Mhando aleta mtafaruku kati ya wabunge na serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhando aleta mtafaruku kati ya wabunge na serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Jul 18, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HATUA ya Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, William Mhando imeibua mvutano kati ya wabunge na Serikali.
  Mwishoni mwa wiki, bodi hiyo iliwasimamisha kazi Mhando, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Huduma za Tanesco, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi, Ununuzi, Harun Mattambo.

  Hata hivyo, baadhi ya wabunge walio katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na wengine wa Kamati ya Nishati na Madini, wamesema uamuzi huo umejaa maswali kuliko majibu.

  Moja ya maswali hayo ni mchakato wa kumsimamisha wakihoji kikao kilichochukua uamuzi huo kuitishwa na wizara badala ya bodi, kupatikana Mkaguzi Kampuni ya Ernst&Young kukagua hesabu za Tanesco bila kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma na tuhuma za ukabila dhidi ya bosi huyo wa Tanesco.

  Lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo za wizara kuingilia mamlaka ya bodi, alijibu: “Kesho (leo) tunakutana na kamati, kwa hiyo siwezi kuzungumza chochote nitazungumza ndani ya kamati.”

  Hata hivyo, habari kutoka kamati hizo za Bunge zinasema mkutano kati ya watendaji wa wizara, bodi na wajumbe wa kamati hizo unatarajiwa kuwa na mvutano mkali.

  Tayari baadhi ya wajumbe wa POAC wamehoji tuhuma za ukabila ambazo anatuhumiwa kuwa nazo Mhando, huku wakimnyooshea kidole Maswi na waziri wake.

  “Hivi Mhando ukabila wake ni nini...? Hivi, tunapaswa kujadili uwezo wa mtu au kabila lake?” alihoji mmoja wa wajumbe wa POAC.

  Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alipoulizwa kuhusu kikao chao cha kesho alisema tayari wameshamwandikia barua Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na wanatarajia kukutana na bodi kupata ufafanuzi.

  KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI: MHANDO ALETA MTAFARUKU KATI YA WABUNGE NA SERIKALI
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Serikali imezidi kuingilia sana mambo ya ndani ya mashirika especially Tanesco.

  Mnakumbuka yule mwenyekiti wa bodi ya Tanesco aliyejifanya yeye ni sehemu ya menegejimenti akawa anakaa ofisini akakomeshwa na Dr Rashidi?

  Mimi naona serikali ijipange upya itimize ahadi zake kumuondoa Muhando haitasaidia kitu.
   
 3. l

  luckman JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  suala si kumuondoa au kutomuondoa, suala hapa ni haki, kama anatakiwa kuondolewa viwepo vigezo kama sio viwepo vigezo ambavyo haviachi maswali masikioni mwa watanzania.
   
 4. T

  TATOO Senior Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo watu wengi hatujui maana ya kuchukua hatua za dharula,,,kwani kama mhando ameonekana ni kikwazo ndani ya tanesco na hatua sitahiki au hatua ya kwanza ni ya kumuondoa kwa haraka kuna sababu gani gani ya kuita bodi kama mamlaka hayo hata waziri wake anayo??? anachukua hatua na anaitisha bodi na kuipa taarifa,,kwasababu ieleweke kwamba hawa watu kuna wengine wanakuwa na interest zao binafsi na hata tumeweza kushuhudia tuhuma dhidi ya hata hao wajumbe wa kamati ya nishat na madini ya kuhongwa na hata pia wabunge kuhongwa na hiyo wizara ya mhando....na zaidi hao wabunge ambao ndio wajumbe wa kamati wapo wenzao ambao wameshikwa na rushwa na kesi zao zipo mahakamani...kwa maana hiyo kumchelewesha mhando kwa kusubiria bodi na kamati ya nishati na madini mnatakiwa kufaham hao watalichukulia kisiasa zaidi kwasababu wengi wao watakuwa na masilahi yaleyale ya akina mbunge wa Bahi .....Mohamed Baladweiii
   
Loading...