Mh. Rais, Wabunge wa CCM Wanakuponza!

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,041
1,250
Mh.Rais wetu kwanza nikupongeze na pia nikupe pole kwa uchovu wa kazi nzito uzitendazo.

Naomba nikupe maoni yangu kwa hili suala la madini na raslimali zetu. Katika eneo hili nikuambie tu wabunge wa CCM hawakusaidii. Hebu mwenyewe jaribu kuwasikiliza wakiongelea jambo hili makinikia na madini kisha unukuu hoja/points katika maelezo yao halafu uzitafakari na kisha uone kama zitakusaidia uweze kutoka katika mtanzuko huu kwa namna utarajiayo!

Hebu funguka, utaelewa hii vita siya kitoto. Tukienda kwa hoja za wabunge wengi wa ccm utakwama. Hawajengi hoja, wao ni mapambio tu kwako mkuu. Wanakuponza rais wetu. Wale ni ma opportunist tu. CCM wanakungamiza rais na wanaliangamiza taiga.

(Mod.naomba msiuunganishe Uzi huu na nyinginezo)
 
kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
3,954
2,000
Si wabunge hapa ni executive na parliament kwa umoja wake
Rejea ishu ya kutaka kumng'oa PM, anko aliwafunga mikono
kwa hiyo wabunge wa ccm wayafanyayo mjengoni ni echo ya anko pale magogoni
 
spika

JF-Expert Member
Dec 7, 2014
458
500
Ngoja wampitishie bajeti aliyoiwasilisha kwao halafu ikifika septemba akumbuke kwamba bado Rwanda wanatuzidi kwa idadi ya ndege, au kasi ya kuhamia Dodoma ni ndogo..ndio utaelewa ni upande gani unapaswa kushauriwa.
 
Dahafrazeril

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,501
2,000
Sabalkheri Mshauri wa Rais.

Hivi Rais si alikuwa Mbunge kabla ya huu wadhfa alio nao hivi sasa?.Au ndiyo kusema kashazeeka sasa, hivyo kawa Malaika?.

Kama wabunge wa CCM hawamshauri vyema Rais, Je awasikilize kina nani?. Wabunge wa upinzani?.Kama ndiyo, huoni kuwa wabunge wa upinzani watapigwa BAN kama wanavyozungumzaga pasipo kupepesa macho?.

Tulipofikia sasa ni kwamba ukizungumza ukweli ni shida.Na pia ukizungumza uongo ni shida.Hatuna tofauti na chumvi katika chakula.Ikizidi sana watu wanalalamika, pia ikipungua watu wanalalamika.

If you close your eyes to facts, You'll learn through accident.Lets learn through accident.

[HASHTAG]#PressFreedom[/HASHTAG] [HASHTAG]#UhuruWaHabari[/HASHTAG]
 
  • Thanks
Reactions: MTK

MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,255
2,000
Yeye ni Rais anayejiamini, tena ukimwambia fanya hivi au vile ndio umeharibu kabisaaaa!
 
Abuha

JF-Expert Member
Feb 5, 2017
304
250
Mh.Rais wetu kwanza nikupongeze na pia nikupe pole kwa uchovu wa kazi nzito uzitendazo.

Naomba nikupe maoni yangu kwa hili suala la madini na raslimali zetu. Katika eneo hili nikuambie tu wabunge wa CCM hawakusaidii. Hebu mwenyewe jaribu kuwasikiliza wakiongelea jambo hili makinikia na madini kisha unukuu hoja/points katika maelezo yao halafu uzitafakari na kisha uone kama zitakusaidia uweze kutoka katika mtanzuko huu kwa namna utarajiayo!

Hebu funguka, utaelewa hii vita siya kitoto. Tukienda kwa hoja za wabunge wengi wa ccm utakwama. Hawajengi hoja, wao ni mapambio tu kwako mkuu. Wanakuponza rais wetu. Wale ni ma opportunist tu. CCM wanakungamiza rais na wanaliangamiza taiga.

(Mod.naomba msiuunganishe Uzi huu na nyinginezo)
Ni kweli kabisa,masuala ya msingi,kuhusu hili,wabunge wa upinzani,ndio wanaoweka wazi suala hili kitaalamu,sababu kubwa ,Ni Kuwa CCM wengi wanajua kusoma na kuandika tu.
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
47,687
2,000
Wabunge wenyewe vilaza. Hata hiyo mikataba wakipewa hawataelewa kilichoandikwa.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
5,678
2,000
Anajipotosha mwenyewe.
Amejawa na visasi
Hashauriki
Hapangiwi
Mpenda sifa
Dikteta

Acha akalie hicho kiti, lkn siku nikishika madaraka mm nitaondoa kinga kwa marais ili nimshughulikie
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
8,985
2,000
Mwenyewe anasema huo urais hakupewa na mtu na hasikilizi mtu. Tumwache aendelee kusikiliza moyo wake
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,322
2,000
wabunge wa CCM hawakusaidii. Wanakuponza rais wetu. Wale ni ma opportunist tu. CCM wanakungamiza rais na wanaliangamiza taifa.
Ukimpigia mbuzi gitaa, wimbo ukiwa mzuri sana, kuna wakati mbuzi huwa anacheza, hivyo kumpigia mbuzi gitaa imo!.

Paskali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom