisia za kila namna, Mathalani; Uoto wa asili ambapo kuna misitu mizuri kabisa, vichaka vifupi na virefu, maua ya kila namna, miti ya kila namna miongoni mwa uoto wa asili. Pia rasilimali madini kama vile, dhahabu, almas, Tanzanite miongoni mwa madini mengine.
Pia kuna, Rasilimali wanyama wa mwituni na wakufuga. Tuna mbuga za kila namna zenye wanyama wa kila namna. Mbuga nyingi zenye ukubwa wa kistaajabisha na wanyama wa ajabu isivyo elezeka. Pia tuna Rasilimali ardhi kubwa yenye Rutuba na kiasi kidogo kisicho na Rutuba. Tuna milima kwa aina zake tena mingine ya kipekee duniani haipo. Mito, maziwa na bahari vyote tunavyo.
Bila kusahau Rasilimali watu ambapo kwa idadi nchi yetu inashika nafasi ya tatu kwa wingi wa watu. Sasa je, ni nini adui alichotuzidi pamoja na mambo yote hayo?
Mhe. Rais, Adui ametuzidi jambo moja muhimu mno ambalo kama tutalishughulikia tutajinasua kwenye makucha yake.
Mhe. Rais, najua unalengo la kuacha alama hasa ya kuinua maisha ya Watanzania. Unatamani kuona watanzania wakiishi maisha mazuri. Ni jambo jema sana, tena sana. Lakini njia itumiwayo sio sahihi.
Watanzania hawana shida ya umeme, watanzania hawana shida ya maji, Watanzania hawana shida ya madege makubwa uliyoyanunua. Watanzania hawana shida na nyumba nzuri, Watanzania hawana shida ya Treni ya mwendo kasi, Watanzania hawana shida bandari kubwa ya kisasa. Ipo shida muhimu na yalazima ambayo watanzania wanayo ambayo ni mtaji wa adui zetu. Na shida hiyo isipotatuliwa basi mambo utakayo yafanya ni kama utakuwa unapoteza muda wako tuu.
Kitu pekee walichotuzidi adui zetu ni ELIMU NA MAARIFA. Hapo ndipo tulipopigwa vibaya na adui zetu. Mhe. Rais ni muhimu kusema haya kwa mustakabali wa nchi hii na kizazi kijacho. Kiongozi bora atakaye kumbukwa kwa kuijenga nchi hii ni yule atakayetoa elimu sahihi na maarifa sahihi kwa taifa hili.
Ninasikitika sana kusema kuwa unapoteza muda wako kama walivyopoteza wengine. Kama hutatoa elimu na Maarifa muhimu kwa taifa hili basi tambua chochote ulichokianzisha kitakufa na wala hakitadumu. Sijui viwanda vitakufa, hayo madege yatakufa, sijui Reli ya mwendo kasi itakufa, sijui nini.... Vyote vitakufa na cha ajabu havitafikisha hata miaka ishirini vitakuwa vimepotea na aliyevianzisha ataonekana kama alikuwa anacheza mdumange.
Utaungana na mimi yakuwa kabla yako, enzi za Baba wa Taifa vilijengwa viwanda kadhaa lakini karibia vyote vilikufa. Na ipo sababu ya viwanda hivyo kufa, lakini sababu kuu ni ELIMU NA MAARIFA ambayo jamii yetu haina. Hata Reli ya kaskazini iliuawa kwa kuhujumiwa lakini kwa bahati njema umeweza kuifufua upya.
Hongera sana lakini nakuhakikishia, vyote vitakufa hata kabla ya miaka ishirini ijayo baada ya wewe kutoka madarakani. Embu niambie ikiwa vitakufa vitu ulivyovianzisha je bado muda huu haupotezi muda wako?
