Mhe.Rais Magufuli, fedha za kujikimu UDSM kizungumkuti!

mtanganyika wa kweli

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,420
1,720
Mhe.Rais Magufuli JPM,bodi ya mikopo imeendelea kuwa jipu la muda mrefu,tokea tusaini mpaka sasa bodi imeendelea kupiga danadana kuhusu kuingizwa kwa pesa za kujikimu;mpaka hiyo kesho wasipoingiza hizo fedha usishangae kuona wasomi wakiingia barabarani mpaka sehemu husika kushindikiza kwa kutumia ngumu maana hali imekuwa tete kwa sisi watoto wa wakulima!


=====================================

TAARIFA KWA UMMA

*MSIMAMO WA WIZARA YA MIKOPO UDSM*

Wizara ya mikopo chuo kikuu Dar es salaam inapenda Kutoa taarifa Kwa umma juu ya msimamo wake kuhusu fedha Za kujikimu awamu ya nne

Wizara inatambua shida na changamoto zinazowakumba katika kipindi hiki kigumu hivyo basi wizara haitafumbia macho na haitavumilia ucheleweshaji Wa fedha zetu Unaofanywa na BODI YA MIKOPO (HELS mpaka Muda huu Kwa jitihada tulizozifanya tumejiridhisha fedha zetu zimekwisha tolewa na serikali Kuu na zimeshafika BODI YA MIKOPO (HELS

Hivyo basi msimamo WA wizara ya mkopo ni kama ifuatavyo Kulingana na Muda umeshafika yaani siku 60 Za Malipo

1.Wizara imetoa masaa arobaini na Sita (46) yaani kuanzia Sasa mpaka jumatatu saa tano kamili 5:00 asubuhi fedha Za kujikimu ziwe Zimeshafanyiwa ama kufikishwa Kwa Wanafunzi husika

2 . Wizara kutambua unyeti Wa jambo hili kama bodi ya mikopo(HELS hawataidhinisha fedha Za wanafunzi ambao wanahali ngumu katika kipindi hiki Wizara itahamishia kambi BODI YA MIKOPO mpaka fedha itakaapoingizwa

Wizara ipo bega Kwa bega kutetea haki Za Wanafunzi wote wa chuo kikuu cha DSM.

Imetolewa na WIZARA YA MIKOPO UDSM

KASUNZU Eliud
0658202828

Makupa Erick
0655191254

Mahmud Abdul Nondo
0762599672
 
Mmeanza masomo semister ya pili tarehe 26 March sasa inakuwaje mseme mmecheleweshewa malipo.
 
Back
Top Bottom