Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Wanahisa wa kampuni huwa na haki ya kuthibisha wakurugenzi wote waliopendekezwa kuwa kwenye bodi ya wakurugenzi. Bodi ya wakurugenzi ina wakurugenzi wa aina mbili. Kundi la kwa kwanza linakuwa na wakurugenzi ambao wanafanya kazi muda wote kwenye kampuni (kwa kiingereza executive directors). kundi la pili linakuwa na wakurugenzi ambao hawafanyi kazi muda wote kwenye kampuni (kwa kiingereza non-executive directors). MAKUNDI YOTE MAWILI YANATHIBITISHWA NA WANAHISA SIKU YA KIKAO CHA MWISHO WA MWAKA WA FEDHA WA KAMPUNI HUSIKA. Kwahiyo basi CRDB itakuwa imepitisha wakurugenzi wa bodi leo ambapo Sumaye naye amedhibitishwa kuwa mkurugenzi. kwakuwa sikuwepo wala sijasikia agenda na wakurugenzi watarajiwa wa kampuni hiyo sijui kama amethibitishwa kuwa mkurugenzi wa kundi la kwanza au la pili. Ila mara nyingi sitegemi waziri mkuu mstafu awe executive director. Nadhani maelezo haya yatakuwa yamesaidia kiasi kwa watu kuelewa taratibu za uongozi kwenye makampuni duniani.
Mkuu uko sahihi. Non-executive directors huchaguliwa, executive directors huomba kazi na kuhojiwa na bodi ya wakurugenzi ama kamati ya bodi hiyo nadhani kisha wanapata baraka za AGM. Hawa executive directors huunda Management Team.