Mhariri wa Gazeti la The Guardian ameonesha uzalendo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,858
Wakati magazeti karibu yote yakiongozwa na habari zinazohusiana na maazimisho ya sherehe za May Mosi,Gazeti la The Guradian limebeba habari kuu juu ya utata wa ununuzi ndege aina ya Boeing Dreamliner.

Katika ukurusa wake wa mbele,gazeti hili limechapisha taarifa iliyoko katika mtandao wa Boeing taarifa inayoonyesha ndege hiyo kukataliwa na baadhi ya mashirika ya ndege duniani na ambayo hata sisi hapa JF tumekuwa tukiijadili kutoka katika website hiyo.

Gazeti pia limemuhoji Mkurugenzi Mkuu wa ATCL kuhusu sakata hili na wameweka nukuu ya alichokisema katika ukurasa wa mbele ila kutokana na maandishi kuwa madogo nimeshindwa kusoma nukuu hiyo.

NB:Naomba ieleweke nimepitia blgo ya MillardAyo asubuhi hii kuangalia magazeti yameandika nini na ndio nikakuta hiyo habari kwahiyo hata mimi sina details hivyo usinihoji bali tafuta copy yako.

milard.jpg
 
Kwa wale ambayo wameshasafiri na ndege za bombadia watakubaliana na mimi kwamba hizi ndege ni kweli zina tatizo serikali imeingizwa chaka kwa kununua ndege ambazo zimekataliwa zaidi ya nchi 10. Sitosahau tarehe 18.04.2017 nikiwa natoka likizo Arusha kwenda tukiwa angani kwa muda dakika kuna hali ya sitofahamu ilitokea tukiwa ndani ya ndege kila mtu aliomba Mungu tulipofika salama airport rubani anatuomba radhi anashindwa kutuambia ndege za bombadia zina matatizo.
Kuna ila tunafichwa kuna thread nyingine humu JF unaweza kuisoma
Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8
 
mi naona wamefanya kazi yao wala si uzalendo

je? magazeti yote yangeandika kuhusu ununuzi wa ndege na moja likajitokeza kuandika juu ya meimosi nalo tungesema limeonesha uzalendo.

hili suala la ndege lifatiliwe tupate majibu kama tulipigwa tujue

Mpiga deal wa Kivuko KIBOVU tuamuamini alipotuletea Dream liner mbovu halafu mnashangaa
 
Tusibeze juhudi za serikali ktk kutafuta na kuthubutu kuchukua hatua za kuleta maendeleo. Magufuli amethubutu na anajitahidi. INGAWA serikali na taasisi zake inapaswa kufanya upembuzi na utafiti wa kutosha kubla ya kufanya maamuzi yatakayoligharimu taifa hata kuingia kwenye hasara.
 
Sio swala la kubeza ni kukosoa ili kuboresha
Tusibeze juhudi za serikali ktk kutafuta na kuthubutu kuchukua hatua za kuleta maendeleo. Magufuli amethubutu na anajitahidi. INGAWA serikali na taasisi zake inapaswa kufanya upembuzi na utafiti wa kutosha kubla ya kufanya maamuzi yatakayoligharimu taifa hata kuingia kwenye hasara.
 
kweli JF inalisha familia nyingi kwa hio habari ya Jf imeiingizia pesa IPP safi sana
na tunamshukuru Mh WAZIRI kwa ku respond quickly kwamba watafanyia uchunguzi habari hii
 
Tusibeze juhudi za serikali ktk kutafuta na kuthubutu kuchukua hatua za kuleta maendeleo. Magufuli amethubutu na anajitahidi. INGAWA serikali na taasisi zake inapaswa kufanya upembuzi na utafiti wa kutosha kubla ya kufanya maamuzi yatakayoligharimu taifa hata kuingia kwenye hasara kwenye hasara kubwa.

Swali kubwa ni hili, je hao/hizi taasisi za kufanya upembezi na utafiti wa kutosha wanapewa fursa ya kufanya hivyo?? Si unajua kwa asili yetu baba akishaongea na kutoa ultimatum hakuna wa kuhoji tena hata mama??
 
Tusibeze juhudi za serikali ktk kutafuta na kuthubutu kuchukua hatua za kuleta maendeleo. Magufuli amethubutu na anajitahidi. INGAWA serikali na taasisi zake inapaswa kufanya upembuzi na utafiti wa kutosha kubla ya kufanya maamuzi yatakayoligharimu taifa hata kuingia kwenye hasara.
Nyie ndio wa kuwashangaa.... facts mnapewa mnasema msibeze...nchi ikiwa na watu wengi kama hawa inakua ya wajinga
 
Wakati magazeti karibu yote yakiongozwa na habari zinazohusiana na maazimisho ya sherehe za May Mosi,Gazeti la The Guradian limebeba habari kuu juu ya utata wa ununuzi ndege aina ya Boeing Dreamliner.

Katika ukurusa wake wa mbele,gazeti hili limechapisha taarifa iliyoko katika mtandao wa Boeing taarifa inayoonyesha ndege hiyo kukataliwa na baadhi ya mashirika ya ndege duniani na ambayo hata sisi hapa JF tumekuwa tukiijadili kutoka katika website hiyo.

Gazeti pia limemuhoji Mkurugenzi Mkuu wa ATCL kuhusu sakata hili na wameweka nukuu ya alichokisema katika ukurasa wa mbele ila kutokana na maandishi kuwa madogo nimeshindwa kusoma nukuu hiyo.

NB:Naomba ieleweke nimepitia blgo ya MillardAyo asubuhi hii kuangalia magazeti yameandika nini na ndio nikakuta hiyo habari kwahiyo hata mimi sina details hivyo usinihoji bali tafuta copy yako.
Tatizo lako wewe ni Moja unapenda kuona habari zinazokufurahisha wewe tu.ukiona tafouti unadhani wahariri wendawazimu ,
Likini ukisikia magu anasema magazeti yaandiki mazuri ya serikali,unalia sana huoni kuwa ,siku magazeti yakiwa yaana isema vibaya serikali ya chadema utaona siyo wazalendo .Jifunze siasa nzuri acha chuki na serikali
 
Back
Top Bottom