Mhadhiri udom mtegoni

Mhadhiri udom mtegoni

Miken

Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
15
Reaction score
1
Katika hali ya wahadhiri vyuo vikuu kuendelea kuwatumia wanachuo kama sehemu ya kutimizia haja zao na kuonyesha umaarufu wao,sasa umeingia sura mpya baada ya Mwalimu mmoja(jina tunalo)wiki iliyopita kujipambanua kama member wa Royal families na kuwadharau Wahadhiri wenzake kuwa wanawafundisha ujinga wanafunzi huku akijisahau na kumtaja hata mkuu wake wa kitengo ambaye wanachuo hao wanamheshimu kwa ufundishaji uliotukuka.Haikuishia hapo,aliendelea ku kuwadharau wanafunzi wanaosoma kozi tatu za Utawala wa umma,siasa na uhusiano wa kimataifa kuwa hawana pa kwenda kwa kuwa wamekuwa wakijidai kuwa wanajua kujenga hoja.Mhadhiri huyu aliendelea kuwaeleza wanazuoni hao kuwa anawachukia mno na ana mtazamo hasi dhidi yao,hakuishia hapo akaendelea kuwaeleza kuwa watafeli mno watake wasitake huku akiwapa matokeo ya test zao na kuwapiga 0 karibia darasa zima.Wakadhani kamaliza,akaendelea kuwaeleza kuwa walijiunga chuo wakiwa wachanga(huku zaidi ya nusu ya darasa wakiwa wanamzidi umri).Baada ya mhadhara huo,wanazuoni hao hawakuridhika na hoja hizo na inasemekana wameanza taratibu za kulishughulikia suala hilo na wengi wamejipanga kumkataa hata kama management itashinikiza kuendelea naye.
 
Someni bwana, hiyo ni sawa na kusema "I want a small class,....a teachable one......, this class is very big.....!!" Halafu at the end of of studies, kila mtu anafaulu na anakwenda kutumia elimu yake!
 
Acha woga, soma kw bidii
 
Wana udom pigeni kitabu achaneni na huyo leacturel sababu yeye sio mungu had awatabirie kuwa hamna kwa kwenda. "hayo ni maneno tu hata kwenye kanga yapo siku hiz hata kwenye t-shirt yapo".
 
Yni kila nikisoma thread karibu zote za udom zimekaa kimajungujungu, yani mnanifanya nikione chuo hiki kama high school na kwamba waliowachagua kujiunga na chuo hcho huenda walifanya makosa. Yani inshort sijaweza kuona kama thread zenu zimekaa kwa kujenga zaidi. Naona tu majungu, mara leo huyu amefanya hivi kesho vile.
 
Hata wakipiga kitabu ni kazi bure kwani mwisho wa siku atawapa 0%, wamdhibiti asiaribu maisha yao

Ninyi vijana acheni uvivu, kaeni chini mpige shule. Hakuna mtu yeyote atakae wabadilishia mwalimu. Acheni kuzoea shule lainilaini. Nendeni Library someni sana muelimike vizuri. Hamuwezi kuwa discontinued!!. Mimi pia ni mwalimu wa chuo kikuu. Hizo ni strategies za kuwafanya wanafunzi wasome kwa ku concentrate. Watu wengi huwa hawawezi kusoma bila ongoing pressure, na ndo maana huwa mitihani ikikaribia huwa watu wanasoma sana, sasa kwa nini soma ile isiwe kuanzia mwanzo wa semester?. Mimi mwenyewe nilipokuwa nasoma nilikuwa naambiwa hivyo hivyo, "darasa hili ni dogo sana na nyie watu ni wengi lakini tutajua cha kufanya". Mkitoka hapo kila mtu anasambaa liblary. lakini mnajikuta watu mnafaulu, ikitokea kukamatwa au disco hata watu wengine wote, deep down mnaona kabisa kuwa mwenzetu huyu alistahili. Si mnafahamu kufeli university is not accident, Huwa mtu unaona kabisa kwamba somo hili ninafeli, kwani Continous assessments huwa zinakuonesha kuwa unakoelekea ni kufeli. Na mtu akifeli maana yake ni mjumuisho wa CAs na UE. So kaeni chini msome muweke sawa hizo CAs. The quality of education should not be left to be compromised by students' politics. Kama mnataka kusoma ingieni madarasani msome.

Kumbukeni University, pamoja na kufundishwa taaluma zenu, pia mnafundishwa namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha. Siyo unatoka hapo hujapigwa stress hata kidogo, unaenda uraiani unapata challenge kidogo unakimbilia kujinyonga, badala ya kutumia akili na uvumilivu kutafuta ufumbuzi.
So kupigwa zero is part of life, kaeni msome. Hata hao waalimu wenu iko siku moja chuoni kwao walipata maksi za ajabu i.e single digits, wakaongeza bidii na ndo maana leo wako hapo. Sasa nyie endeleeni kulilia miteremko muone mtaishia wapi.

Mwisho kabisa natoa wito kwa mwalimu muhusika kama utasoma hii thread, nakuomba uzidi kukaza kamba, kwani hii ndo njia pekee itakayowafanya vijana hawa wasome kwa bidii na kutoka wakiwa na elimu ambayo watanzania wanatarajia watakua noyo. Napia walimu wengine wa vyuo tujitahidi kuwaweka bize vijana hawa kwani ndo namna pekee ya kuwafanya wafungue makaratasi kwenye vitabu.
 
  • Thanks
Reactions: aye
Pigeni kitabu kwa sana izo ni chalenge mnapewa ili msome msizoee lainilaini
 
Mtoa mada kama na wewe ni mwanafunzi hata mimi ningekukamata tu kwani inaonyesha unataka kuleta mipasho kwenye elimu ya chuo kikuu. Kwanza muda wa kukaa na kuandika ujinga huu umeupata wapi wakati test zimepamba moto?
 
Ulitoka kwenu alone,
In any case utarudi home alone
Achana na Upuuzi huo dogo Piga Book, ebo!!
 
Vijana wa Udom ndio waliomba mkopo wa laptop ili washinde JF. Mtakula majungu yenu wenzenu tuna kazi zetu na kiinua mgongo. Shaurienu.
 
Kuna mambo Tanzania kama nchi inabidi iangalie;

1. Kama wanafunzi wengi (25% or more) wanafeli kwenye somo fulani ni lazima mwalimu wa somo hilo ahojiwe na kujiridhisha kuwa kufeli huko ni kutokana na makosa ya wanafunzi wenyewe na sio mwalimu/lecturer.

2. Kwa vyuo vikuu, kila mwisho wa term au mwaka wanafunzi watoe maoni juu ya kila lecturer aliyewafundisha. Questionnaires zinaandaliwa na kuwepo na section ya maoni. hili lifanyike bila kuandika jina la mwanafunzi kwenye questionnaire paper. Hii itaondoa kabisa tabia ya lecturers ku-play hand of god na future za watu. Huwezi kumfelisha mwanafunzi kwa makusudi. Totally unacceptable.
 
Kufeli ni subjective sana na inaweza kutafsiriwa kwa namna nyingi zote sahihi. Mfano unaposema 25% unamaanisha nini? kikubwa tunaofundisha tunajua lazima katika kila course mwisho wa siku kuna "normal distribution". At least this can be a scientific measure in most instances kuliko hiyo percentage unayojadili. Kitu kingine cha kujiuliza kwa nini mwalimu ahojiwe tu wanafunzi idadi fulani wanapofeli, wakifaulu wote inakuwaje? Utanijibu lengo ni kufaulu na si kufeli.....fine! At least saikoloji inasema watu wawili wakipewa kazi kushughulikia jambo fulani yafuatayo yatatokea: kwanza wataliona jambo hili kwa njia mbili tofauti, na pili watajaribu kulitatua sawa na jinsi kila mmoja alivyoliona tangu mwanzo na hivyo majibu yao yanaweza kupishana. Pengine hii ni "relativism" kwa wanaoweza kunielewa. Hoja hii inanipelekea kujiuliza kuna kweli mbili au ukweli ni mmoja tu? Kama kweli ni nyingi, maana yake ni "no one size fits all" na pengine majibu ni mengi...? In essense, no one size fits all ni principle ambayo inamaanisha kwamba hakuna jibu moja sahihi katika sehemu tofautitofauti...lakini shuleni tunatoa the same exam and class lessons hivyo normal distribution should be obvious. Nimeandika kwa kirefu kuonesha kuwa elimu ni sector nyeti isiyotaka hata punje ya siasa ndani yake, vinginevyo vyuo vitageuka certificate factories.
 
Kufeli ni subjective sana na inaweza kutafsiriwa kwa namna nyingi zote sahihi. Mfano unaposema 25% unamaanisha nini? kikubwa tunaofundisha tunajua lazima katika kila course mwisho wa siku kuna "normal distribution". At least this can be a scientific measure in most instances kuliko hiyo percentage unayojadili. Kitu kingine cha kujiuliza kwa nini mwalimu ahojiwe tu wanafunzi idadi fulani wanapofeli, wakifaulu wote inakuwaje? Utanijibu lengo ni kufaulu na si kufeli.....fine! At least saikoloji inasema watu wawili wakipewa kazi kushughulikia jambo fulani yafuatayo yatatokea: kwanza wataliona jambo hili kwa njia mbili tofauti, na pili watajaribu kulitatua sawa na jinsi kila mmoja alivyoliona tangu mwanzo na hivyo majibu yao yanaweza kupishana. Pengine hii ni "relativism" kwa wanaoweza kunielewa. Hoja hii inanipelekea kujiuliza kuna kweli mbili au ukweli ni mmoja tu? Kama kweli ni nyingi, maana yake ni "no one size fits all" na pengine majibu ni mengi...? In essense, no one size fits all ni principle ambayo inamaanisha kwamba hakuna jibu moja sahihi katika sehemu tofautitofauti...lakini shuleni tunatoa the same exam and class lessons hivyo normal distribution should be obvious. Nimeandika kwa kirefu kuonesha kuwa elimu ni sector nyeti isiyotaka hata punje ya siasa ndani yake, vinginevyo vyuo vitageuka certificate factories.


25% or more ya idadi ya wanafunzi walifanya mtihani. Siongei siasa hapa hii ni method imefanyika sehemu nyingi duniani and it works. Waalimu nao I think huwa wanatoa evaluation report every year dhidi ya ufundishaji wao, na kama hii haifanyiki nadhani inatakiwa iangaliwe.Huwezi kutatua tatizo bila ya kupata maoni ya pande zote. Na huwezi kuboresha kitu kama hujui ni wapi hasa kunahitaji kuboreshwe. Kwa bahati nzuri mwaka jana nilikaa na baadhi ya wanafunzi wa law school toka chuo fulani and it was shocking to me waliponiambia idadi ya wanafunzi wanaorudia mtihani (nearly 40%). To me either, entry qualifications zina matatizo, au ufundishaji una matatizo, au wanafunzi ni wakarofi!!

Hata hivyo malalamiko ya lecturers kwa baadhi ya vyuo vikuu hapa nchini kufelisha wanafunzi hayajaanza leo. Na wanaokusanya hizi questionnaires ni special body inashughulika na 'education quality ya chuo husika'.

Hizi habari zingine za 'one size fits all' I am not sure what you are talking about but I hope I have clarified my point.
 
Back
Top Bottom