Mh Rais watie ndani kina Mwanakijiji!

Status
Not open for further replies.
Sijaelewa unataka rais atoe maelezo anahusikaje na Dowans au amtie ndani Mwanakijiji????
 
Nimekuwa nikifuatilia makala mbalimbali za huyu mtu anaitwa Mwanakijiji, katika makala hizo anaonekana ni mtu wenye ufahamu mzuri, mbali ya kuwa data za kumwaga! Lakini kuna hili la kumtajataja Mh RAIS ..linanitia Jakamoyo! Hata kama sikumchagua LAKINI ...!

Katika makala ya Tanzania Dima JANA jamaa anasema wazi kuwa Rais aeleze anahusikaje suala la DOWANS! Hapa haulizi kama alihusika ! Anahoji alihusikaje !

Kwa mamlaka aliyopewa Rais na katiba yetu shutma hizi ni nzito .....! Mkuu anatakiwa aibuke azitolee maelezo au awashughulikie wanaomsema ...la sivyo kama hana majibu, basi wenye akili tutaanza kuoona ni kweli! Na kumbuka hata uongo ukirudiwarudiwa, unabadilishwa na kuwa ukweli! BABA inuka useme, au basi wadhibiti watu wako ...kama unaweza!

Kinyume cha hapo hawa kina Mwanakijiji wataendelea kukuharibu ...au labda unajiharibia mwenyewe!

Kumbuka watu hawa ni wengi, muulize yalivyomwuuliza TYSON wako kule Bunda, je unajuaje ni Watanzania wote wanajiuliza maswali hayo?

Usiende mbali sana ndugu yangu mtu wa kwanza kumshitaki alikuwa ni Dr Wilbload Slaa ambaye alimtaja wazi wazi ndugu kikwete' kwamba ni fisadi katika orodha yake ya watu 11, lakini kakaa kimya na hii ni inaweza kuwa ni kwasababu hana la kujitetea na ninavyo mfahamu huyu mtu kwa fitina angekuwa hana hatia Slaa kwa sasa angekuwa ananyea ndoo.
 
Niliwahi kusoma makala ya mwanakijiji kuhusu CCJ kwamba chama makini kitaleta changes two days later hamna cha CCJ wala harufu yake.
Mwanakijiji mbona kawaida tu wanaomsujudia poa tu lakni kwa ufupi HAJULIKANI hatujawahi ona kaalikwa hata kwenye tv kama wachambuzi wengine.
Kuhusu kujibu jk anaamini katika uhuru wa kutoa maoni..mwanakijiji analijua hilo ndo maana anaropoka bila breki angejaribu enzi za Nyerere ama hata mkapa angefia kizuizini.
Na jk hana shida ya kujibu kwa shinikizo la akina mwanakijiji .
Mwanakijiji alikua wapi kumuuliza mkapa kuhusu umiliki wake wa benki M

Kikwete anapenda sana kujibu hoja za wasomi wengi ila uwezo huo hana, he is not able to build strong arguments zilizoshiba shule.

Nasema hivyo kwa sababu kwa kiwango cha ujiko na kupenda sifa alichokuwa nacho mkulu kama angejaliwa uwezo wa kuchambua mambo basi tungekuwa kila siku tunamuona kwenye luninga akishusha shule.

Ukweli ni kwamba anatamani sana angekuwa na uwezo wa kujibu hizo hoja ila ni wazi kuwa area ya kujenga hoja imempita kushoto kabisa. Sad though!
 
Kuna watu wanashangaza sana.......,kwa mtanzania mzalendo hawezi kuropoka kama KYALOSANGI.Nadhani angeshauri rais awajibike kwa uhusika wake na ukimya wake katika suala zito kama hili........,Pia ni uelewa finyu wa kutaka kuipeleka nchi hii kwenye full dictatorship.Rais hana mamlaka ya kumfunga raia yeyote bila sababu..........ebu kuweni wazalendo na sio watumia matumbo
 
Ieleweke rais ana mamlaka ya kuwaweka watu kizuizini kwa muda wowote anaotaka yeye, shida inakuja unaweka mtu jela kwa sababu gani?
Amini usiamini unapoanza vita na watu weledi tena wenye kujua mambo jua unaukaribisha mwisho wa utawala wako, hebu jiulize mwanakijiji aliipata wapi ripoti ya akina mwakyembe na mambo mengine mengi tu. Bila shaka huyu jamaa ni mjuzi wa mambo mengi hivyo kudeal na watu kama hao huwa inahitaji akili kuliko nguvu.
Mwisho sidhani kama ni suluhu kukamata watu wanakusema mapungufu yako kwani unaweza kujaza jela zote mpaka ukakosa pa kuwaweka na siku wakitoka jua nawe upo mashakani.
 
