duocore
Member
- Aug 27, 2012
- 55
- 4
Natoa hongera zangu kwa Mhe. Dkt. John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni siku chache tangu aapishwe katika nafasi hiyo na mabadiliko yameanza kuonekana.
Hivi sasa kuna mkutano wa kimataifa unaendelea huko Paris kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi. Mhe. Rais nchi yetu pamoja na kuanza kupata athari za mabadiliko ya tabia ya nchi lakini bado mungu ametujalia kupata mvua kwa kiasi.
Mimi kwa mtazamo wangu hatujafikia kiwango cha kupata athari kubwa (significant) kwa kiasi hicho. Mhe. Rais kwa utashi wa kisiasa ulionao nashauri kwa mvua kidogo tunazozipata viongozi katika maeneo yao wapande miti kwa kasi.
Pia tutumie nguvu kazi iliyopo magerezani kama sehemu ya kurekebisha tabia ya wafungwa kulitumikia taifa wa kupanda miti, kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Pia Mhe. Rais suala la mrahaba unaotolewa na makampuni mbalimbali kama Corporate Social Responsibility imekuwa ni kama hisani wakati ni suala la lazima.
Nakutakia utekelezaji mwema wa kazi za kuwatumikia wananchi wa Tanzania. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania:lock1:
Magufuli Hoyeee!!