Jiulize ni mawaziri wangapi na makatibu wakuu wangapi wamepita hiyo wizara na wote wameishia kuwa watuhumiwa.Jiulize richmond ilhusisha waziri na katibu mkuu tu.Jiulize mbona kashifa hiyo ya richmond ilizimwa bungeni. Jiulize mbona bodi ya wakurugenzi haitajwi sana. Hii issue kuna jambo limejificha na mimi siamini kabisa kama TANESCO walifanya haya bila watu fulani kujua na kukaa kimya.Hata hii kampuni ya PUMA licha ya bei yake ndogo inahitaji kuchunguzwa mahusiyano yake na wakubwa wa serikali hii.Bei ndogo isiwe sababu hatujui nini kiko nyuma yake.Waziri mpya katibu mkuu mpya.
Jiulize ni mawaziri wangapi na makatibu wakuu wangapi wamepita hiyo wizara na wote wameishia kuwa watuhumiwa.Jiulize richmond ilhusisha waziri na katibu mkuu tu.Jiulize mbona kashifa hiyo ya richmond ilizimwa bungeni. Jiulize mbona bodi ya wakurugenzi haitajwi sana. Hii issue kuna jambo limejificha na mimi siamini kabisa kama TANESCO walifanya haya bila watu fulani kujua na kukaa kimya.Hata hii kampuni ya PUMA licha ya bei yake ndogo inahitaji kuchunguzwa mahusiyano yake na wakubwa wa serikali hii.Bei ndogo isiwe sababu hatujui nini kiko nyuma yake.
<br>Kukurupuka kivipi labda wewe ndio hujui.. Siku zote misukumo huwa ni kwa kujinufaisha lakini hapa hata mjinga anaona ni kwa jinsi gani hapa katibu mkuu katuokolea fedha zetu kuliwa na wajanja, funguka mzee mafisadi hutumia wakati mwingine sheria kujinufaisha.. hushangai bei iliyopatikana kupitia tenda ni kubwa kuliko bei iliyopatikana kupitia uamuzi wa katibu mkuu? Haya sasa tukio lenyewe limepelekea kuvunjwa kamati ya bunge ya nishati.. mengi yataibuka labda yatakutoa gizani.
Acha tabia ya kufunika kombe mwanaharamu apite.wabunge na watanzania wengi hawakuridhika na utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusu richmond kwa mfano wahusika kuwajibishwa.Lakini wakati wabunge na wananchi wakitaka wahusika wawajibishwe kilichotokea ni spika kuja na hoja kuwa mjadala kuhusu richmond umefungwa rasmi na kanuni zinazuia kuongelea jambo lililokiwisha fanyiwa uamuzi.Sasa hii ni nini kama sio kufunika kombe mwanaharamu apite?Hembu we iba kuku alafu uone kitakachokutokea.Kashfa ya Richmond ilizimwa bungeni? hivi wewe uko dunia ipi? hujui kuwa hata waziri mkuu na mawaziri wengine watatu wamejiuzulu kwa uongo wa Richmond?
Wizara zote mawaziri na makatibu wakuu wanapitia na kuondoka na hata huyu ikifika wakati ataondoka kama wengine. Hii ni kawaida toka enzi na enzi na si Tanzania tu ni dunia nzima.
Ni mawaziri wachache Tanzania hii waliomaliza miaka kumi katika wizara moja. Hiyo rikodi inashikiliwa na Kikwete kwa sasa alipokuwa waziri wa mambo ya nje wakati wa wa Ben.
Mhando angefunguka tungejua mengi
Hawezi kufunguka, maana amefunguliwa tayari - nadhani hata yeye anashangaa and naamini hakutegemea hii sinema ingekuwa hivi? hii ya kufanya personal business na ofisi ya umma hataweza funguka tena, sana anaomba huo unaofanywa juu yake ufanywe na Mungu ambaye anasoma dhamira ya mtu kwa undani.
Hivi ulijipa muda kidogo wa kufikiri? au umeamka usingizini na kuanza kuchangia! Zito anautaka uraisi kupitia cdm, Tanesco ni shirika chini ya serikali ya ccm, ndio waliomuwajibishaMhando, Zito lipotaka kumtetea mhando, pamoja na ushaidi wote unaoonyesha mhando amehusika kwa namna moja au nyingine ndio uliowafanya wabunge wengine kutaka kujua kulikoni Zito amtetee mtu wa aina hiyo? kaa ukijua ccm wanapenda sana Zito aendelee kutangaza nia ya kugombea uraisi kupitia cdm, kwa sababu kubwa mbili;Ukishautaka Urais utapata kila aina ya kashfa......Za ukweli na za Uongo!!!! basi tu uonekani hufai kuwa Rais... Na ataandamwa sana huyu Zito ila akishasema kuwa hawezi kuwa RAIS then watamuacha....
Mimi najiuliza hivi huyu jamaa alikuwa anakula peke yake bila kushirikisha bwana wakubwa au wamegeukana?
Kama sikosei bwana Msabaha aliwahi kusema katolewa kafara na kauli hii nadhani ilipita kimyakimya.Sasa huyu sijui nae atakuja na lipi.Tusubiri
Hivi ulijipa muda kidogo wa kufikiri? au umeamka usingizini na kuanza kuchangia! Zito anautaka uraisi kupitia cdm, Tanesco ni shirika chini ya serikali ya ccm, ndio waliomuwajibishaMhando, Zito lipotaka kumtetea mhando, pamoja na ushaidi wote unaoonyesha mhando amehusika kwa namna moja au nyingine ndio uliowafanya wabunge wengine kutaka kujua kulikoni Zito amtetee mtu wa aina hiyo? kaa ukijua ccm wanapenda sana Zito aendelee kutangaza nia ya kugombea uraisi kupitia cdm, kwa sababu kubwa mbili;
1.Zito yuko karibu sana au ni rafiki mkubwa wa mwenyekiti wa ccm (JK Kikwete)
2.Zito staili anayotumia kutangaza nia inaibua migogoro ndani ya cdm mfano kuwasingizia wabunge wenzake kwamba
wanamuunga mkono yeye kugombea uraisi.
kwa mazingira haya wabunge wa ccm lazima wangemuunga mkono zito ili aendeleze hizo propaganda za kuisambaratisha cdm. lakini hawajafanya hivyo sababu inawezekana ni kweli zito anahusika na hujuma hizo anazotuhumiwa. kwa hiyo sio suala la uraisi hapa.