Mhe Mbowe angeshinda kwa 100% angepimwa utendaji wake

Mhe Mbowe angeshinda kwa 100% angepimwa utendaji wake

emgitty06

Senior Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
141
Reaction score
26
Chaguzi zimekwisha sasa, kazi kubwa ambayo watu wengi wanaifanya kwa sasa ni kufanya tathimini ya kilichotokea wakati wa uchaguzi, wengine bado wanamaumivu ya kushindwa kupata fursa ya kuonyesha uwezo na umahiri wao wa kukiongoza chama kwa nafasi walizoomba huku wengine wakiwa na shangwe kubwa kwa kutimiza ndoto zao.

Kila nafasi ilikuwa na changamoto zake, si BAVICHA, BAWACHA wala BARAZA LA WAZEE kote kuliwaka moto. Hii ilikuwa ni salamu tosha kwa wale wote waliodhani CHADEMA inaweza kuondoshwa ama kuyumbishwa kwa fitina za wachache wasioitakia mema Tanzania. Lakini pia ilikuwa ni salamu tosha kwa watawala kwamba CDM sasa imeiva na iko tayari muda na wakati wowote kuwapokea kulisukuma gurudumu hili la kuwaongoza watanzania.

Kama kuna nafasi ilikuwa ikiwanyima watu usingizi basi ni nafasi ya MWNYEKITI WA TAIFA wa chama. Kila mmoja alitolea macho hapo kujua nini kitajiri iwe kwa kuombea mabaya yatokee ama kuombea mema ili CDM isonge mbele.


Wapo waliojitolea kwa umasikini wao kumchukulia fomu waliyemwona tumaini lao huku wengine wakikimbia mbio kwa msajili ili kuweka mapingamizi. Yote haya yalikuwa yanafanyika huku kila mmoja akijaribu kulinda na kukitetea anachokiamini.

Wenye nguvu wakashinda, msajili alikosa nguvu kwa kukosa hoja za msingi. Kila mmoja alitolea macho hapo kujua nini kitajiri iwe kwa kuombea mabaya yatokee ama kuombea mema ili CDM isonge mbele.



Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo.

Mwenyekiti,
Kura zilizopigwa………….811
Freeman Aikael Mbowe…….789 sawa na asilimia 97.3%
Gamba Mong’ateko……….20.sawa na asilimia 2.466%
Kura zilizoharibika …………..2


Matokeo haya ndiyo yaliyowafanya watu wenye akili mgando kufikiri yasiyofikirika. Wengi wao wakiangalia kura 20 alizopata bwana Gamba wakasahau asilimia tisini na saba(97.3%) za ushindi wa mhe Mbowe.

Wengine wakasema Mbowe hafai kwa kuwa watu ishirini hawakumpigia kura huku wengine wakisema Mbowe angegombea na Fulani asingeshinda. Anyway sitaki kufanyia kazi hisia za kila mmoja ila mimi pia nilikuwa na mtazamo wangu juu ya matokeo haya haya.


Nilikuwa nikijiuliza ikitokea Mhe Mbowe akishinda kwa asilimia zote(100%) jamii yenye kufikiri kwa mapana ingefanya hitimisho gani? .hivi ni kweli wakati wa uongozi wake alikuwa anafanya maamuzi yaliyokuwa yakimridhisha kila mwanachama?. Jibu ni hapana. po waliokuwa wanakerwa na namna alivyokuwa akifanya maamuzi, wapo waliowahi kuumizwa na maamuzi yake wala wasitamani kumuona tena akiendelea kuwa mkuu wao, na wengine walimchukia tu bila hata sababu za msingi. Hawa wote wakipewa fursa ya kuongea sirini bila yeyote kufahamu ni lazima tu wasimpigie kura, na hata angekuwa peke yake kwenye kinyang’anyilo hicho basi wangepiga kura ya hapana ili kutuliza machungu yao.


Kama watu walifanya maamuzi yao sirini na bado akaibuka kidedea kwa asilimia nyingi namna hii ni dhahili kwamba idadi kubwa ya wanachama iman yao kubwa sana wameiolekeza kwake na hawataki kabisa kuukosa mchango wake kwenye chama hasa katika kipindi hiki cha lala salama. Na huu ni msumari tosha kwa wapinzani waliondani ama walio nje ya chama.


Mwisho kabisa naomba nichukua fursa hii kumpongeza mhe Mbowe kwa kuwa mwadilifu na mzalendo kwa chama na nchi yake, nimpongeze pia rafiki yangu Said Mohamed kwa kushinda nafasi ya makamo mwenyekiti Zanzibari, Profesa safari upande wa bara, DR Wilbroad SLaa kwa kuendelea kuwa injini ya chama, JJ Mnyika kwa kuwa naibu katibu bara, Halima Mdee(bawacha), paschal patrobass(bavicha),na viongozi wengine wote.


Mungu ibariki CHADEMA.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom