Mhe. Rais Magufuli, dhana ya 'Tanzania ya viwanda' itekelezwe hivi

NEWLY

Member
Sep 1, 2015
13
12
MH. RAIS JPM, TANZANIA YA VIWANDA IFANYWE KWA NAMNA HII..

Dhana ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ni nzuri sana na napenda kuunga mkono, lakini utekelezaji wake unahitaji fikra mpya na jitihada mpya zenye msukumo wa kizalendo na nchi yetu. Naomba nitoe mchango wangu kwa baadhi ya mikoa namna ya uanzishwaji wa viwanda kama ifuatavyo.

A. MIKOA YA KANDA YA ZIWA: Kwa kuwa katika mikoa hii pamoja na mambo mengine kuna shughuli za uvuvi, naomba ushirikishe wadau ili vianzishwe viwanda vya kusindika samaki. Lakini jambo hili litawezekana kwa kushirikiana na wavuvi, wadau na wafanyabiashara wakubwa.

Kabla ya yote hapa inafaa kuandaa (workshop trainning) yaani mafunzo kwa wavuvi na wadau wengine ili wapate elimu ya kutosha namna ya kuvua samaki kwa kutunza pia samaki wadogo ili kuwe na ustawi endelevu wa samaki. Baada ya trainning, ni kwamba sasa yafaa kuandaa mazingira ya kuanzisha viwanda vya kusindika samaki pamoja na mabaki ya samaki ambayo ni zao la mwisho litatumika kutengeneza chakula cha mifugo.

Naamini kwa kushirikiana na wadau kanda ya ziwa itakuwa na viwanda vya samaki ambavyo mbali na kuwezesha kusindika samaki pia vitazalisha ajira nyingi sana.

B. MIKOA YA JAMII ZA WAFUGAJI: Katika mazingira haya ya jamii za wafugaji, jambo la kwanza ni kuanzisha mafunzo kwa wafugaji kufuga kisasa, pili kuwashirikisha namna ya kuvuna mazao ya mifugo kwa lengo la kukuza kipato kwa familia zao na taifa kwa ujumla, baada ya kufanikisha hilo katika mazingira hayo, vitaanzishwa viwanda vya kusindika nyama, pia vitaanzishwa viwanda vya kutengeneza vifungi, mapambo, na vyombo vya udongo kwa kutumia kwato za ng'ombe na mifupa ya ng'ombe, mbali na hilo, tutatumia manyoya na ngozi za wanyama hao kujenga viwanda vya viatu, ni jambo ambalo litawezekana kama tutatenda kwa uzalendo na kutanguliza maslahi ya taifa mbele.

C. MIKOA YA SINGIDA NA DODOMA PAMOJA NA ILE INAYOLIMA ALIZETI KWA WINGI: Katika mikoa hii jambo ka kwanza ni kuwatrain wakulima wa alizeti na kuwapa mbegu bora za alizeti pamoja na vitendea kazi, baada ya kufanikisha hilo ni kuwapa kila mwananchi angalau shamba la ekari kuanzia tano ili wazalishe alizeti kwa wingi.

Baada ya kufanikisha hilo, vijengwe viwanda vikubwa vya alizeti na kutengeneza mafuta bora kabisa ambayo yatauzwa ndani na nje ya nchi, lakini jambo hilo lifanywe pia katika mikoa ya kikimo cha karanga kwa utaratibu huo huo. Naamini jambo hilo litazalisha ajira nyingi, wananchi watakuza kipato na nchi itakuwa kiuchumi na kuondokana na utegemezi. Niko tayari kutoa ushirikiano kwa hilo maana nimefanya utafiti binafsi nikaona inawezekana.

D. MIKOA YA KILIMO CHA TUMBAKU YAANI TABORA, RUVUMA N.K - Kwanza zao hili ni miongoni mwa mazao yanayowatesa sana wakulima na kuwafanya waishi maisha duni sana licha ya zao hilo kuwa na thamani kubwa. Sasa basi ili kuwasaidia wakulima hawa wa tumbaku, napendekeza viwanda vya tumbaku vijengwe katika mazingira ya wakulima, na pia wakulima wakopeshwe moja kwa moja na bank au serikali badala ya makampuni ya Tumbaku, maana hayo makampuni yanawanyanyasa sana na wanateswa sana.

