Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,770
- 121,817
Wanabodi,
Kiongozi mzuri ni yule anayeyaishi maneno yake, yaani ku "practice what you preach". Ile preaching ya jana ya Rais Magufuli kuomba Watanzania wanaohukumiwa kifo Wanyongwe tuu, imenigusa na kumshauri ayaishi maneno yake kwa kuanza na hawa wa nyumbani waliohukumiwa kunyongwa mpaka wafe, mafaili ya hukumu zao, yako mezani kwake yakisubiri tuu saini yake,adhabu zao zitekelezwe.
Adhabu ya kifo ndio adhabu kubwa na kali kuliko adhabu zote, mtu akiishahukumiwa adhabu hiyo, huwa haitekelezwi mpaka rais asaini hati ya kifo ya utekelezaji wa adhabu hiyo inayoitwa "death sentence".
Rais anakuwa huru kusaini ama kutosaini, hivyo katika kipindi chá miaka 23 ya utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, inasemekana alisaini hati mbili tuu, moja ni ya Mwamwindi, aliyemuua Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kleruu, na ya pili ni ya mhindi mmoja aliyemuua mke wake, kisha kuuweka mwili wake kwenye gari, kisha kulisukumia bondeni ionekane ni ajali ili alipwe bima nono!.
Mwinyi katika kipindi chake cha miaka 10,anasemekana alisaini hati kadhaa na watu wakanyongwa hadi kufa.
Mkapa katika kipindi chake chote haikutolewa taarifa kama aliwahi kusaini hati yoyote ya kifo.
Kikwete kiukweli kwa jinsi alivyokuwa dhaifu kwenye mambo makubwa, sidhani kama angeweza kusaini, hata angetaka kusaini, mkono ungetetemeka!.
Udhaifu wa Kikwete ulianzia alipo wasamehe wale watuhumiwa wa EPA.
Kuonyesha alivyo dhaifu rais Kikwete aliwaombea msamaha Watanzania waliohukumiwa kifo nchini China kwa kukutwa na madawa ya kulevya.
Mpaka sasa Kuna mamia ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa tangu enzi za Nyerere ambao hukumu zao hazitatekelezwa zikisubiri saini ya Magufuli.
Marais tangu Nyerere, Mkapa na Kikwete (Mwinyi alisaini), walishindwa kusaini kutokana na udhaifu wa mioyo yao, walikuwa na roho yepesi zenye huruma hivyo kulitia taifa hasara kubwa kutokana na udhaifu wao.
Wafungwa hawa, hawaruhusiwi kufanya kazi yoyote kule gerezani, kazi yao ni kula na kulala tuu. Sasa just imagine hasara wafungwa hawa wanavyolisabishia taifa.
Zaidi ya kula bure na kulala bure, na kuvaa bure, bado wakiugua wanatibiwa kwa gharama kubwa hadi wapone, kwa vile wameisha hukumiwa kifo kwa kunyongwa hadi wafe, wakiugua kwa nini wasingeachwa tuu waugue hadi wajifie zao, na kehesabu hiyo ni kazi ya Mungu, au hata kupewa sumu very lethal poison, wanakufa faster na watuondolee msongamano magerezani.
Zaidi ya kula na kulala bure, pia wanapoteza nguvu kazi kubwa ya taifa, kuwalinda 24/7. Kila mfungwa wa kifo anafungiwa jela ya chumba cha peke yake na kila mmoja anatumia walinzi watatu wa shift za masaa 8 kila siku.
Kama hilo halitoshi taifa linaendelea kupata hasara kwa ku train wanyongaji wanaolipwa mshahara wa bure bila kufanya kazi yoyote ya kunyonga!.
Tunapoteza, fedha nyingi kununulia vifaa vya kunyongea na kuvi maintain muda wote hadi vinachakaa bila kutumika.
Hivyo kwa tangazo la jana la Rais Magufuli kutaka Watanzania waliohukumiwa kunyongwa huko nje wanyongwe, hii inaonyesha rais Magufuli ni rais jasiri na asie muoga muoga na dhaifu kama watangulizi wake, hivyo nashauri kabla MFA haijatuma Note Verbale nchini China kuruhusu Watanzania waliohumiwa vifo wanyongwe, aanze kwa kusaini hati za vifo zilizoko mezani kwake kwa haraka haraka kama alivyosaini ule muswada wa habari.
Kwangu mimi hili limekaa poa, waliohukumiwa kunyongwa mpaka wafe, wanyongwe tuu wafe, jee wenzangu hili mnalionaje? .
Paskali
Update.
Kwa vile mimi ndio mwanzisha mada, na kuna mada mtu unaanzisha with the motive behind, amini usiami, mada kama hizi zimesaidia sana kuleta mabadiliko na the desired changes, sasa imebaki kufutwa tuu rasmi kwa adhabu ya kifo, toka kwenye vitabu vyetu vya sheria.
Thanks for changing for the better.
Paskali
Rejea
Idadi ya walionyongwa tokea uhuru Tanzania ni 232
Idadi ya wanaosubiria kunyongwa yafikia 465
Mamia wanasubiri kunyongwa nchini