Mh. Riwa nisaidie hili tafadhari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Riwa nisaidie hili tafadhari!

Discussion in 'JF Doctor' started by kiparah, Apr 1, 2011.

 1. k

  kiparah JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  1. Hivi ni kweli kwamba mtu mwenye HIV akivunjika mguu, mkono na popote kwenye mfupa hawezi kuunga?
  2. Ni kweli kwamba mgonjwa wa HIV akiwa na kidonda kikubwa hawezi kupona?
  3. Kwanini ukinywa pombe ukipata ajali hauwezi kuchomwa sindano yoyote hadi pombe ikitoke kichwani, hakuna dawa ya kutoa ulevi kichwani?

  NB: Ni hayo, nimekutaja Riwa kwa sababu naona u-mtaalamu wa mamabo haya, lakini kwa yeyote yule anayeweza kunisaidia kujua haya anakaribishwa.
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  1. Si kweli. Mtu mwenye HIV mifupa yake inaunga kama mifupa ya mtu mwingine yeyote pindi mfupa unapovunjika.
  2. Mtu mwenye HIV huwa anapata upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI/AIDS) pale CD4 cells zake zinapopungua sana, hali hii humuweka karika uwezekano wa kushambuliwa na maambukizi ya kila mara kwa sababu mwili wake unashindwa kupigana na magonjwa. Kidonda chochote huwa hakiponi kinapokuwa na maambuki ya bacteria hata kwa watu wasio na HIV, lakini mgonjwa wa HIV yuko kwenye risk kubwa ya kupata haya maambukizi ya bacteria kutokana na kupungukiwa na kinga ya mwili. Kwa hiyo kidonda chake kisipotunzwa katika hali ya usafi anaweza pata maambukizi na kuchelewa kupona.
  Ushauri: Kuweka kidonda kiwe kisafi na kumpa antibiotics kutasaidia kidonda chake kupona mapema.
  3. Pombe inaponywewa huwa inanyonywa na kuingia kwenye damu ili kuweza kufikia ubongo na kuleta zile effect zake kama euphoria (kuchangamka), stupor (kuzima) au coma (kuzimia). Pombe inatoka kwenye damu kwa kuvunjwa vunjwa na maini kisha kuchujwa kwenye mafigo na kutoka kama mkojo. Sijajua bado dawa ambayounaweza kunywa au kuchomwa ili pombe itoke kwenye damu au kichwani. Ila kunywa maji mengi kunaweza harakisha process hiyo ya kuchujwa kupitia mafigo.

  Unapokunwa au kuchomwa dawa nayo huwa inanyonywa na kingia katika damu ili kuweza kufanya kazi yake. Hivyo kama umekunywa pombe, Dawa na pombe zote hukutana kwenye damu. Kuna dawa amabazo zina'interact' na pombe na kusababisha athari kwa mgonjwa. Kuna dawa ambazo huzuiwa kufanya kazi vizuri zinapokutana na pombe kwenye damu mfano dawa nyingi za Malaria, HIV, TB (kifua kikuu), Kisukari etc, na kuna dawa ambazo huongezwa nguvu na kumdhuru mtumiaji zinapokutana na pombe kwenye damu...mfano mzuri dawa za jamii ya Flagyl, dawa za shinikizo la damu (Pressure) etc.

  Unapotaja ajali kama umeumia na unahitaji mfano kutumia dawa ya ganzi...dawa za ganzi zina effect ya kulaza, na pombe ikizidi huwa na effect hiyo pia. Kwa hiyo unaweza ukamlaza mgonjwa ukijumlisha effect ya pombe akalala moja kwa moja asiamke. Kwa hiyo ni hopsitali kubwa tu zenye uwezo wa vifaa na wajuzi wenye kuweza kutoa matibabu yatakayohitaji ganzi wakati umelewa.
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Ukitaja jina langu kwenye title ya thread unazuia watu wengine wasichangie. Nafahamu wenzangu wengi tu kwenye fani ya afya ambao wako humu, na michango yao ni ya muhimu sana kwani kuna areas za kitabibu ambazo nina mapungufu nazo.
   
 4. k

  kiparah JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,176
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa maelekezo yako... pia nashukuru kwa kunihabarisa kwamba kuna wengine wanajua na nisingestahiri kukutaja wewe moja kwa moja, Asante sana Mkuu.
   
 5. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaaaaaa mkuu usiogope kutuhabarisha!
   
Loading...