Mh Warioba,rasimu yako iko wapi??

Mh Warioba,rasimu yako iko wapi??

Boeing

Senior Member
Joined
Apr 16, 2017
Posts
151
Reaction score
422
Tumeshuhudia yaliyotokea Kenya!! Ndiyo uliyopendekeza kwenye rasimu yako. Tumeitupilia mbali tunaishi unafiki usiofuata katiba yoyote,iwe ile mbovu iliyopo wala isiyokuwepo duniani. Tafadhali baba rudi na rasimu yako.

Kenya pamoja na uchanga wake,pamoja na ushiriki wake Mdogo katika ukombozi kwa nchi za Afrika,imeongoza kuwa nchi ya kidemokrasia.
Tafadhali baba rudi na rasimu yako.

Wakati Kenya wakiwa na mihimili mitatu iliyo na nguvu na heshima katika Taifa,sisi hatuna jaji mkuu,mahakama imekuwa briefcase ya mh. Asipoifungua hakua haki inayotoka na kinyune chake.
Tafadhali baba rudi na rasimu yako.
HONGERA KENYA KUWA KIOO CHA DEMOKRASIA AFRIKA. NATAMANI KUWA MWANAKENYA.
 
Kweli tunachakujifunza kutoka Kenya.Bila katiba mpya 2020 sijisumbui kupiga Kura.
 
Rasimu ya Warioba ilirekebishwa na CCM wabunge ukawa walipinga.
Hivyo hakuna chochote cha kulingansha kenyaa na Tanzania.
Kenya ni kitu kingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania kwa kutembea na matukio nawaaminia, Diamond akimtukana Kiba mnasahau hizo habar ya katiba
 
Kikwete ndiye anajua alipoweka maoni yetu yaliyokusanywa na Warioba!
 
Jamani jamaa alishasema hapangiwi cha kufanya na pia aliwahi kusema KATIBA MPYA sio kipaumbele chake yeye anataka Kazi Tu.

Kwa style hiyo juhudi zote za Mzee Warioba zimekufa kifoo cha mende. Yule kijana wake ndio keshapewa kitengo cha uenezi wa chama sidhani tena kama atakuwa na msimo + udhubutu wa kuhoji kama aliokuwa nao kipindi kile kabla ya kukabidhiwa kitengo.

Ama kweli safari yetu bado ni ndefu saana. Leo hii kwa katiba hii hii bado kuna watu wanajaribu kudai eti jamaa aongezewe muda wa kutawala...
"NAKULILIA TANZANIA YANGU"
 
Back
Top Bottom