Mhadhiri Bashir Ally (UDSM) Atafutiwe Jimbo!

....

Ili Taifa liweze kunufaika na weledi wa Bwana Bashiru, naomba ashawishiwe kujiunga rasmi na siasa za majukwaani na atafutiwe jimbo ili kuanzia 2016 inshallah Taifa linufaike na vipawa vyake. ....
Kote huko tulikuwa pamoja ila kwa hili sikubaliani na wewe....yaani akiwa anafundisha taifa halinufaiki na vipawa vyake...au unataka kuniambia atakuwa mbunge na wakati huo akiwa mwalimu. Muache naye atengeneze watanzania wenye weledi kama yeye au hata kumzidi. Tumeona walimu/wahadhiri wengi waliojiunga na siasa wameshidwa kutumia vipawa vyao vizuri...hatutaki kumtumbukiza Bwana Bashiru huko.
 
Mimi nadhani aandike vitabu vya kitaaluma zaidi vitakavyosomwa na vijana hata akitoweka duniani kama Prof H Othaman. Lakini huku kwenye siasa kwa wanaomsikiliza BBC Swahili au DW akichangia mada mbali mbali hasa zinazohusu dunia mbili za Magharibi na Watu Mashariki ya kati huchelewi kuona biasses kwenye michango yake ikilalia upande mmoja. Unaweza ukashawishi watu zaidi kwa kuandika maandishi ambayo yanakuwa researched na kuwa-backed na facts zaidi kuliko hisia (emotions) za kiimani. Vinginevyo atabakia kuwa kama maprofesa wetu wengi bongo wanaosifika kwa title za u-profesa lakini hakuna vitabu maktaba walivyo andika, zaidi ni kuchangia articles kwenye majarida!

Wachangia hoja ambao utawasikiliza bila wewe kuhisi imani zao kuathiri uchambuzi (balanced analysis) wao ni kama Jenerali Ulimwengu, Zitto Kabwe na baadhi wengine...
 
Wewe mleta hoja yawezekana una matatizo, au kuna hisia fulani zimekusukuma kuandika uzi huu.
Mwanzoni sikuweza kung'amua unachokimaanisha ila nimekuja kukuelewa kwa hapa "agombee Bukoba Vijijini, hasa Ibwera au Katoro" why Ibwera na Katoro, na si kwingine? Je, ndiko anakozaliwa? Kwa mtu anayesoma tu bandiko lako hawezi kung'amua kitu gani au ni msukumo gani uliyo ndani ya moyo wako, isipokuwa kwa mtu anayeweza kuyasoma mazingira. Huyu jamaa unayempigia promo inasemekana ni mdini sana.
 
Hapo kwenye red: Unamaanisha Dr. Bashiru yupo kwenye kundi la Dr. Benson Bana; yule mpiga tarumbeta maarufu wa Lumumba? Kama yupo kwenye kundi hili naye hana maana zaidi ya wachumia tumbo.
Si kila Mhadhiri wa UDSM ni PHD holder....

Bashiru Ally sio Daktari wa Falsafa....Sio Dk. Kama unavyodhani...
 
Anafaa sana kuwa imamu wa msikiti!
Tukumbuke na ma-Imam pia wanafaa kuwa viongozi kama walivyo Mch. Msigwa (MB), Mch. G. Rwakatare (MB), Mch. Natse (MB), Mch. Mwanjelwa (MB) au alivyokuwa Dr.W.Slaa (retired-MB)
Wewe mleta hoja yawezekana una matatizo, au kuna hisia fulani zimekusukuma kuandika uzi huu.
...... Huyu jamaa unayempigia promo inasemekana ni mdini sana.
weka wazi matatizo yangu nipate kutafuta tiba. By the way "mdini" maana yake ni nini?
Definition ya mdini Hapa Tanzania ni Muislamu yoyote ambaye yupo katika wazifa wowote ule...
So sad, Poor us!
....Mdini mkubwa huyu hope anatumia kiarabu kufundisha huko na si Kiingereza .
Onyesheni udini wake badala ya kuandika kwa kutumia hisia zisizo na hata chembe ya ushahidi. Kwa nini kila mmoja anaandika tu bila ushahidi walau wa tukio moja linaloonyesha kuwa Mhadhiri Bashiru ni "mdini"? Kwa kuwa Kyenju, TUKUTUKU, Lunyungu na wenzenu mnaotoa tuhuma tu bila ushahidi, mie nikisema nyie ndio wadini wakubwa nitakuwa nakosea? Kwa nini mnakuwa na hisia kali juu ya majina kuliko uhalisia?
 

mbona waliomsifia ujawaomba watoe ushahidi?acha ujinga mkuu,huyu mtu wako anafaa sana kuwa imamu wa msikiti,kwani kuwa imamu wa msikiti ni kitu kibaya?
 
