Mhando kaamua kufa na tai shingoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhando kaamua kufa na tai shingoni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 27, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,968
  Likes Received: 37,525
  Trophy Points: 280
  Jioni hii nimefuatilia bunge kwa makini kuanzia mwanzo mpaka miwisho.Nimegundua mambo haya:-


  1. Mhando na wenzake inaonekana na inawezekana wamefanya makosa na sijui kama watapona
  2. Zitto na baadhi ya wabunge wa ccm wanaonekana kushambuliwa na kutuhumiwa kuchukua rushwa kwasababu kuna wabunge walikuwa wakitaja majina yao kwa sauti wakati mjadala ukiendelea
  3. CCM leo ni kama wameibuka washindi hasa mbunge mmoja maarufu wa upinzani anapotuhumiwa kuhongwa na kwamba tatizo la umeme sasa chanzo sio ccm pekee bali hata wapinzani wanahusika.
  4. kuna jitihada za dhati kabisa kumsafisha katibu mkuu na kutupa lawama zote kwa TANESCO na kwamba wanasiasa hawahusiki kabisa ktk sakata hili.

  Binafsi licha ya dalili zote kuonyesha bwana Mhando na wenzake huenda wamefanya makosa mimi nina maswali yafuatayo ambayo tunahitaji kujiuliza:-


  1. Mbona shutuma zote hizi zimeibuka wakati huu na ni makosa ya muda mrefu tu?
  2. Mbona karibu wabunge wote hawajatoa wazo la kuundwa tume huru kuchunguza jambo hili na badala yake wanahukumu upande mmoja tu?
  3. TANESCO Waliweza kufanya haya yote na kwa muda wote bila wizara na bodi ya wakurugenzi kujua?
  4. Ilikuwa sahihi kuwatuhumu watendaji wa TANESCO ambao hawana nafasi ya kujitete bungeni na kujiaminisha kuwa kama ni ufisadi basi TANESCO wako peke yao?
  5. Zitto na wenzake waliokuwa wanashambuliwa walitaka uchunguzi ufanyike au walikuwa na hoja gani?

  Bosi wa TANESCO bila shaka anajua kila kitu ila huenda ataamua kukaa kimya. Kama kweli ana makosa ni vigumu kwa yeye kusema ukweli kwa usalama wake na washirika wake ambao huenda wamemgeuka.Hapa kuna walioshika mpini na wengine kwenye makali

  Bila shaka ataamua kufa na tai shingoni.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni kweli Zitto ni kati ya wabunge wanaotuhumiwa kuhongwa katika sakata hili? Naomba jibu maana mwili unasisimka kusikia wapinzani ni miongoni mwa wanaounga mkono ufisadi TANESCO.
   
 3. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ni kweli Zitto anatuhumiwa lakini ni yeye peke yake maana msimamo wa chama cha CDM kama ulivyoelezwa na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ni tofauti na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh.Zitto Zuberi Kabwe!! naanza kuelewa kwanini walimwambia asiwe Mwenyekiti wa CDM pengine sasahivi chadema kingekuwa kama NCCR umaarufu wake ungekuwa una-decline kwa kasi!!!
   
 4. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,925
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  ukweli utawekwa mezani soon.
   
 5. peri

  peri JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mhando angefunguka tungejua mengi
   
 6. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ukishautaka Urais utapata kila aina ya kashfa......Za ukweli na za Uongo!!!! basi tu uonekani hufai kuwa Rais... Na ataandamwa sana huyu Zito ila akishasema kuwa hawezi kuwa RAIS then watamuacha....
   
 7. F

  Fofader JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Nafikiri kama alivyosema mh. Mnyika kwamba wakati huu huwezi kusema CCM wameshinda kwa siku ya leo kwa sababu kilicho kikubwa kwetu kwa sasa ni maslahi ya taifa halafu vyama vifuate.
   
 8. M

  MVENGEVENGE Senior Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye cm ya mhando aiweke hapa tumpigie atupe upande wake anasemaje ili kumtendea haki.
   