Mtu asiye na elimu wala maarifa hana tofauti na mnyama. Nitakupa mfano; Mtengenezee kuku au ng'ombe banda la kuishi. Utakuwa umefanya jambo jema lakini kutokana na kuwa ng'ombe hana elimu wala maarifa hilo banda litaharibika, atanyea humo humo bila kufanya usafi. Banda litaharibika na hatakuwa na uwezo wa kulitengeneza. Hii ni kutokana na ukosefu wa elimu na maarifa.
Basi mtu asiye na elimu na maarifa hana tofauti kubwa na ng'ombe. Ukimnunulia ndege, sijui bombadie lazima zife tuu. Ukimjengea Reli utashangaa mwezi tuu anaiba mataruma akauze. Ukimjengea barabara ya lami utashangaa anapakiza mizigo mingi yenye uzito kupitiliza mwishowe barabara inaharibika. Ukimuwekea mitandoa ya kijamii, usishangae akapost matusi au picha za uchi, usimlaumu kosa sio lake bali akili yake ni kama mnyama tuu haina tofauti na Mbwa au paka.
Mhe. Rais, nakuhakikishia unapoteza muda wako. Sema nini, sio wewe pekeako bali karibia viongozi wote wa Afrika ndivyo wanavyofanya. Wanapoteza muda wao tu.
Kama kiongozi hataki kupoteza muda, na anataka kukumbukwa daima kwa kuleta maendeleo kwa taifa hili hana budi kuwekeza zaidi kwenye suala la ELIMU na MAARIFA. Kuwekeza kwenye elimu utatumia gharama kubwa lakini pia utapata matokeo makubwa. Kuwekeza kwenye sekta zingine utatumia gharama kubwa lakini hutapata faida yeyote zaidi ya kuishia kupata hasara.
Serikali ni kama mzazi. Mzazi anapowekeza zaidi kwenye kumnunulia mtoto sijui nguo kali, viatu, saa, na mambo mengine ya kitoto ili amfurahishe mtoto na kuacha kuwekeza kwenye elimu ya mtoto basi tunasema kuwa mzazi huyo anapoteza muda wake kwani mtoto huyo atakapokuwa mkubwa bila elimu atajikuta yupo yupo tuu. Tumewaona wazazi waliojibana wakasomesha watoto wao na matokeo waliyapata. Lakini wale waliowekeza kwingine pia matokeo waliyapata.
Hata wewe Mhe. Rais ninajua ya kuwa hapo ulipofika ni matokeo ya wazazi wako kujizuia na kuwekeza kwenye elimu yako. Leo hii wewe ni Rais wa nchi. Lakini kama wangewekeza kwingine si ajabu leo hii ungekuwa upo kijijini umechapika haswa na maisha. Lakini elimu imekufikisha hapo.
Adui zetu wametuzidi kwenye suala la elimu na maarifa. kama ni hivyo Mhe. Rais unatakiwa macho yako yote yaelekee huko. Ujikite huko zaidi. Uwekeze huko.
Elimu na Maarifa tuliyonayo ibadilishwe iendane na mazingira ya sasa. Iwe ya Mafunzo kwa vitendo. Iwe kimkakati zaidi. Sio Elimu ya GPA sijui ya Division gani sijui huko.
Kama taifa hili elimu yake ukiibadilisha nakuhakikishia utakuwa umesaidia taifa hili kwa kizazi hiki na kijacho. Wala hutokuwa unapoteza muda.
Elimu iwe ya vitendo
Elimu ijihusishe na kubadili mtazamo na fikra za watanzania,
Elimu itengeneze watu wanaofikiria zaidi na kubuni na sio kusubiri kubuniwa na watu wengine.
Mhe. Rais, ukubali au ukatae bila kubadili mfumo wa elimu hapa nchini, Ni wazi utakuwa unapoteza muda wako tuu.
