Mhe. Mengi ondoa tangazo la kulazimisha ngono ITV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Mengi ondoa tangazo la kulazimisha ngono ITV

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbwambo, May 28, 2012.

 1. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Nina uchungu mkubwa kuona kwamba mheshimiwa Mengi anakubali kutangazwa tangazo lakulazimisha ngono litangazwe kwenye kituo chake cha itv.

  Mheshimiwa , mimi nakuamini kwamba una heshima na unapenda uelemeishe jamii sambamba na kusadia jamii katika michango mbali mbali ya maendeleo yao. Na sikuamini kuona umetoka kupewa tuzo kubwa sana hivi karibuni ambalo unastahili lakini unakubali jamii yako ya kitanzania ifedheheshwe kwa tangazo la kulazimisha ngono. Kweli watu wengi tumejisikia vibaya sana kwamba kweli jamii imeelimishwa au watoto na vijana wamefundishwa jinsi wazazi wao wanavyolazimishana kufanya tendo hilo? Kweli linatolewa tena kwenye vipindi vya taarifa za habari ambapo sisi walala hoi hatuna tv zetu wenyewe na watoto zao wenyewe hivyo inapokuja taarifa ya habari saa mbili mimi nakosa raha na ninashindwa hata kuondoka nitaona wapi taarifa ya habari?

  Nakuomba mheshimiwa Mengi ondoa tangazo hilo haliwasaidii watoto na vijana wa kitanzania
  ninakuheshimu sana na ninapenda sana itv kuliko tv zingine
  naamini utaliondoa kwa busara zako nyingi ulizo nazo
  asante na mungu akubariki
   
 2. c

  chakarikamkopo Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu katika ulimwengu huu watoto huwezi ukawaficha haya masuala na ukaamini hawatafahamu hilo Tangazo hata wao pia linawahusu maana nao ni wanandoa watarajiwa. Miaka ya sasa ni tofauti kabisa na miaka ya zamani tulikuwa tunadanganywa kwamba watoto hutolewa chini ya mwamba Mkubwa na tulikuwa tunaamini mpaka tukiwa na Umri wa miaka 10+. Leo hii mdanganye mtoto ujinga huo atakuchora tuu maana anafahamu fika ili mtoto azaliwe lazima watu wawili wa jinsia tofauti wajamiiane.
   
 4. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  teh teh teh duuu mkubwa umenikumbusha mbali sana .Watoto tulidanganywa sana aiseee
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hata mi najiskia vibaya sana nionapo tangazo hilo pembeni yuko Mkwe, mtoto, mume yani ni aibu na utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana, TUSIENDELEE KUFUMBIA MACHO MMOMONYOKO HUU WA MAADILI.
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  .
  Akili za namna hii ndizo zilizoshusha miaka ya kuishi ya binadamu mpaka sasa wastani wa kuishi wa baazi ya nchi umefikia miaka 35 kutoka 900 ya kina Adamu.
  Kwa nini tukubali kuwa waovu? Uovu ni mambo mema ambayo mtu anafahamu kuwa anapaswa kufanya, lakini hata hivyo hafanyi. Tunafahamu kuwa kuna haki ya kuwalinda watoto wetu na masuala ambayo hawapaswi kuyafahamu kwa ujuzi wake kabla ya wakati wao yaani umri unaoruhusu. Mojawapo ya mambo hayo ni suala la mahusiano ya ngono. Ni kweli kwamba kuna vipindi ambavyo tunawalinda watoto wetu wasivifuatilie katika Tv. Sasa hata taarifa ya habari tuwahami wasifuatilie? Maana ndiko mlikopeleka hili tangazo lisiloheshimu mila na utamaduni wetu sisi waafrika tuwapo na familia zetu zilizochanganyikana.
  Kingine ni Uasi. Uasi ni mambo ambayo tunafahamu hatupaswi kufanya lakini hata hivyo tunayafanya. Sii kweli kwamba Mengi na ITV hawajui kuwa hawapaswi kujjadili ama kuashiria ashki za kingono mbele ya under age. Hivyo kutekeleza vitendo hivyo kwa Mengi na Tv yake mbele ya under age ni uasi. Ni uasi kwa mila zetu, ni uasi kwa tamaduni yetu na ni uasi kwa ulinzi wa watoto wetu. Maana yake kuliweka tanzazo hili ndani ya mda wa Taarifa ya habari ni nini?
  .
   
Loading...