Hapa kwa serikali makini, sio mhando tu, hata mwenyekiti wa bodi nae lazima aondoke, ila kwa kuwa alikuwa Mjeshi Former CDF, ndio wamuogopa!
Yeye anajibu kwenye Twitter na FbMkuu mashmbulizi yamefanyika bungeni na yeye hakuwa na nafasi ya kuongea ndani ya bunge.Naona tumpe muda ila kama atakaa kimya au kuja na utetezi wa uongo basi ajue ndio amejimaliza kisiasa.
Nafikiri wengi hamkusikia vizuri hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani. aliomba kamati maalumu iundwe kwa ajili ya uchunfuzzi wa suala hiliumkuu hawezi kufunguka maana akifunguka ccm itakuwa ndani ya ndapo la tabata itakwisha ndani ya masaa tu
Kukurupuka kivipi labda wewe ndio hujui.. Siku zote misukumo huwa ni kwa kujinufaisha lakini hapa hata mjinga anaona ni kwa jinsi gani hapa katibu mkuu katuokolea fedha zetu kuliwa na wajanja, funguka mzee mafisadi hutumia wakati mwingine sheria kujinufaisha.. hushangai bei iliyopatikana kupitia tenda ni kubwa kuliko bei iliyopatikana kupitia uamuzi wa katibu mkuu? Haya sasa tukio lenyewe limepelekea kuvunjwa kamati ya bunge ya nishati.. mengi yataibuka labda yatakutoa gizani.Acheni kukurupuka.Una uhakika na kilichomsukuma Katibu mkuu huyo?Mimi na wewe hatujui, dawa hapa ni kuunda kamati ya uchunguzi tu.Na kwaninii swala la kamati halipewi nafasi?
Jioni hii nimefuatilia bunge kwa makini kuanzia mwanzo mpaka miwisho.Nimegundua mambo haya:-
- Mhando na wenzake inaonekana na inawezekana wamefanya makosa na sijui kama watapona
- Zitto na baadhi ya wabunge wa ccm wanaonekana kushambuliwa na kutuhumiwa kuchukua rushwa kwasababu kuna wabunge walikuwa wakitaja majina yao kwa sauti wakati mjadala ukiendelea
- CCM leo ni kama wameibuka washindi hasa mbunge mmoja maarufu wa upinzani anapotuhumiwa kuhongwa na kwamba tatizo la umeme sasa chanzo sio ccm pekee bali hata wapinzani wanahusika.
- kuna jitihada za dhati kabisa kumsafisha katibu mkuu na kutupa lawama zote kwa TANESCO na kwamba wanasiasa hawahusiki kabisa ktk sakata hili.
Binafsi licha ya dalili zote kuonyesha bwana Mhando na wenzake huenda wamefanya makosa mimi nina maswali yafuatayo ambayo tunahitaji kujiuliza:-
- Mbona shutuma zote hizi zimeibuka wakati huu na ni makosa ya muda mrefu tu?
- Mbona karibu wabunge wote hawajatoa wazo la kuundwa tume huru kuchunguza jambo hili na badala yake wanahukumu upande mmoja tu?
- TANESCO Waliweza kufanya haya yote na kwa muda wote bila wizara na bodi ya wakurugenzi kujua?
- Ilikuwa sahihi kuwatuhumu watendaji wa TANESCO ambao hawana nafasi ya kujitete bungeni na kujiaminisha kuwa kama ni ufisadi basi TANESCO wako peke yao?
- Zitto na wenzake waliokuwa wanashambuliwa walitaka uchunguzi ufanyike au walikuwa na hoja gani?
Bosi wa TANESCO bila shaka anajua kila kitu ila huenda ataamua kukaa kimya. Kama kweli ana makosa ni vigumu kwa yeye kusema ukweli kwa usalama wake na washirika wake ambao huenda wamemgeuka.Hapa kuna walioshika mpini na wengine kwenye makali
Bila shaka ataamua kufa na tai shingoni.
Prof wa ukweli Muhongo amekubali ombi la Mbatia la kuivunja bodi ya Tanesco ila amesema atatangaza nafasi za members wa bodi kwenye magazeti ili competent applicants waombe. Tumpe nafasi Prof Muhongo kama magamba hawatamharibu tunaweza kuona japo mafanikio kidogo. We should nt forget that he is just a human and not an angel.Hapa kwa serikali makini, sio mhando tu, hata mwenyekiti wa bodi nae lazima aondoke, ila kwa kuwa alikuwa Mjeshi Former CDF, ndio wamuogopa!
0763174444Mwenye cm ya mhando aiweke hapa tumpigie atupe upande wake anasemaje ili kumtendea haki.
Uadilifu ndo ulimsukuma katibu mkuu. Na akatumia discreation yake kulinusuru taifa
Hekoooooo! Katibu Mkuu