Mhando amkana mkewe mahakamani

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,533
Reaction score
28,686
Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TANESCO, William Mhando, amemkana mkewe Eva Mhando mahakamani kwa kukataa kwamba Eva sio mke wake. Mkurugenzi huyo amefunguliwa kesi ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na moja ya mashtaka yanayomkabili ni kula njama za kufanya ufisadi akishirikiana na mkewe, Eva, anayedaiwa kupewa zabuni ya mabilioni ya walipakodi kinyemela.

Source: Raia Tanzania.

MAONI YANGU
Naona wakili wa mhando ameamua kufanya hii kesi iwe complicated na kuchukua muda mrefu huku fisadi Mhando akizidi kutafuna fedha za umma alizojichotea. Haya ndio matatizo ya mawakili 'waganga njaa' tuliokuwa nao ktk nchi hii. Mawakili kama hawa hawana hata chembe ya uzalendo.

Mpaka vyeti vya ndoa vije vipatikane ili kuthibitisha uanandoa kati ya Mhando na Eva, kesi itakuwa imemaliza karne kabla ya kuamuliwa. Hivi nchi hii tumerogwa na nani?



 
wakili wake yuko kazini, yeye anachokifanya ni kutoa huduma kwa mteja wake,

je , ya tundu Lisu umeyasahau
 
Kwi kwii Mke alisemaje pale alipokanwa hadharani mahakamani? Kama Eve naye amekubali/atakubari kirahisi, hiyo ina implication kubwa, baadaye katika mgawanyo wa mali in case of anything. Eve anaweza huko usoni asipate kitu kwenye mali za Mhando kama ataachia hili liende hivi hivi na mahakama iamue kwamba Eve kweli sio Mke wa Mhando. Hii inanikumbusha kesi ya jamaa mmoja aliyefunga ndoa "fake" na mwalimu mmoja kwa kusudi la kumsaidia ahamie shule za mjini. Bahati mbaya yule bwana akafariki, yule mwalimu aliyefunga ndoa "fake" na huyo jamaa akajitokeza baada ya kifo akidai mgawanyo wa mali, kwamba na yeye ni mke halali wa ndoa wa marehemu kwa kuonesha marriage certificate!
 

Kuliko aingie jela kwa kujifanya mke wa Mhando ili tu apate mali huko mbeleni, bora hizo mali azisamehe huko mbeleni lakini leo asiingie jela!!
 
Iwapo mke atakubali kuwa Mhando sio mume wake issue itàkuwa imekwisha. Waendesha mashtaka hawataleta vyeti, Mhando ataleta cheti cha kuonyesha mke ni mtu mwingine kabisa.
 
wakili wake yuko kazini, yeye anachokifanya ni kutoa huduma kwa mteja wake,

je , ya tundu Lisu umeyasahau

Safi sana wakili! Tayari serikali ya magamba imeshalizwa hapo! Ooh mbona wanaishi nyumba moja? Mhando anasema alikuwa mpangaji wangu! Magamba kwishney!!
 
[
USIJIFANYE MJUAJI WA KILA KITU?KWANI WEWE NDIE NJAGU ULIOCHUNUZA SUALA HILI?YAELEKEA UNA MAFRASRESHENI YAKO

QUOTE=tpaul;9803541]Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TANESCO, William Mhando, amemkana mkewe Eva Mhando mahakamani kwa kukataa kwamba Eva sio mke wake. Mkurugenzi huyo amefunguliwa kesi ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na moja ya mashtaka yanayomkabili ni kula njama za kufanya ufisadi akishirikiana na mkewe, Eva, anayedaiwa kupewa zabuni ya mabilioni ya walipakodi kinyemela.

Source: Raia Tanzania.

MAONI YANGU
Naona wakili wa mhando ameamua kufanya hii kesi iwe complicated na kuchukua muda mrefu huku fisadi Mhando akizidi kutafuna fedha za umma alizojichotea. Haya ndio matatizo ya mawakili 'waganga njaa' tuliokuwa nao ktk nchi hii. Mawakili kama hawa hawana hata chembe ya uzalendo.

Mpaka vyeti vya ndoa vije vipatikane ili kuthibitisha uanandoa kati ya Mhando na Eva, kesi itakuwa imemaliza karne kabla ya kuamuliwa. Hivi nchi hii tumerogwa na nani?[/QUOTE]
 
Ukoo wa panya,nchi hii imeishalizwa na wengi,ukianza na ndugu Change aliyesema ni vijisenti na hakuna aliyeuliza swali mpaka leo.Na huu ni mwendelezo,kama kweli watanzania tunataka mabadiliko,tuondoe ukoo wa panya kwanza.
 
...bonge la trick,kwani definition ya ndoa/mke ni nini ? Kama walikuwa wakiishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili tayari ni mke na mume...

Mahakamani unatakiwa ushahidi mzuri usiotia shaka..."kuishi naye kwa miaka kadhaa" unaweza kukuthibitishaje mahakamani? Mahakama wanataka cheti halali cha ndoa (official document)kilichotolewa na mamlaka inayotambulika kisheria. Hapa ndipo penye ugumu. Usidhani kwamba wakili aliyemfundisha kumkana mkewe amekurupuka. Atakuwa amefanya legal analysis ya kutosha akaona kwamba Mhando akijitetea hivyo anaweza kuchomoka kwenye kesi hii. Sio kwamba ninatetea uhuni huu ila kwa mahakama zetu jinsi zilivyo ni vigumu sana kupokea ushahidi wa maneno/kusikia.
 
.......kwamba na yeye ni mke halali wa ndoa wa marehemu kwa kuonesha marriage certificate!
Mbele ya sheria hii kitu ndio inatakiwa na sio habari za kuishi pamoja miaka 8,bila uthibitisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…