Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ...

Nakuunga mkono kabisa. NAD ni wataalamu haswa. Mtoa mada anapaswa kujua mifumo ya elimu inabadilika kulingana na wakati. Na ukiona hivyo ujue utendaji wake ni mzuri.
Ludovic Utouh ana ADA, lakini ndio mkaguzi mkuu wa serikali, Chini yake kuna watu wana PGD, Masters, Doctorates etc
ADA na CIMA au CPA ,MR UTOUH yuko vizuri saana, ila mkaguzi mkuu ni ASSAD , utouh alikuwaga
 
Ukiona tangazo wanataka mhasibu ujue wanataka mtu mwenye ujuzi wa muda mrefu kwenye field CPA ni mbwembwe tu mkuu. Kuna jamaa aliuliza swali ilikuwaje Bw Mwigamba akawa mhasibu pale makao makuu wakati amesomea maswala ya electronics na mass media?



Habari yako ni nzuri sana lakini ulitakiwa ujipange kwanza nadhani kama ana diploma stahiki ya hiyo field then anayo stahli ya kuwa mhasibu lakini angekuwa ana diploma ya utabibu wa wanyama halafu akawa mhasibu huo ni ufisadi wa mchana kweupe. Ukistaajabu ya Mussa unaweza ukayaona ya................... Tafakari
Huwezi kua mhasibu bila CPA, huyo mzee ni karani tu na sio mhasibu
 
Haha, WaTanzania ndo maana tunaliwa na kudhulumiwa kila kukicha. Yani hapa watu mnatetea elimu ya diploma kisa eti experience.

Hivi mambo mangapi tunasikia yameoza serikalini? Mtu amesoma enzi za nyerere, tena ka_diploma... Wakati duniani siku hzi accountants are professionals,..not only skills but also with new technologies.

Watu siku hizi wanaiba kwa technology na kujua vifungu flan flan kwenye accounts. Nina wasiwasi hata mhasibu wa Tanesco nae ana_experience ya 20, with kidiploma. (Ndo maana huwa wanalia hela hazionekani kwenye shirika, na wanapata tu hasara kila siku) Hahaha

Mbali na kuwa na experience, ukiwa na elimu ndogo, una_lacky confidence... Sishangai kuona hela zinachotwa meremeta, epa. Kama tuna wahasibu kama hawa.
always ccm ni mapoyoyo.

swissme
 
Ulaya na USA cheti( certificate) bado kina nguvu sana, wanacho zingatia ni skills hapa kwetu hata Shahada(first degree) imeshapoteza mvuto!!!
 
Wizara ya Mambo ya Ndani pameoza kwenye kitengo cha Manunuzi ni wababaishaji sana na watu wa magumashi sana wanapenda rushwa..Madudu mengi ya manunuzi yanayotokea kwenye taasisi zilizo chini ya Wizara ile kama polisi, uhamiaji,magereza na nida yanasababishwa na wao..
 
Kuna jamaa mmoja namfahamu kasoma Ifunda Technical School baada ya hapo hakuendelea na masomo zaidi ya hapo.
Amefanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi kwa muda wa miaka 24. Kwa sasa ni Engineer wa kampuni hiyo!
 
Si Tatizo kama mhusika ana experience ya kazi mda mrefu! Pia hapo kazini navyojua mimi ameshakula on-job training nyingi sana ambazo zinamfanya awe vizuri kuendana na mahitaji ya kazi husika! Pia niwaulize, hivi kunamtu anaweza kusema ya kwamba alivyosomea Masters ndicho anachofanyia kazi?
Kama mtu alikuwa serious na shule kila daraja la elimu unalopanda huwa linakuongezea upeo na maarifa ya kile ulichosomea na maisha kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom