Mh. Sitta alikuwa baba asiye na mfano

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Kila ninapoangalia vikao vya Bunge vinavyoendelea naishia kumbuka Baba mpendwa Mh. Sitta alivyokuwa mahiri katika kuungoza mhimili muhimu wa nchi. Kwangu mimi alikuwa baba mwenye kuijua vizuri familia yake (bunge) na wakati wote alitenda bila kuangalia kuwa huyu ni mtoto wa nyumba kubwa au nyumba ndogo. Kwakwe yeye wabunge wooooootre walikuwa sawa.

Umuhimu wa kuwa na Spika mahiri umejionyesha baada ya Baba wa familia kuondoka na mama kuanza kuongoza nyumba. Kwa kweli alichoweza kukifanya ni kuanza kwa ubaguzi wa kusema huyu ni wangu wa kumzaa na yule ni mke mwenza. Matokeo yake kazi za Bunge zimekuwa za kihuni na kizushi kabisa. Inapotokea mtoto wa kumzaa yeye hata akisema uongo au uzushi mama humtazama na kumpongeza. Inapotokea mtoto wa mke mwenza akisema jambo lenye maslahi kwa familia mama humkaripia na kumfanya aonekane kituko kwa wengi.

Mlio makini ni kuwa Bunge letu kwa sasa ni la kihuni na halina maslahi ya dhati kwa Taifa. Badala ya kuzingatia na kuweka wananchi kwanza Bunge linaendelea kuweka maslahi ya vyama aka Chama mbele na matokeo yake tutaendelea kuumia. Vituko vilivyotokea kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa vinatosha kusema kuwa mama kashindwa kulea familia iliyoachwa na Baba yetu mpendwa


BABA TUTAKUKUMBUKA DAIMA KWA KUTUUNGANISHA WATOTO WA FAMILIA ZA MAMA MBALIMBALI KWA MANUGFAA YA FAMILIA.

LONG LIVE MH. SAMWEL SITTA - MZEE WA SPIDI NA VIWANGO
 
Usimpambe sana, huyu jamaa pia ana mapungufu yake mengi tu:
 
Usimpambe sana, huyu jamaa pia ana mapungufu yake mengi tu:

Nakubaliana kabisa na FUSO kuwa Baba huyu alikuwa na mapungufu meeeengi sana lakini ni wazi kuwa aliweza kumudu kuliongoza Bunge kwa spidi na viwango vya hali ya juu kitu ambacho kwa sasa kimepotea kabisa. Think big
 
Back
Top Bottom