Mhe. Lissu, 2015 imefika

sisi wanaSingida mashariki tunawasubiri ccm watuletee hela na tutazila kweli kweli ila kura tunajua tutazipeleka wapi!

2010 Njau wa ccm alifilisika rasmi sasa amebaki anafuga mizinga ya nyuki kwao Mahambe!

mkuu mungu awabariki sana...
 
Jambo kubwa ambalo Lissu kafanya Ikungi ni kupiga sindano ya ganzi maendeleo, kwa hilo amefanikiwa sana kuliko Mbunge yeyote yule wanyaturu kwa upeo wao mdogo wanamsifia sana kwa hilo.

Wanyiramba niliwahi wasikia mitaa ya Urughu, Ndago, Kaselya, Shelui, Kiomboi na Kinampanda wakisema tuchangie elimu, afya ili tuwashinde wanyaturu ambao wamelala fofofo.

Wanahamasisha maendeleo kwa kasi ili kuwapiku Wanyampaa! Na baada ya miaka Kumi badaye basi wanyiramba watawapiga gape kubwa sana Wanyaturu! Wanyiramba wanashangilia sana kwa tabia ya Lissu
 
Wilaya ya Ikungi ndio ya Mwisho kwa kila Kitu kama vile ujenzi wa maabara zipo mbili tu tena zilizojengwa na World Bank, Zahanati vijiji vingi HAKUNA, Maji Ndio usiseme ni shida kubwa Ikungi, uchumi umedorora sana Hata kuchangia CHF wanyaturu wana 1% wakati wanyiramba WANA 86%.

elimu ya msingi na secondary Ikungu ndio inashika Mkia, wao wanachojua maendeleo yataletwa na serikali tu hata Nyumba zao zitajengwa na Serikali ndio maana kuna tofauti kubwa sana ya kipato na maendeleo kwa wilaya za Iramba na Ikungi
 
Wewe kutokulisoma haimaanishi wala haiondoi hadhi yake.. . Vinginevyo Lisu atazidi kushine kisiasa hadi unune.

Na sisi wanyiramba tunafurahi sana kwa mambo anayoyafanya Lissu kwa kutohamasisha maendeleo. Lissu uongoze miaka 100 ili tuwapige gape Wanyampaa
 

Haujui majukumu ya Mbunge wewe Gamba..

Haikuwa lazima pia wananchi kutoa rasimali zao kujenga/kuchimba hiyo mitaro, kupitia halmashauri ya Wilaya ya Ikungi nao wangeweza kuchangia kwani kupitia bajeti wanapata fedha za miradi ya maendeleo.
 
Akakona Mwinowere, Basi awe chifu wa ikungi si mezoea akija anawapa nyama choma na pombe hasa ile ya K Vant nadhani unaijua vizuri na nyie ndo mnamuaminisha kua hali ya siasa jimbon iko shwari, mmebugi.

Endelea kujilisha upepo ila kaa ukijua kwamba Lissu atashinda nadhani Uchaguzi Serikali za Mitaa ni kiashiria kimojawapo.
 
Kati ya Wanyaturu na Wanyiramba kuna vita Kali iliyojificha ni kama Wapalestine na Waisrael.......
 
Endelea kusubiria Ndege Bandarini.

Wanyiramba tunamuombea Lissu Maisha marefu awaongoze Wanyaturu kwa zaidi ya miaka 100 ili akina Kitundu, Makala, Mzengi, Shillah, Msengi, Kingu Siku Moja wawaongoze wanyaturu kwa kila sector kama ilivyo Kituo Cha Afya Sepuka Mkuu wa Kituo Myiramba, wauguzi Wote Wanyiramba, Lab technicians Ni Wanyiramba Lakini walinzi Ni wanyaturu
 
Serikali za mitaa Lissu kakomba mitaa yote ya CCM..

Bahati nzuri nimeishi Mwangeza Iramba jangwani maji km 20... Nyumba za walimu za tembe, sasa sijui wanyeramba wamewazidi vipi wabyaturu??
Tembea mpaka Kidarafa hadi kinampanda hawajui maji ni kero... Shule hazina madawati.
Hii imepelekea wana Mkalama na Iramba kuiamini Chadema kwenye serikali za mitaa... Maji maji maji Iramba ni tatizo.
 

Naombeni msaada. Hivi kweli kama sheria zinaandikwa kwa siyo na ndiyo inawezekana zikawa sheria nzuri? Huyu AG ni ni mweupe kabisa kichwani. Hata huyu waziri wa katiba na sheria yupo yupo tu. Sasa hizi sheria zitakuwaje? Nadhani kuna haja ya watu kwenda mahakamani kuzipinga. Kwa wingi wao CCM walikuwa wanampinga Lissu bila kutumia akili wakidhani wanawakomoa wapinzani. Hakika inatisha na kuudhi.
 

Kwa kweli mtoto kama Lissu ni faraja kwa familia, ukoo na kijiji.
 

Akina Mhitu, Mtaturu, Nkuwi bado ndo watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Iramba... Jitanganye! Kuku zenu mnaziuzia wanyaturu ili wawauzie watu wa Dar, Arusha, Mwanza na Dodoma.
Wanyiramba wanafanya vibarua Mbulu, Karatu na Hanang.... Wanawaita "Mandaa Kibarua."
 
Acha apiganie haki za wengi,

Kwanza jiulize, hao wabunge wengine wameleta mabadiliko gani sehemu wanazotoka kabla ya kumshambulia Lisu. Shida zote mnazopata ni kwa sababu ya serikali yenu dhaifu ya intarahamwe,

Serikali dhaifu ya intaeahamwe hahahahahahaa. Yeye kamuona lisu tu huyo mnaemuita raisi kafanya nini ??
 
Ni mjinga tu pekee ndio anaweza kumbeza lisu,,tatzo kubwa la tz hatujui kazi ya mbunge,,na hii ni kutokana na watu kulithi siasa,kisa baba ccm basi mtoto nae eti unakuwa ccm,,kama jimbo halina maendeleo laumu serikali na sio mbunge coz mbunge ni msemaji tu,,lakini pia ukumbuke kwamba ubunge sio kazi ya kudumu so huwa mtu anapoleta vitisho kama hivi ni unachekesha
 

haa haa kwani kazi ya serikali ni nini? je hao wananchi hawalipi kodi? kwani majimbo yanayoongozwa na ccm yana tofauti gani na ikingi? kwa mujibu wa katiba lissu amefanya kazi za kibunge ipasavo. tatizo watanzania wengi hawajitambui. hongereni singida mashariki kwa kutuletea mtu huyu....
 

hayo yote wa kulaumiwa ni serikali iliyopo madarakani. haiwezekani chama kimeongoza taifa letu miaka 50 na zaidi hali ikawa hivo. ccm must go. kodi za hao wananchi zinafanya nn huko ikungi? wa kulaumiwa ni serikali ya ccm na sio lissu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…