Mwl. Nyerere alijua hili kabisa. Ndio maana kwenye azimio la Arusha 1967, akaja na sera ya Education for self Reliance, naam ndio elimu ya kujitegemea. Hapo ndipo ugomvi wake ulipo na adui zake. Wala hakugombana eti kisa sijui alitaja nchi iwe ya kijamaa. Ujamaa sio kikwazo kwa adui zetu. Kikwazo pekee ni kuwa na elimu sahihi itakayo wafanya watanzania wajitambue na kujitegemea.
Mhe. Rais, Elimu iliyokuwepo kwa sasa hata ujenge pepo hapa Tanzania nina uhakika pepo hiyo haitadumu hata kwa miaka 20. Itageuka kuzimu. Hata ufanye nini bila kutoa elimu kwa watanzania utakuwa unacheza mdumange tuu.
MAPENDEKEZO YANGU KUHUSU NAMNA ELIMU YETU INAVYOTAKIWA KUWA:
Elimu iwe katika ngazi tatu;-
a) Ngazi ya Familia
b) Ngazi ya serikali za mitaa
c) Ngazi ya taifa
A) NGAZI YA FAMILIA.
Katika muundo wa elimu unapaswa kuanzia ngazi ya chini kabisa ya familia. Kuanzia mama anapokuwa mjamzito mpaka mtoto anapofikisha umri wa miaka saba.
Hii ndio ngazi muhimu kabisa kwa mtoto kwa mustakabali wa nchi.
Hapa napendekeza mambo yafuatayo:
i) Viandaliwe vitabu mahususi kwa ajili ya kutoa elimu kwa ngazi hii.
ii) Wazazi(Baba na Mama) au walezi, wanapaswa kuhudhuria kwa wiki mara moja kwenye mafunzo maalumu kuanzia wakati wa mimba mpaka mtoto anapofikisha miaka saba.
iii) Serikali iandae kozi maalumu ya wafanyakazi wa ndani(Housekeeping course) ambapo wafanyakazi watalea watoto kulingana na miongozo waliyofundishwa. Wafanyakazi wa ndani hao watakuwa pia na elimu ya Uuguzi kwa watoto hata kwa ngazi ya cheti.
iv) Katika umri huu mtoto atakuwa anafundishwa adabu na wazazi na kwa vile wazazi watakuwa bize basi housemaid(msaidizi wa ndani aliyehitimu mafunzo) atakuwa na wajibu wa kumfunza mtoto elimu.
v) Umri huu mtoto afundishwe usafi, adabu, Upendo na maadili.
vi) Au ziundwe Daycare zinazotambulika na serikali ambazo zitahusika na malezi ya mtoto tangu akiwa mdogo mpaka miaka saba. Pawe na vitabu maalumu na miongozo itakayotumika nchi nzima. Walimu waliosomea ndio wahusike na angalau muuguzi mmoja kwa afya za watoto.
vii) Kila baada ya nyumba arobaini kuwe na angalau Daycare moja kwa ajili ya mafunzo.
Na mambo mengine..
B) NGAZI YA SERIKALI ZA MITAA.
Hii ni ngazi ya pili ambayo mtoto atadumu kwenye ngazi hii kwa miaka saba tena. Kumaanisha atakuwa amefikisha miaka kumi na nne.
Hapa mtoto atafundishwa uzalendo, masomo ya kazi za mikono kulingana na mapenzi ya mtoto au kwa msaada wa wazazi. Atafundishwa Historia ya nchi yake. Na elimu ya msingi ya mazingira na mwili wake.
Napendekeza:
i) Kila mwaka ndani ya miaka saba kuwe na masomo masomo manne. Ambayo kila siku yatafundishwa. Liwepo somo la Uraia, Sayansi, Utamaduni, na somo moja liwe somo linalohusu fani yake. Ambapo mtoto atafundishwa kulingana na umri wake vitu rahisi rahisi vitakavyomfanya aelewe.
