Chipolopolo
JF-Expert Member
- Feb 14, 2012
- 1,425
- 725
Mahali ni pale pale. Msafara uleule. Spidi ile ile ya mbio za mwenge. Wakati msafara wa Makamu wa Rais Dk. Mohammed Bilal ukipita eneo la Kabwe- Mwanjelwa Mbeya kuelekea mashariki ya jiji hili lenye changamoto kadhaa za kisiasa, baada ya muda mfupi msafara ukiwa umetokomea, zilisikika kelele za shangwe eneo hilo la Kabwe.
Gari likitembea kwa mwendo wa polepole huku likiwa linasindikizwa na kundi kubwa na vijana wakishangilia.Ndipo ilibainika kuwa aliyekuwa amezingirwa na kusababisha msururu wa magari kuwa mkubwa ni Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu.
Akiwa amevalia mawani ya makubwa ya jua, na kombati la CDM, alitumia dakika kadhaa kuwasalimia wananchi akiwa ndani ya gari kisha kuwaomba wamruhusu aendelee na safari. Akaruhusiwa kisha akaondoka.
Haikufahamika mara moja kwanini hakuambatana na ule msafara wa mbio za mwenge?