Mhe. Magufuli kwa hili hatupo pamoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Magufuli kwa hili hatupo pamoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babu M, Feb 1, 2011.

 1. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Magufuli amekuwa ni kati ya mawaziri wachache ambao utendaji wao umekuwa ni wakuridhisha.Wiki hii tumeona amefanikiwa kuliokolea taifa zaidi ya billion 5 kutoka kwenye malipo hewa. Wakati akiwa anafichua ufisadi huo alielezea pia kuhusu ulipaji wa fidia, ambapo kuna sehemu niliona amepotoka . Nina mnukuu “Kama nyumba yako imeingia nusu ndani ya eneo la barabara, itabomolewa hiyo nusu na wewe utalipwa kulingana na ulivyobomolewa, hatuwezi kulipa gharama ya nyumba nzima wakati umebomolewa nusu”

  Kwanza haya ni makosa ambayo yameanywa na serikali kwa tamaa za watu wachache kukiuka taratibu zilizopo ili kujinufaisha wao wenyewe.Watu kama awa matokeo ya udhalimu wao awatakaa wayaone na labda wanaishi happy life Mbezi beach.

  Waliouziwa viwanja nusu kiko kwenye eneo la barabara ni binadamu kama sisi, na sio mashine uneyoweza kuiprogramu ifanye jinsi unavyotaka,.Ni watu ambao wamekuwa wanaanya kazi kwa bidii na wakafanikiwa kutimiza ndoto zao za muda mrefu.

  Sasa leo unakuja kuwaambia nitakulipa fidia nusu ya aka kabafu,sebule,jiko na chumba cha watoto .SIO HAKI KABISA. Kwa nini isiwe f idia ya nyumba nzima na pesa za usumbufu ili start from the scratch na kuishi life ambayo walikuwa wameipangilia toka mwanzo.

  Mbona wasijifunze kwenye swala la Radar tulilipa £28m lakini tukalipwa fidia ya £30m na radar tunabaki nayo.
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  basi mshitaki hizo city council waliowapa land! kwani huo uwezo hamna?
   
 3. e

  ezra1504 Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu mji una ramani tangu wakati wa mkoroni, so wanaposema hifadhi ya barabara ni kwa wale tu ambao wamejenga majumba na kuyatanua mpk maeneo ambayo ni restricted kwa ajiri ya barabara. Ndo maana wamesema kuna mtaa nadhani Yombo huko, wao watalipwa in full kwa sababu barabara imewakuta na wao hawakuifuata. Nadhani hiyo ndo idea ya Magufuri.
   
 4. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  binafsi, huyu mzee simkubali kabisa. Ana kiherehere tu,na mtu wa kupenda sifa machoni kwa watu huku akiwakandamiza walio chini yake...pia ni just another fisadi. Muda ukifika atakapotaka kwenda ikulu tutayaweka bayana wananchi wamjue.

  inashangaza kuona makosa na gharama ya ama wizara husika,ama halmashauri ama manispaa husika wanabebeshwa wananchi walalahoi pekee; kwani hao waliotoa vibali wako wapi? kwanini na wao wasiwajibishwe? mnaogopana eeh

  kwasababu mtu unakuta ana file lililopita kwa viongozi husika wote, kalipa kodi zote..eti ghafla barabara inapita chumbani kwake?! Jamani..au kwakuwa yeye ndio analala hapo, na nyie mnalala huko mnapolala
   
 5. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Mwacheni afanye kazi. wewe unajenga barabarani unategemea nini?
   
 6. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Alichosema ni magufuli ni sawa kabisa. Kama hukubaliani ni wewe na si wananchi wote.

  Wengi ya watu waliojenga barabarani wamejenga maduka, bar, fremu na masuala mengine yahusuyo biashara na walifanya hivyo wakijua fika kuwa ipo siku watabomolewa. Sioni sababu ya kulalamika, tena hata kulipa hiyo nusu amefanya fea lakini hawakustahili malipo kabisa.

  Nitoe mfano mmoja: pembezoni mwa barabara ya morogoro kushoto na kulia yaliwekwa mabango makubwa (enzi magufuli akiwa waziri wa ujenzi) yanayoonesha mipaka ya barabara tena yalikuwa yanaeleza kuwa hairuhusiwi kufanya shughuli yoyote katika eneo hilo la hifadhi ya barabara ikiwemo kujenga. Badala yake watu waliendelea kujenga huku mabango hayo nayo yakiendelea kuwapa onyo; walijifanya hawayaoni au walitegemea nini?
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  wacha utanuzi ufanyike sio kila mahali duka,grocery,salon,bar na vibanda vya chips...bila utawala wa sheria jiji lote litakuwa vichochoro
   
 8. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Anti- Hebu weka simile kidogo. Hivi unajua maana ya mwanasiasa? Unasema kiherehere. Siasa ni kuonekana machoni mwa watu ukitenda mema. Ni yupi anayekufaa wewe? Nani Kawambwa, anayepwaya kila aendako?

  Usahihi hautokani na sahihi ulizopata kukupa nafasi ya kujenga bali pia ni kwa kiasi gani wewe binafsi ulitafuta uhalali wa hiyo nafasi. Ni jukumu lako wewe muhusika kutumia ufahamu wako kuona kama hiyo ni nafasi halali. Nafasi haiwezi kuwa halali kwa sababu ya sahihi ya rais tu! lakini,

  Kumbuka kuna watu wanatafuta nafasi hizo kwa kuwa-influence watendaji ili wapate sahihi hizo. Ikifika kwa magufuli, imekula kwako. Si ulimuona huyo jamaa aliyetaka kumushitaki Tibaijuka, yuko wapi? unalikumbuka lile ghorofa lililopigwa nyundo kule karibu na Golden tulip?
   