Viwanda kujengwa maeneo yanayolima tumbaku yatalifanya zao liwe na thamani zaidi, pia itawafuta madalali wote wa tumbaku pia ajira nyingi zitazalishwa katika mikoa hiyo.

E. MIKOA INAYOLIMA MAHINDI NA MPUNGA KWA WINGI (MOROGORO, IRINGA, MBEYA, RUKWA, RUVUMA, NJOMBE N.K) - Katika mikoa hiyo kwanza ni kugawa ardhi kwa kila mwananchi, pili kutoa mafunzo na pia kuwashirikisha wadau na wataalam wa kilimo na wahandisi, baada ya kufanya hivyo, kuandaa mpangokazi madhubuti wa kuanzisha viwanda vya kusaga unga na vile vya kumenya mpunga(Milling Industries).

Hapa unaweza kutuma watu kadhaa kwenda vietnam kupata mafunzo maana wavietnam wako vizuri sana katika eneo hilo. Sasa mbali na viwanda hivyo kuzalisha unga na mchele lakini pia kuna pumba za mahindi na pumba laini ya mpunga yaani (bran meal), katika mazingira hayo hayo vitajengwa viwanda vya biskut ambazo zitatengenezwa kwa kutumia pumba lain ya mpunga na pumba ya mahindi.

Sambamba na hilo pia kwa kutumia pumba ngumu za mpunga yaani Husk utajengwa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia steam ya pumba hizo. Naamini kwa kiasi kikubwa tutapiga hatua.

F. MIKOA INAYOLIMA MITI YAANI IRINGA, MBEYA, N.K - Katika mikoa hiyo kwanza kabisa ni kutenga mashamba kwa kilimo cha miti pia kutoa elimu kwa umma juu ya kilimo hicho na namna ya kuitunza .Baada ya hapo kushirikisha wadau na wataalam wa ndani na nje ili kuanzisha viwanda vya mazao hayo.

Hivyo basi, kwa kutumia mazao hayo vitaanzishwa viwanda vifuatavyo;

Viwanda vya mbao, viwanda vya vijiti vya kuchokonolea meno (tooth-pick) na viwanda vya karatasi..

Aina hizo za viwanda zitazalisha ajira, pia tutapata bidhaa za kuuza nje ya nchi na uchumi wetu utakua kwa kasi sana.

Mhe. Rais JPM, kwa leo naishia hapo. Sehemu ya pili nitakuja na mpango wa viwanda vya aina nyingine.

NB: Ili hayo yawezekane, serikali yako ipeleke umeme na maji katika kila mkoa kwa uhakika zaidi.

Mwalimu Sadick Francis Masilu,
+255 686 018 006
smasilu@yahoo.com.
 
Umeme pia usambazwe na uwe wa uhakika vinginevyo itakuwa ni hadithi za Siku zote.
 
Wanajukwaa tukumbuke kuwa Dr. Magufuli wakati anagombea uraisi aliahidi viwanda japo hakusema viwanda hivyo vitajengwa kwa muda gani na kwa vyanzo gani vya mapato.

Kwa uongozi wake huu wa kubana matumizi, kutumbua majipu, kuboresha ukusanyaji wa kodi na kuimarisha utumishi wa Umma, uhakika wa Tanzania kuwa nchi ya viwanda ndani ya miaka 10 inawezekana tofauti na ahadi za aliyekuwa mgombea wa ukawa.

Aliyekuwa mgombea wa ukawa ndugu Edward Lowasa aliahidi kuwa angetumia gesi ya Mtwara kujenga viwanda, kama ndo ulikuwa mpango wake, basi viwanda vingekuwepo miaka 100 ijayo.