Ni haki yake kugombea nafasi yoyote, lakini sio lazima wasomi wote waingia kwenye siasa. Mwl Bashiru anafanya kazi nzuri UDSM, anaweza kuleta mabadiliko hapo alipo bila kuingia kwenye siasa kwa kufundisha vijana wengine waje kuleta mabadiliko.
 
mbona waliomsifia ujawaomba watoe ushahidi?
Tunawasha taa ili kuondoa mwanga au tunaondoa giza kwa kuwasha taa?
acha ujinga mkuu...
....dalili ya kukosa hoja!
mkuu,huyu mtu wako anafaa sana kuwa imamu wa msikiti,kwani kuwa imamu wa msikiti ni kitu kibaya?
uliposoma hii post ulielewa?
..tukumbuke na ma-imam pia wanafaa kuwa viongozi kama walivyo mch. Msigwa (mb), mch. G. Rwakatare (mb), mch. Natse (mb), mch. Mwanjelwa (mb) au alivyokuwa dr.w.slaa (retired-mb)
 
Hivi kila mjenga hoja akikimbilia bungeni wasomi watazalishwa na nani?
 
Ingawa naheshimu maoni yako ila jua kuwa siyo kila msomi mzuri lazima awe mwanasiasa. Anaweza kujenga nchi akiwa kule kule chuoni.
 
Mh! Mbona hiyo PhD yake hadi kesho hajaimaliza?!?
Bashiru Ally amepata promotion mwezi July 2013 kutoka Assistant Lecturer na kuwa Lecturer...Ameitafuta muda mrefu Phd kwa sababu ya ukiritimba uliopo kwenye system ya Elimu Tanzania huku wenzie wakienda Ulaya hususani Ujerumani na Uingereza na kurudi na Phd ndani ya miaka mitatu. Ni Mwalimu mzuri sana
 
Si kila Mhadhiri wa UDSM ni PHD holder....

Bashiru Ally sio Daktari wa Falsafa....Sio Dk. Kama unavyodhani...
Hujapata updates Mkuu....Jamaa amepata PhD Mwezi uliopita sasa ni Dr. Pita noticeboard pale UDSM utakuta tangazo la Promotion. Hata hivyo jamaa kasotea sana hiyo PhD
 
yawezekana ni hazina kama ulivyoeleza, lakini kwa sura yake na maeneo anayotoka yawezekana ni kati ya wanaotakiwa kurudi kwao. tumwachie kanali Masawe aendelee na kuhakiki uhalali wa wanaosadikiwa kuingia nchini bila kufuata taratibu
 

Si kweli kwamba wanavuma kwa sababu wanapewa AIR TIME, bali wanavuma kwa sababu kuna waliowaona kwamba ni mahiri na walipopata air time wakaitumia vizuri na kwa hiyo vyombo vya habari hupenda kuwatumia. lakini una hoja, kwa maana kwamba waandishi wa habari wenye kiburi cha utafiti, wanaweza kuwafuatilia wasomi na wachambuzi wengine wengi tu na kuwaibua. tatizo ni kwamba mwandishi au mwanahabari mwingine akitaka kupata maoni ya wachambuzi anawafuata hao hao. nadhani hawatutendei haki. binafsi nilishangaa wakati wa Kongamano la kujadili Amani Tanzania miaka 50 ijayo, lililoandaliwa na UDASA wiki mbili zilizopita, kwamba hawakutangaza mapema majina ya watoa mada. na kwa kweli ukiacha Ayoub Rioba, wale wawili; Prof. Bernadeta Killian na Bw. Onesmo (mwanasheria) sikuwahi kuwasikia katika anga za uchambuzi. lakini walidhihirisha kwamba ni wachambuzi mahiri sana na kwa hiyo tuwashukuru UDASA kwamba hawakutuletea watu wale wale, bali walitafuta "damu mpya".

Lakini kwa upande mwingine, hawa wanaovuma ni kwamba wanavuma kutokana na umahiri wao, na kwa kuwa vyombo vya habari pia vinapenda kuuza, wengi watapenda kusikia Bashiru kasema kitu gani kwenye ishu fulani. binafsi napenda sana kusikia uchambuzi wa Bashiru. jamaa namkubali sana tena sana tu.
 
nakubaliana na wewe tena inakuwa aibu unapokuta msomi mwenye hadhi ya Phd ama Prf. anakuwa weak - narrow sana anapokosolewa na kupewa changamoto na mtu kama Anna kilango, Pfo.Maji marefu, Serukamba etc wa aina hiyo. Hebu fikiria watu kama Dr.Msabaha walivyoaibika, au angalia Prof.Maghembe au Dr. Matayo Daudi Matayo, Prof.Tibaijuka, Prof.Msolla (Kilolo) ambao hata sijui wamekuwa majuha waliyosahau professionals zao - ila ni maoni yangu tu
 
Kwani nasi hatujui wakuu wa idara za kitaaluma na wahadhiri wanavyofanya kwa wanafunzi wakiislamu na mabaya kwa wakristo kusudi muonekane mnafaulu kumbe wapi majina yenu

Kilalo tuambie yafanywayo na wakuu wa idara kwa wanafunz wa kiislam na chuo waweza kitaja pia
 
Last edited by a moderator:

binafsi si mhadhiri lakini huwa napigiwa simu na Idhaa ya Kiswahili ya DW,Pamoja na Redio Iran na huwa natoa uchambuzi,kwa mara ya Mwisho Ujio wa Obama,Nilipigiwa Sim na DW redio na nikatoa maoni yangu juu ya UJIO WA MJALUO OBAMA,nadhan pia hivi vyombo vya habar huwa vinaangalia jinsi unavyoweza kujieleza
 

niliskia anaifanyia Ujeruman,since 2010,,,,hajamaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…