 9. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  un,mkubali nani? Asante kawambwa? Acha uzandiki..
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Huyo Magufuli ana huruma sana, ilitakiwa aliyevamia eneo la barabara awajibike kulipia gharama za kuvunjiwa!
   
 11. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Kwanza hata kama wanakulipa hiyo nusu wamekuhurumia sana ulipaswa uvunje mwenyewe harafu ulipe gharama za usumbufu. Watu wanapimiwa viwanja halali halafu wenyewe wanatanua mpaka barabarani hebu tuache unafiki bwana! Hamjaona mijini watu wanavyojiongezea viwanja kwenda ndani ya hifadhi ya barabara? Kama hilo atalifanya mimi namfagilia na aendelee hivyo hivyo! Watu hatuna adabu na nchi yetu bwana!!

  Lazima watu tuheshimu sheria zilizopo! Tena hata hiyo fidia ya nusu amewahurumia sana mlitakiwa kutopata kitu hapo maana mmeingilia barabara. Magufuli tunakuomba uchape kazi!!
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,729
  Likes Received: 4,948
  Trophy Points: 280
  ..kama mtu amevunja sheria na kujenga barabarani basi jengo lake linapaswa kuvunjwa bila fidia, na mara nyingine inawezekana mvamizi huyo alipishwa faini kwa makosa yake.

  ..ninachoomba kuuliza huu utaratibu wa kulipa nusu au robo ya gharama za jengo lililovunjwa upo KISHERIA au Magufuli anataka kuanzisha utaratibu wake mwenyewe?

  ..ubabe wa Magufuli ulisababisha serikali kulipa faini ya shilingi bilioni 15 kwa mmiliki aliyevunjiwa kituo cha mafuta kule Mwanza.

  ..naona JK ameona mapungufu ya Magufuli kwenye kufuata sheria hivyo akamteua Dr.Mwakyembe, mzamifu ktk masuala ya sheria, kuwa naibu waziri wa ujenzi.
   
 13. k

  kayumba JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Kama kiwanja kipo barabarani kweli ni haki kilipwe?

  Kama nyumba ipo kwenye eneo la barabara nionavyo mie si halali kulipwa kwa sababu watu wengi watakuwa wanajenga kwenye barabara.

  Magufuli anatimiza matakwa ya sheria, kama anatenda kinyume cha sheria basi watu wana haki ya kwenda mahakamani na fidia zitalipwa!


   
 14. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Big up magufuli pia eti utakuta mtu kaweka ukuta ina maana hapo ndio mwisho wa kiwanja chake, ajabu nje ya ukuta anajenga bustani na kuweka minguzo hadi barabarani. wananchi tuwe wastaarabu kama unataka bustani kwa nini usiweke ndani ya fensi yako?

  Nampongeza sana huyu magufulu
   
 15. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Sheria inasemaje? Magufuli yupo makini sana na suala la sheria. Jiridhishe kwanza ndipo upinge.
   
 16. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Tatizo ya hizi hela za kupata kwa deal. Watu wanajenga bila kufuata sheria ilmradi wana pesa. Sasa akiingia kiongozi anayefuata sheria ndo wanaanza kuhaha. Mimi kwa upande wangu nadhani inabidi watanzania tubadilike. Tufuate sheria maana hizi sheria hata kama hazitumiki zipo kwenye vitabu. Akitokea mtu wa kuzitumia wengi tutaumia.

  Mi naimagine mtu kama yule jamaa wa Landmark Hotel pale Ubungo....kajenga barabarani kabisa..kisa..he has money....sasa akikutana na watu design ya akina Magufuri ndo wanaanza kulalamika. Hata kununua viwanja..utakuta watu wananunua viwanja well aware kabisa kwamba kuna barabara inapita/au itapita. To be honest..mimi nikiwa kiongozi nitaanza kudeal na wananchi wazembe kama hao. Harafu kibaya wanasingizia wataala wa jiji/manispaa..well..I wont buy it... Kwa nini udanganywe? Unless umejiridhisha kabisa otherwise..hivi viwanja vya deal tuviepuke..vina matatizo.

  Hapana bwana watanzania tumezidi. Tufuate sheria. siyo kujenga tuu..simply because one has money!
   
 17. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,947
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kwamba mipango miji walistahili kupangilia viwanja vizuri tokea awali walijisahau ktk hili kutokana na sababu wanazozijua wao...lakini nijuavyo wanaotakiwa kufidiwa ni wale nyumba zao zimeingia kwenye hifadhi ya barababara kwa upimaji uliofanyika baada ya watu hao kujenga na si wale walioingilia hifadhi ya barabara wakati upimaji ulikwishafanyika!
   
 18. t

  tulipo 04 Member

  #18
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bravo bravo Maguful kaz unayoifanya tunaiona utekelezaj wa sheria hauna msamaha wala kuoneana huruma si unajua huruma huzaa dhambi?
  hii itakuwa fundisho kw wahuni wengne wote, wakaambiane bila kufchana wajue kwamba hiyo wizara ya ujenz ameingia mtu wa kaz.
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  I 'm surprised it took you this long to realise this guy was an idiot!
   
 20. T

  Tom JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2011
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Serikali ipo kusaidia watu wake, kama hawakuwazuia kujenga huo ni uzembe wa serikali na ni vema wakalipwa pesa ya jengo zima. Watu wengine hawana uwezo wa kujenga tena, sasa wakibomoliewa nyumba wataishi wapi - ama watapewa mahema kwa muda na kujengewa nyumba baadaye kama wanaokumbwa na Mafuriko.

  Hiyo ya kulipwa kipande cha nyumba vema iwe ni kwa wale tu waliowahi andikiwa barua za kusitisha kujenga lakini wakakaidi.
   
Loading...