Pasco, are you serious? Unataka wanyongwe ama unataka JPM asaini? Kuna uzi mwingine pia umejaribu kusema kuwa huruma ya JK ni udhaifu hasa kwa kutopenda watu wanyongwe! Kwa Mantiki hiyo Nyerere alikuwa dhaifu sana kwa kuwa aliidhinisha unyongwaji muuaji wa rafiki yake Dr. Kleruu na Mkapa pia alikuwa dhaifu zaidi kwa kuwa hakuidhinisha unyongwaji. Madikteta wote wanashabikia unyongwaji na kwa kweli ni wauaji!
Nilimsikia Nyerere katika hotuba yake moja akieleza kwanini hakupenda wakosaji waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa wanyongwe. Alisema kuwa mkosaji huyu amehukumiwa kunyongwa kwa kuwa alimuua mtu. Na hilo ni kosa kubwa sana lenye adhabu ya kiwango kikubwa sana. Alisema, "Mimi nikiruhusu kuwa mkosaji huyu anyongwe, maana yake na mimi nafanya kosa lile lile alilofanya! Aliua mtu na mimi naruhusu kuwa auwawe kwa hiyo tuko sawa hapa. Wote ni wauaji. Sheria si kigezo kwa kuwa sheria hizi tumetunga sisi, na kwakweli mwenye ruhusa ya kuuondoa uhai wa mtu ni yeye aliyeuweka ambaye ni Mwenyezi Mungu!" Pia alitoa sababu nyingine kuwa mtu akiua mtu, taifa limepoteza raia mmoja. Tukiruhusu aliyeuwa naye auwawe maana yake taifa linapata hasara ya watu wawili. Lakini pia nani aliyewahi kuonja mauti akarudi ili atuambie kuwa adhabu ya kumuua mtu inalingana na kosa lake la kuumuua mtu?
Huenda huo ndio ulikuwa udhaifu wa Nyerere na ndio udhaifu(?????) wa Kikwete! Ila mimi naamini kuwa kumsamehe mtu ni moja ya evidence za maturity. Mtu dhaifu hawezi kumsamehe mtu. Ni mtu mjasiri tu na mkomavu wa nafsi ndiye anayeweza kusamehe. Ni ngumu sana kwa mwanaume mdhaifu kumsamehe mkewe anapokosea. Ni mwanaume mkomavu tu ndiye awezaye! Tabia za kulipiza kisasi, ubabe, kutumia nguvu badala ya hoja, kuamrisha badala ya kujadiliana na kutumia nguvu ya ushawishi, kuzira, kulalamika, kusingizia wengine, kutokuwajibika n.k. zinaonyesha kuwa mhusika ni dhaifu kwa ndani na kwa nje ana compplement udhaifu huo na udikteta. Kikwete hakuwa dhaifu!!!