Mh. Wassira apokelewa kwa kishindo Bunda

Mh. Wassira apokelewa kwa kishindo Bunda

msemakweli tza

Senior Member
Joined
Sep 25, 2014
Posts
177
Reaction score
10
Waziri wa nchi ofisi ya Rais mahusiano na uratibu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bunda mkoan Mara jana tarehe 19/10/2014 ameshitushwa baada ya kukutana na mapokezi makubwa ambayo hayajawahi kutokea jimboni humo ambayo yaliandaliwa na wananchi kwa malengno ya kumpongeza shujaa wao juhudi kubwa na uzalendo wa hali ya juu wa kufanikisha upatikanaji au kukamilika kwa katiba inayo pendekezwa.

Hata hivyo mh. Wasira kwa furaha na kujiamini alifafanua baadhi vipengele vya katiba vikiwemo ukomo wa ubunge,maadili ya viongozi nk na wananchi walifurahishwa na ufafanuzi huo.
 
Kishindo kikowapi? Nilitegemea angalau utupie angalau kapicha kuthibitisha habari yako hii! Fanya hivo basi.
 
Sawa mkuu mimi bado nipo mwaka 2014 huko
tarehe 19/20/2024 mimi bado kabisaa...Endeleeni kusherehekea labda tutaonana!
 
Kwa kishindo? Mzimu wa Bulaya na Warioba unamtesa
 
duuhh...mleta mada ana mzaha sana..19/20/2024?????????????????????????????????????????
 
labda amepokewa na wale wavuta bangi mbona hamna picha huu ni uhuni kiboko wa wassira ni Esther Bulaya tuu
 
Wassira Vs Wafanyakazi.jpg
 
Eti anataka urais atapewa na nani huyo jimbo limemshinda ataweza upresidaar.
 
Hii ni baada ya Kamanda Nyerere kufanya mambo bunda .... na bado!
 
waziri wa nchi ofisi ya rais mahusiano na iratibu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la bunda mkoan mara jana tarehe 19/20/2024 ameshitushwa baada ya kukutana na mapokezi makubwa ambayo hayajawahi kutokea jimboni humo ambayo yaliandaliwa na wananchi kwa malengo ya kumpongeza shujaa wao juhudi kubwa na uzalendo wa hali ya juu wa kufanikisha upatikanaji au kukamilika kwa katiba inayo pendekezwa.

Hata hivyo mh. Wasira kwa furaha na kujiamini alifafanua baadhi vipengele vya katiba vikiwemo ukomo wa ubunge,maadili ya viongozi nk na wananchi walifurahishwa na ufafanuzi huo.
yani wewe mwehu kweli mara iratibu na bunge mara 2024 umevuta bangiii??? Unaandika kama unakimbizwa! ! Umbea mtupu
 
labda amepokewa na wale wavuta bangi mbona hamna picha huu ni uhuni kiboko wa wassira ni Esther Bulaya tuu

unautani na chuki wewe atakuja hapa na povu jingi sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom