Mh waziri sisi wakazi wa mwanagati, kitunda Ilalla tumechoka na mateso
Tumekuwa kukivamiwa mara kwa mara na majambazi kuibiwa, kuteswa na pengine watu kupoteza maisha, hali hii inasababishwa na mapori mengi yaliyoko maeneno ya mwanagati. Mapori haya ni viwanja vya wafanyakazi wengi wa wizara ya ardhi ambao walijigawia huku wakiwa hawana uwezo wa kuyaendeleza na sasa yamegeuka kuwa mapori ya kufichia kila aina ya waarifu. Mh waziri sisi wakazi wa mwanagati tumeshafanya kila jitihada ya kusaidiwa ili swala lakini linaonekana kuwa sugu kwa sababu wahusika wanaotakiwa kutoa suluhisho ndo wenye maeneo hayo, hivyo basi tunakuomba utusaidie kutafuta suluhisho ya tatizo hili, hili nasi tuishi kwa amani ndani ya nchi yetu.
Pia kuna tatizo la viwanja vya wazi, wafanyakazi wa ardhi wameviuza na vingine kugawa hali inayopelekea kukosa maeneo ya wazi kwa ajili ya shughuli mbalimbali, tunakuomba pia uliangalie na hili maana nalo ni kero sana
Ninatumaini mh waziri utaliona huili na kulichukulia kwa uzito unaostaili.