Ratiba inaweza kuwa hivi:
Ratiba kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni:
Uraia = saa 02;00 - 3;20
Sayansi = Saa 3:21 - 4: 40
MAPUMZIKO= 4;40 -5;00
Utamaduni = 5;00 - 6;20
Somo la fani = 6:20 - 7: 40
MAPUMZIKO YA CHAKULA CHA MCHANA= 7:40 - 8:00.
Stadi za kazi = 8:00 - 10:00 jioni. Hii ni kila siku ipo muda huu huu.
Mfano wa masomo hayo utafundishwa kila mwaka.
Mtoto afundishwe mada nyepesi kulingana na umri huo wa miaka saba mpaka akihitimu baada ya miaka saba ambapo atakuwa na miaka kumi na nne ataenda ngazi ya taifa.
C: NGAZI YA TAIFA
Hapa asome kwa miaka mitatu. 14 -18.
Hapa mtoto atakuwa anasomea kwa kina fani yake. Kama ni mwalimu, Daktari, mwanasheria n.k.
Mapendekezo
Naomba niweke wazi kuwa masomo hayo niliyotolea kama mfano yatawekwa kulingana na uhusiano wa somo na somo. Hivyo huo ni mfano tuu.
FAIDA YA MABADILIKO YA KIMUUNDO
CHANGAMOTO TARAJIWA
NAMNA YA KUZIKABILI CHANGAMOTO.
Pawe na bodi maalumu ya wanaharakati ambapo kama mtu atakiuka sheria zitakazo wekwa basi atafutwa kwenye fani hiyo na hataruhusiwa kukemea, kutetea au kukosoa jambo. Na hii iwe kwa wasio wazalendo.
Mwanaharakati hataruhusiwa kuwa na ushabiki wa chama au dini ili kuepusha upendeleo kwa kundi fulani.
Mwanaharakati sharti awe na uwezo wa kupiga pande zote na kutoa hoja zenye mashiko pasipo kuvunja haki za utu.
Ilani ya nchi na sera za nchi ziwe kwa viipindi kumi kumi. Hata kama watawala watachaguliwa kila baada ya miaka mitano. Hata kama Rais ataongoza awamu moja, atakayefuata atakamilisha alipoishia mwenzake ili mradi ndani ya miaka kumi yaliyoahidiwa kwenye ilani yamefanyika.
Endapo Rais atashindwa kutimiza malengo ya ilani na Sera ya nchi ndnai ya muda husika atashitakiwa kwa kosa la kushindwa kutimiza ilani ya muda husika.
Mhe. Rais, naomba niishie hapa. Ila kama unataka ukumbukwe na udumu katika fikra za Watanzania kwa zaidi ya miaka 1000 basi fanya mchakato wa kubadili uelekeo wa ELIMU na MAARIFA kwenye mashule.
Pia rekebisha katiba hasa kwa nafasi ya Urais.
Tanzania kwa vizazi vyetu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300

Katika ngazi hii mtoto afundishwe sayansi ya kawaida atakayoitumia kwenye mazingira ya kawaida. Mtoto atafundishwa hesabu muhimu tuu katika mazingira halisi. Isipokuwa wanafunzi wenye ndoto za kuwa aidha madaktari, mainjinia, wanajiografia, wahasibu na fani zote zenye hesabu, hawa watakutana na hesabu ngumu kidogo kwenye masomo ya fani zao kwenye kipindi husika.Sayansi (Hisabati, biolojia, phizikia, kemia n.k)
Hapa mtoto atafundishwa mambo yote ya uraia, historia ya nchi, mahusiano, maadili, uzalendo n.k Watapewa elimu ya msingi wote.Uraia
Hapa mtoto atafundishwa masuala yote ya utamaduni, kuwe na topic(mada) za lugha na mawasiliano, mavazi, vyakula, utembeaji, ngoma n.k.Utamaduni
Hapa mtoto atafundishwa kile anachotaka akiwa mkubwa akifanye. Kama ni daktari, au mwalimu, mwanasheria, mhandisi, mchoraji, fundi nguo n.k.Masomo ya Fani.
