Mh. Rais Magufuli, Itumie JamiiForums kupima na kutathmini kazi yako

ndoze

JF-Expert Member
Sep 2, 2016
1,187
1,108
Mheshimiwa nikuombe kwa dhati kabisa yatumie maoni ya wanajf kupima kama ulichokifanya au unachotaka kufanya ni kizur au laa na kujua kama kimepokelewaje kwenye jamii ya watanzania.

Achana na tafiti za Twaweza, wanakudanganya hao ili wapate vyeo kutoka kwako, na pia CCM na subordinates wako wengine hawawezi kukukosoa sababu wanaogopa utawatumbua na CCM watakusifia katika kila jambo sababu wanataka uwape vyeo.

Lakini hapa hapa JamiiForums, Waziri Mkuu, mama Samia, na subordinates wako wengine wanaweza wakaja na ID tofauti wakakupinga katika jambo ulilolifanya lakini ana kwa ana hawawezi sababu wanaogopa utawatumbua baaba na wao wanataka kaugali ka watoto.

Njoo Jamiiforum chukulia watu walioko humu kama sample yako ya kufanya utafiti sababu wanakuja na fake ID kwahiyo wanaweza kutoa mawazo kwa uhuru.

Mwisho nikuombe utuachie kauhuru humu JF sasa mikutano umezuia baba tuachie basi JF yetu tutoe mawazo kwa uhuru, tunaomba mwanzilishi wetu Maxence Melo asibughuziwe tena.
 
Kwa mfano waziri mkuu na mama Samia sidhani kama wangekua na uhuru wa kuongea wanakubaliana na jinsi ulivyolishughulikia swala la kagera, ajira mpya, unavyonunua ndege hata Kama wananchi tunaumia, wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo, mi naamini hao viongozi wako wanakupinga na wanakujaga kuanzisha threads za kukunanga humu jf na ndio wanao kuporomoshea matusii hapa ukiwakera huko ofisini
 
Yeye huo ukweli ndio haupendi kuusikia sababu unamkera lakini kuwakera waathirika wa tetemeko,watumishi wa umma,wafanyabiashara,waanafunzi anasikia raha..nahisi huwaga anasomaga humu huku kafumba kijicho kimoja.
aitumie jf kuchukua ushauri na kuimarisha na kurekebisha anapokosea.
 
Kila siku tunapiga kelele mafisadi wa lugumi,escrow,richmond,boti mbovu,nyumba za serikali wafikishwe kwa pilato..tunachoambiwa ni kuwa mahakama ya mafisadi imekosa wateja wakati wapo mtaani wanadunda
tena lugumi hii ya juzi bado mbichi kabisa lakini hakuna aliyefikishwa mahakamani, halafu wanatuambia eti raisi hapendi ufisadi, kafanya nini ili tuseme kweli raisi wetu anachukia ufisadi?
 
tena lugumi hii ya juzi bado mbichi kabisa lakini hakuna aliyefikishwa mahakamani, halafu wanatuambia eti raisi hapendi ufisadi, kafanya nini ili tuseme kweli raisi wetu anachukia ufisadi?
Mwenye lughumi ni swaiba wake
 
Raisi anasema yeye anapenda ukweli lakini sidhani kama ni kweli kwasababu hataki kukosolewa kwa maana hiyo hataki kusikia ukweli,
Humu jf ataupata ukwel tena sio ukweli tu bali ukweli mchungu.
 
Mheshimiwa nikuombe kwa dhati kabisa yatumie maoni ya wanajf kupima kama ulichokifanya au unachotaka kufanya ni kizur au laa na kujua kama kimepokelewaje kwenye jamii ya watanzania.

Achana na tafiti za twaweza, wanakudanganya hao ili wapate vyeo kutoka kwako, na pia CCM na subordinates wako wengine hawawezi kukukosoa sababu wanaogopa utawatumbua na CCM watakusifia katika kila jambo sababu wanataka uwape vyeo.

Lakini hapa hapa Jamiiforum waziri mkuu, mama Samia, na subordinates wako wengine wanaweza wakaja na ID tofauti wakakupinga katika jambo ulilolifanya lakini ana kwa ana hawawezi sababu wanaogopa utawatumbua baaba na wao wanataka kaugali ka watoto.

Njoo Jamiiforum chukulia watu walioko humu kama sample yako ya kufanya utafiti sababu wanakuja na fake ID kwahiyo wanaweza kutoa mawazo kwa uhuru.

Mwisho nikuombe utuachie kauhuru humu jf sasa mikutano umezuia baba tuachie basi jf yetu tutoe mawazo kwa uhuru, tunaomba mwanzilishi wetu Mexence Melo asibughuziwe tena.
Wazo bovu sana, yaani awasikilize chadema na negatives zao?? Maana ndo wamejaa humu, navicha hawakosoi isipokuwa wako NEGATIVE, hawana hopes. Ningeshauri asiingie kabisa jf.
 
Wazo bovu sana, yaani awasikilize chadema na negatives zao?? Maana ndo wamejaa humu, navicha hawakosoi isipokuwa wako NEGATIVE, hawana hopes. Ningeshauri asiingie kabisa jf.
Unaweza ukasema ni CHADEMA ila hata wewe barafu ya moto unayo ID yako nyingine, akizingua unakuja unamtukana kisawasawa, kwani uongo?
 
Mheshimiwa nikuombe kwa dhati kabisa yatumie maoni ya wanajf kupima kama ulichokifanya au unachotaka kufanya ni kizur au laa na kujua kama kimepokelewaje kwenye jamii ya watanzania.

Achana na tafiti za twaweza, wanakudanganya hao ili wapate vyeo kutoka kwako, na pia CCM na subordinates wako wengine hawawezi kukukosoa sababu wanaogopa utawatumbua na CCM watakusifia katika kila jambo sababu wanataka uwape vyeo.

Lakini hapa hapa Jamiiforum waziri mkuu, mama Samia, na subordinates wako wengine wanaweza wakaja na ID tofauti wakakupinga katika jambo ulilolifanya lakini ana kwa ana hawawezi sababu wanaogopa utawatumbua baaba na wao wanataka kaugali ka watoto.

Njoo Jamiiforum chukulia watu walioko humu kama sample yako ya kufanya utafiti sababu wanakuja na fake ID kwahiyo wanaweza kutoa mawazo kwa uhuru.

Mwisho nikuombe utuachie kauhuru humu jf sasa mikutano umezuia baba tuachie basi jf yetu tutoe mawazo kwa uhuru, tunaomba mwanzilishi wetu Mexence Melo asibughuziwe tena.
Upo sawa mkuu upo sawa kabisa
 
Majuzi TANESCO ilipotaka kupandisha bei za umeme,hisia za Watanzania zilipitia hapa JF,sote tunafahamu kilichotokea.So ni kweli Rais anaweza kuwa anapita hapa kufanya "Random Sampling".Good idea
 
Hapa wamejaa wanafiki tupu wa ufipa, kazi yao kupinga kila kitu (Wanapinga kushuka bei ya umeme, wanapinga elimu bure, wanapinga kununuliwa kwa ndege, wanapinga kupanda bei ya korosho na pamba) na kutetea mafisadi
.
wakiwa ufipa wanakosa sifa ya kuwa wananchi?
JF wamejaa walioenda shule walau kidogo,woga wa ccm unaanzia pale wanapojua mtu kaelimika!
 
Back
Top Bottom