Mhamiaji haramu akamatwa ndani ya sanduku la nguo!

ng'wandu

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2011
Posts
333
Reaction score
105
Je, ni kwa kiasi gani uko tayari kuhatarisha maisha yako ili uweze kufikia malengo yako? Kijana mmoja kutoka Mali huko Afrika ya Magharibi akiwa na ndoto za kufika Ulaya, mahali alipokuwa na matumaini kuwa ataweza kuishi maisha yaliyo bora zaidi, baada ya kujaribu kila mbinu za kufika Ulaya na kutokufanikiwa aliamua kuvushwa akiwa amefichwa ndani ya sanduku la nguo.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alikubaliana na mtu mmoja kutoka Morocco ambaye alimwingiza ndani ya sanduku lake la nguo ili amvushe kutoka Morocco hadi Melilla huko Spain.

Lakini kwa bahati mbaya maafisa wa uhamiaji walitilia shaka sanduku hilo na kumwomba mwenyewe alifungue ili waweze kulikagua.

Kuona hivyo, yule kijana mwenye sanduku aliona mambo yameshaharibika. Ghafla alitimua mbio akiliacha nyuma sanduku lake. Maafisa hao walilifungua sanduku hilo na kumkuta mhamiaji huyo akiwa kajikunyata ndani.

Makubwa hayo ya wahamiaji haramu na ndoto za kufika Ulaya.
immigrant.jpg

MHAMIAJI HARAMU AKAMATWA NDANI YA SANDUKU
 
kama ni maisha ni bora ukakubaliana na pato lako maana ukifanya kama dogo kufa kupo karibu. ...........vijana waache tamaa nani kawaambia maisha kule poa huo ni kuamini uongo daima hauwi ma ukweli.
 
Laiti wangejua kwamba Ulaya hapafai kama una kazi ya maana, wala wasinge hangaika kiasi hicho. Lakini angalau ndoto ya dogo imetimia, amenusa Ulaya hata wakimrudisha au kumfunga tayari amevuta hewa ya Europe.

Tiba
 
Ila kusemakweli Ulaya life ni nguma Kama huna kazi.. Huna mwenyeji Na Spain ni nchi ambayo haina hela wananche wao wenyewe wanakimbia nchi jirani km Germany, Swiss angala hapa kazi mtu anaweza pata Kama ana qualifications zinazohitajika.. Na pia km hujaoa au kuolewa huna chance.. Anyway, life Africa ni ngumu sana Na mtu km hajawahi kufika Ulaya anaona Ulaya km matawi ya miti kazi ni kudanda na kuchuma..
 
Back
Top Bottom