Mtoto afundishwe mada nyepesi kulingana na umri huo wa miaka saba mpaka akihitimu baada ya miaka saba ambapo atakuwa na miaka kumi na nne ataenda ngazi ya taifa.
Mtoto atafundishwa stadi za kazi za kila siku kwa vitendo. Kutunza bustani, kufuga, kulima, kufua nguo, kupika chakula, na mambo mengine. Stadi zitolewe kulingana na umri wa mtoto.Stadi za Kazi.
C: NGAZI YA TAIFA
Hapa asome kwa miaka mitatu. 14 -18.
Hapa mtoto atakuwa anasomea kwa kina fani yake. Kama ni mwalimu, Daktari, mwanasheria n.k.
Mapendekezo
Ili mtu afike ngazi hii atapaswa afanye mitihani kwenye ngazi ya pili ambayo ni ngazi ya serikali ya mitaa. Mtihani huu ujikite zaidi katika Ujuzi na uwezo wa kufaulu kwa njia ya mitihani ya karatasi. Ngazi hii ndio itambulike kama shahada. Na Watakaofika huku wawe kweli wameiva.
Kila kanda angalau kiwe na chuo kikuu kimoja kwa ajili ya kuivisha hawa vijana. Masomo yatakuwa ni nadharia na vitendo zaidi.
Naomba niweke wazi kuwa masomo hayo niliyotolea kama mfano yatawekwa kulingana na uhusiano wa somo na somo. Hivyo huo ni mfano tuu.
FAIDA YA MABADILIKO YA KIMUUNDO
Itaepusha mtoto kusoma miaka mingi kwa muundo wa 7:4:2:3. Hivyo mtoto wa miaka kumi na saba au nane tayari atakuwa na shahada yake ya awali.
Itapunguza mtoto kusoma mambo mengi ambayo hayatamsaidia kwenye maisha yake.
Itasaidia hata mtoto asipofika chuo kikuu anaouwezo wa kuendesha maisha yake kutokana na stadi za kazi alizofundishwa kwa vitendo kwa miaka saba. Hivyo tutapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira.
Watoto watakuwa na uzalendo, kutokana na uwepo wa mada ya uzalendo, maadili kwenye somo la uraia.
Watu watathamini utamaduni wa jamii zao na taifa lao kutokana na uwepo wa somo la utamaduni.
Teknolojia itakuwa kutokana na elimu kwa vitendo vinavyohusiana na mazingira halisi.
Sekta zingine zitainuka kutokana na uwepo wa wataalamu baada ya kufunzwa kwa nadharia na vitendo.
Itakuza vipaji vya watoto kutokana na kusomea mambo wayapendayo tangu wakiwa wadogo.
CHANGAMOTO TARAJIWA
Gharama za kuchapisha vitabu zitatakiwa
Kuandaa mtaala na miongozo ya kufundishia na kujifunzia inahitaji wataalamu waliobobea.
Baadhi ya watu miongoni mwetu kupinga
Nchi maadui kutuwekea vikwazo.
Baadhi ya fani zinaweza kukosa watu kutokana na kasumba iliyomo ndani ya jamii. Kwa mfano fani za sanaa zinaweza kukosa watu na fani za sayansi hasa udaktari madarasa kufurika kutokana na wazazi kuhitaji watoto wao wasomea masomo hayo hata kama mtoto hataki.
Gharama za ujenzi wa miundo mbinu wezeshi zinahitaji kujitoa kikamilifu. Ujenzi wa daycare, shule, vyuo, n.k
Gharama za zana na vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa vitendo zipo juu.
Malalamiko kutoka kwa watu kutokana na mazoea ya mfumo wa zamani.
NAMNA YA KUZIKABILI CHANGAMOTO.
Watu watoe kodi iwe kwa hiyari au kwa lazima kusudi mambo haya yafanyike.