Mheshimiwa Lowasa atulie alishindwa kuwashawishi wananchi wampe ajira ya kuwatumikia, aendelee kukitumikia chama chake kipya, na zaidi aendelee kufadhili VICOBA kama alivyokuwa anafanya awali maana ameacha kufanya vitu vingi alivyokuwa anavifanya kabla ya kugombea uraisi ambavyo vinatafsiriwa na kutoa ushahidi kuwa alikuwa anavifanya kwa nia ya kushawishi waje wampe uraisi. Aendelee kufanya harambee mbalimbali.
 
Kama jpm unaona anaweza kipi kingemshinda lowasa,jpm anacheza na madagaa mapapa anayaacha
yatafikiwa tu hasa hilo babalao la mapapa kwasababu angeanza na hilo babalao angeharibu kwani lenyewe linashirikiana na hivyo vidagaa
 
Hivi hiyo miaka 10 ikipita kama miaka 10 ya JK ilivyopita bila kuwapo na hata Kiwanda kimoja mtasema nini?

Amini nakuambia JPM amepewa kipawa cha kutumbua Majipu tu!
Na hapa ndipo atakapo fanya vyema na Kukumbukwa sana na watanzania atakapo maliza utawala wake.


Rais ambaye mwenye kuweza kujenga Viwanda hapa Tanzania sio yeye ni mwingine Kabisa....
 
Umewahi mapema sana. huna hela ya chai. ofisini za Lumumba bado hazijafunguliwa.
hivi chadema wameshindwa kujenga ofc ama ni masharti ya mungu wao waliyeanza nae kuwa hawaruhusiwi kujenga ofc bali wapange zaidi ya miaka 20?
 
Hivi hiyo miaka 10 ikipita kama miaka 10 ya JK ilivyopita bila kuwapo na hata Kiwanda kimoja mtasema nini?

Amini nakuambia JPM amepewa kipawa cha kutumbua Majipu tu!
Na hapa ndipo atakapo fanya vyema na Kukumbukwa sana na watanzania atakapo maliza utawala wake.


Rais ambaye mwenye kuweza kujenga Viwanda hapa Tanzania sio yeye ni mwingine Kabisa....
kwa namna matumizi yanabanwa viwanda lazima mkuu
 
Kama jpm unaona anaweza kipi kingemshinda lowasa,jpm anacheza na madagaa mapapa anayaacha
Mpaka atakapo mshughulikia Mleta mabariko kwa kuzungusha mikono kwenda nyuma ndipo utakapoamini kuwa hakuna fisadi atakayebainika akabaki salama.
 
Viwandwa vitajengwa nina imani na magufuli. Sasa hivi tumuache atumbue majipu kwanza akimaliza atageukia uchumi
 
Hapa naona umeshaona kwa mwendo huu kutoboa kwenye viwanda kwa miaka hii mitano ya awali ni ndoto,sasa umeanza kutafuta justification mapema ili hii miaka mitano ikipita,wananchi wakihoji muwe na la kusema,nalo ni mlikuwa mnatengeneza mazingira sasa awamu ya pili ni viwanda.Wadanganyika watawaelewa kama ilivyo kawaida,miaka mingine mitano itaisha na mtakuja na wimbo mwingine!
 
Hapa naona umeshaona kwa mwendo huu kutoboa kwenye viwanda kwa miaka hii mitano ya awali ni ndoto,sasa umeanza kutafuta justification mapema ili hii miaka mitano ikipita,wananchi wakihoji muwe na la kusema,nalo ni mlikuwa mnatengeneza mazingira sasa awamu ya pili ni viwanda.Wadanganyika watawaelewa kama ilivyo kawaida,miaka mingine mitano itaisha na mtakuja na wimbo mwingine!
kwani unaelewa nimi mtu akisema ndani ya miaka 10? Au miaka 5 haipo ndani ya miaka 10?
 
Mpaka atakapo mshughulikia Mleta mabariko kwa kuzungusha mikono kwenda nyuma ndipo utakapoamini kuwa hakuna fisadi atakayebainika akabaki
salama.


Majipu ni suala ambalo limesababishwa na mfumo ukianza kumchunguza kila mtu kwa ndani hakuna kiongozi yeyote wa Ccm au aliyekuwa kwenye utawala atakayebaki.
 
Back
Top Bottom