 9. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,968
  Likes Received: 37,525
  Trophy Points: 280
  Mkuu huo ndio mtazamo uliopo.Nlisika mbunge mmoja akimtaja zitto moja kwa moja wakati mbunge mwingine akichangia.Lengo ni umma usikie.
   
 10. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,968
  Likes Received: 37,525
  Trophy Points: 280
  Hivi zitto alikuwa anamtetea Mhando au alitaka kamati ya bunge iwahoji TANESCO pamoja na viongozi wa wizara ili kupata ukweli?
  Hii inaweza kuwa ni mbinu kutaka kummaliza kisiasa ila najua nae atatoa ufafanuzi.
   
 11. b

  bantulile JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,439
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kama Zito kala rushwa, watu wasiseme kwa sababu ni Zito? Kama hajala kwa nini asiombe wanaoseme kuna wabunge wamekula rushwa wathibitishe kauli zao kama ilivyozoeleka kila kauli zenye utata. Nadhani kuna kaukweli kwenye tuhuma hizi, tusikimbilie tu kusema wanamwandama Zito sababu ya rushwa. Kama kala au hakula ni vema tujue mapema kabla safari haijaenda mbali sio kufichaficha kama 2005 majuto itakuwa mjukuu
   
 12. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,968
  Likes Received: 37,525
  Trophy Points: 280
  Mkuu mashmbulizi yamefanyika bungeni na yeye hakuwa na nafasi ya kuongea ndani ya bunge.Naona tumpe muda ila kama atakaa kimya au kuja na utetezi wa uongo basi ajue ndio amejimaliza kisiasa.
   
 13. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kachafuliwa na nini au na wewe umetumwa kusaidia kundi la mafisadi? Jiulize kakataa zabuni ya sh 1800/- kaipa Puma kwa sh 1400/- na sheria inamruhusu kufanya hivyo kwa maslahi ya umma, wewe unafikiri hapo wakuokolewa nani? Au mnataka kujificha chini ya kivuli cha kufuata taratibu za manunuzi ya umma ili kuendelea kutuibia au?

  Kwa bei ya Puma ambayo serikali yetu ina hisa 50% tutaokoa sh bil 3 kila mwezi.. na pia faida ya kampuni itakayozalishwa tutapata mgao.. Kaa, tulia, tafakari, chukua hatua acha kuyumbishwa na mafisadi wanaotumia kanuni/sheria kuifilisi nchi.
   
 14. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,968
  Likes Received: 37,525
  Trophy Points: 280
  Acheni kukurupuka.Una uhakika na kilichomsukuma Katibu mkuu huyo?Mimi na wewe hatujui, dawa hapa ni kuunda kamati ya uchunguzi tu.Na kwaninii swala la kamati halipewi nafasi?
   
 15. kiplagati26

  kiplagati26 JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  kama ndio mtindo huu basi tumekwisha maana madini yetu,gesi yetu ,makaa ya mawe yetu hati leo sisi bado maskini tunakufa huku mapigo ya moyo yanafanya kazi
   
 16. H

  Hon.MP Senior Member

  #16
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elewa kuwa huyu bwana alisimamishwa tu apishe uchunguzi lakini zitto na wenzake waliohongwa wakawa wanakataa hata hilo. Alikuwa hata hajafukuzwa!! Sasa amefanya watu wameteremsha madudu yake live muulize Mnyika & Mbatia wakueleze utalia!
   
 17. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  They always say everyone has a price.. If you offer the right amount utasikilizwa.. Hamna wakati wabunge wanakula hela za kuhongwa kama wakati wa kupitisha bajeti za wizara
   
 18. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Uadilifu ndo ulimsukuma katibu mkuu. Na akatumia discreation yake kulinusuru taifa

  Hekoooooo! Katibu Mkuu
   
 19. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Jamani huyu ZITTO ndo anautaka urais kama MD tu wa TANESCO ameweza kumuhonga je ataweza wawekezaji kama BARRICKS si ndio atakuwa RAIS tajiri kama MOBUTU SESEKO jaamani huyu mtu ni hatari tumuogope.....HONGERA MNYIKA.
   
 20. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mkuu hawezi kufunguka maana akifunguka ccm itakuwa ndani ya ndapo la tabata itakwisha ndani ya masaa tu
   
Loading...