From Sir With Love
JF-Expert Member
- Sep 13, 2010
- 2,076
- 3,797
Pole na Majukumu ya ujenzi wa Taifa Mhe. Rais
Nina ushauri mdogo kwako kama kiongozi wangu wa Nchi, na nishukuru mitandao ya kijamii kunipa hii fursa.
Naomba nijikite kwenye swala la "MTU MMOJA" kumtolea bastola Mhe. Nape siku alipokuwa akutane na waandishi wa habari.
Nilikuelewa ulivyosema huyo "MTU MMOJA" sio serikali, Kosa lake lisiwe kosa la serikali nzima. Nakubaliana na wewe asilimia mia moja. Ikiwezekana abebe lawama, kama vile Cleophace Simon alivyobeba lawama kule Iringa.
Kuna picha zinazunguka kwenye mitandao ya kijamii, zikionyesha wale vijana, waliokuwa wanamwomba Mhe. Nape arudi kwenye gari. Mengi yamesemwa, na mengi yatasemwa. "Vijana wetu" wanafanya kazi ngumu sana, na zingine zinawaingiza matatani kwa kujulikana kirahisi na kwa kitu ambacho kingezuiwa.
Kuna madoa kama matatu, ambayo yatakumbukwa na wananchi, kuhusiana na idara. Ni vizuri haya matukio yakawa case studies kwenye masomo.
Mosi ni swala la Ulimboka, pili ni kifo cha ofisa usalama wa taifa, Ndugu Peter Tyenyi kufia kwenye kisima cha maji pale kijitonyama na sasa swala la "MTU MMOJA" kutoa bastola mchana kweupe na kumtishia aliyekuwa Waziri wako wa habari.
USHAURI:
1. Ni vizuri unapopewa briefings za kila siku ukumbushie "vijana wetu" kufanya kazi kwa ueledi ili wananchi wasiwe na dhana potofu.
2. Kazi ya kumwomba Mhe. Nape arudi kwenye gari, ingefanywa na mtu mwenye umri mkubwa na utashi ungetumika. Waswahili wanasema mtu mzima dawa.
3. Mwaka 2011 ulipokuwa Waziri wa Ujenzi, kuna tetesi zilienea unataka kujiuzulu. Lakini baadaye hizi habari zilikanushwa. Nimekumbushia hilo kwa sababu, ungemuita Mhe. Nape, uongee naye na haya yote yasingetokea. Pamoja na hayo naheshimu uamuzi wako.
Naomba nimalizie Mhe. Rais kwamba, kuna wakati huwa tunawapa chai watoto wetu kwenye vikombe vya glasi. Ukiona mwanao amedondosha "glasi" mara mbili au tatu, basi mbadilishie kikombe na umpe cha "udongo". La sivyo Mhe. Rais utagombana na marafiki zako watakapo mwagiwa chai na mwanao kwa sababu hawezi kuhimili kutumia glasi.
Nikutakie kazi njema.
Ni mimi mwananchi wa kawaida.