Elimu ya Kodi itolewe
Sheria kali zichukuliwe kwa wataobainika kuhujumu, ubadhirifu wa pesa za serikali, ufisadi na Rushwa vidhibitiwe.
Vyombo vya habari vihamasishe na kutunga propaganda mahususi kwa kuwezesha mpango huu. Vyombo vya habari visijikite zaidi kwenye mambo ya udaku isipokuwa labda udaku kwa wasiolipa kodi, mafisadi, na wanaokwamisha miradi. Ziundwe propaganda na utumbuaji bandia na adhabu kali bandia kutisha wale wenye nia ya kuhujumu au kufisadi.
Wanamuziki wapewe muongozo wa nyimbo zitakazo hamasisha zaidi maendeleo na kuonyesha kwa vitendo.
Waigizaji nao waigize madhara yatakayowapata watakaokwamisha mipango hii.
Waandishi wa mitandaoni, magazeti na blogu wapewe semina elekezi ya namna ya kuandika makala zitakazojikita zaidi kwenye maendeleo.
Wanamitindo wapewe miongozo na sheria za ubunifu wa kimavazi yatakayohamasisha mipango hii ya maendeleo.
Wanaharakati wasajiliwe na kutambulika, nao wapewe elimu na semina kuhusu namna ya kutetea kile wanachokiamini.
Pawe na bodi maalumu ya wanaharakati ambapo kama mtu atakiuka sheria zitakazo wekwa basi atafutwa kwenye fani hiyo na hataruhusiwa kukemea, kutetea au kukosoa jambo. Na hii iwe kwa wasio wazalendo.
Mwanaharakati hataruhusiwa kuwa na ushabiki wa chama au dini ili kuepusha upendeleo kwa kundi fulani.
Mwanaharakati sharti awe na uwezo wa kupiga pande zote na kutoa hoja zenye mashiko pasipo kuvunja haki za utu.
Matamasha ya burudani yajikite zaidi kuhamasisha maendeleo.
Viongozi wote wa dini wasajiliwe na wapewe miongozo na sheria zao. Dini ni sehemu ya utamaduni, lakini pia ni biashara inayokua kwa kasi na inayoajiri watu wengi.
Iwepo siku ya elimu na maarifa nchini kwa Mwaka ambapo wale wenye vipaji vya kutisha wataonyesha maajabu yao ya kitaalamu. Kisha watu watapiga kura ni ugunduzi gani unastahili kupewa tuzo. Kisha tuzo zitatolewa.
Kila mtanzania aliyefikisha umri wa miaka kumi na nane atatoa kodi kila mwezi Tsh 2000 kama ishara ya kuwa yeye sio mvivu na aanfanya kazi. Kodi hii ni nje ya kodi nyingine kama za biashara. Hii ni kwa mtanzania yeyote mwenye kuishi na mwenye afya. Bila kujali anakazi au hana.
Itawekwa sera na ilani ya taifa kwa ujumla. Rais atakayeingia madarakani yeyote atafuata miradi atakayoikuta kwenye sera ya nchi na ilani ya nchi. Vyama vya siasa vichukue sera kutoka katika Ilani ya nchi na sio kila chama kiwe na Ilani yake.
Ilani ya nchi na sera za nchi ziwe kwa viipindi kumi kumi. Hata kama watawala watachaguliwa kila baada ya miaka mitano. Hata kama Rais ataongoza awamu moja, atakayefuata atakamilisha alipoishia mwenzake ili mradi ndani ya miaka kumi yaliyoahidiwa kwenye ilani yamefanyika.
Endapo Rais atashindwa kutimiza malengo ya ilani na Sera ya nchi ndnai ya muda husika atashitakiwa kwa kosa la kushindwa kutimiza ilani ya muda husika.
Rais atashtakiwa endapo kiwanda au mradi wowote alioukuta utakufa iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Kwani atahesabika kuwa yeye ndiye kalihujumu taifa.