Mawazo ya mtoa hoja hayajakaa bayana. Kichwa cha thread hakiendan na ulichokifafanua.Je upeo wako unakuonesha alihusika au la? Je unahisi angekuwa hajahusika si wapambe wake wangekuwa washawafungulia mashitaka watu wajasiri wanaotamka bayana ukweli?
 
Nimekuwa nikifuatilia makala mbalimbali za huyu mtu anaitwa Mwanakijiji, katika makala hizo anaonekana ni mtu wenye ufahamu mzuri, mbali ya kuwa data za kumwaga! Lakini kuna hili la kumtajataja Mh RAIS ..linanitia Jakamoyo! Hata kama sikumchagua LAKINI ...!

Katika makala ya Tanzania Dima JANA jamaa anasema wazi kuwa Rais aeleze anahusikaje suala la DOWANS! Hapa haulizi kama alihusika ! Anahoji alihusikaje !

Kwa mamlaka aliyopewa Rais na katiba yetu shutma hizi ni nzito .....! Mkuu anatakiwa aibuke azitolee maelezo au awashughulikie wanaomsema ...la sivyo kama hana majibu, basi wenye akili tutaanza kuoona ni kweli! Na kumbuka hata uongo ukirudiwarudiwa, unabadilishwa na kuwa ukweli! BABA inuka useme, au basi wadhibiti watu wako ...kama unaweza!

Kinyume cha hapo hawa kina Mwanakijiji wataendelea kukuharibu ...au labda unajiharibia mwenyewe!

Kumbuka watu hawa ni wengi, muulize yalivyomwuuliza TYSON wako kule Bunda, je unajuaje ni Watanzania wote wanajiuliza maswali hayo?


Timing Mbaya MH Vyeo vya kuchaguliwa vimeisha.
Hata hivyo umejitahidi.
 
Rais hana uwezo wa kuondoa fikra zinazopinga uozo wa serikali yake. Ni wengi tuna uelewa wa haki zetu si mwanakijiji pekee. Mbona haki hizo zipo katika katiba yetu?? unafiki wako na kujipendekeza ndio sababu ya kuogopa na hata pale unapokuwa na haki ya kusema/kuhoji. Tanzania ya leo hata angekuwepo Nyerere asingeweza kuzuia watu kuhoji utandawazi umepanua demokrasia.
 
Kama JK kidume kweli ajaribu. JK ni dhaifu mno hawezi kitu ndiyo maana hata midahalo na wasomi anaogopa, yeye ni chalii wa kisiasa tu, msanii tu huyu mkwere.
 
Kwa ulichoandika halafu unasema hukumpigia Kikwete kura? Ulichoandika unaonyesha kabisa wewe ni kibaraka wa Kikwete. Katiba tuliyonayo japo si living document japo inabidi iwe ni document inayoishi bado haimpi hayo mamlaka huyo mkwere wako. Nashangaa sana kama katika dhama hizi, na ulipo yawezekana huna maisha ya maana lkn unajilazimisha kuamini kwamba Mungu ndie aliepanga uwe hivyo kumbe ni serikali dhalimu ya CCM. Get a life dude!
 
Mimi ningekushauri umshauri huyu Rais awakamate na kuwatia ndani waliowadanganya watu kuwa "ni chaguo la Mungu" wakati sio kweli bali kwa vile watu wanamwogopa Mungu waliona wasiende tofauti naye. Pia aweke ndani wote wanaoeneza uvumi kuwa Rais anawapenda WaTZ na nchi hii wakati sio kweli ndio maana anaruhusu madude kama Richmond,EPA,Dowans nk ambayo ndio kiini cha mateso ya Walalahoi wa nchi hii.
Hata mie napenda nimshauri Rais kamata wote wanaokusingizia wewe ni chaguo la Mungu wakati wewe ni chaguo la akinas RA. wasemao wewe unapenda nchi hii wakati ni kukuzushia tuu, maana hilo halipo. Weka ndani hao kwa kuhatarisha amani ya nchi kwa kusema uongo dhidi ya Rais,kumwelezea ndivyo sivyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom