Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,198
- 162,736
Jioni hii nimefuatilia bunge kwa makini kuanzia mwanzo mpaka miwisho.Nimegundua mambo haya:-
Binafsi licha ya dalili zote kuonyesha bwana Mhando na wenzake huenda wamefanya makosa mimi nina maswali yafuatayo ambayo tunahitaji kujiuliza:-
Bosi wa TANESCO bila shaka anajua kila kitu ila huenda ataamua kukaa kimya. Kama kweli ana makosa ni vigumu kwa yeye kusema ukweli kwa usalama wake na washirika wake ambao huenda wamemgeuka.Hapa kuna walioshika mpini na wengine kwenye makali
Bila shaka ataamua kufa na tai shingoni.
- Mhando na wenzake inaonekana na inawezekana wamefanya makosa na sijui kama watapona
- Zitto na baadhi ya wabunge wa ccm wanaonekana kushambuliwa na kutuhumiwa kuchukua rushwa kwasababu kuna wabunge walikuwa wakitaja majina yao kwa sauti wakati mjadala ukiendelea
- CCM leo ni kama wameibuka washindi hasa mbunge mmoja maarufu wa upinzani anapotuhumiwa kuhongwa na kwamba tatizo la umeme sasa chanzo sio ccm pekee bali hata wapinzani wanahusika.
- kuna jitihada za dhati kabisa kumsafisha katibu mkuu na kutupa lawama zote kwa TANESCO na kwamba wanasiasa hawahusiki kabisa ktk sakata hili.
Binafsi licha ya dalili zote kuonyesha bwana Mhando na wenzake huenda wamefanya makosa mimi nina maswali yafuatayo ambayo tunahitaji kujiuliza:-
- Mbona shutuma zote hizi zimeibuka wakati huu na ni makosa ya muda mrefu tu?
- Mbona karibu wabunge wote hawajatoa wazo la kuundwa tume huru kuchunguza jambo hili na badala yake wanahukumu upande mmoja tu?
- TANESCO Waliweza kufanya haya yote na kwa muda wote bila wizara na bodi ya wakurugenzi kujua?
- Ilikuwa sahihi kuwatuhumu watendaji wa TANESCO ambao hawana nafasi ya kujitete bungeni na kujiaminisha kuwa kama ni ufisadi basi TANESCO wako peke yao?
- Zitto na wenzake waliokuwa wanashambuliwa walitaka uchunguzi ufanyike au walikuwa na hoja gani?