Mh.RAIS MAGUFULI HEBU KEMEA VITENDO VYA WANANCHI KUVAMIA MAENEO YANAYOMILIKIWA KISHERIA

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Nimeshtusha Na kasi ya wananchi ya kuvamia maeneo ya watu wanayoyamiliki kisheria.Mh.Sumaye anamiliki Shamba eneo la Mabwepande Kwa Hati iliyotolewa Na Serikali.Wananchi wanalivamia Shamba hilo huku viongozi wa mtaa wa mji mpya Na diwani wanaubariki uvamizi huo Kwa kuwa nao wamekatiwa maeneo Na hao wavamizi.Viongozi wa serikali wa kata Na mtaa wanawafahamu Kwa majina wavamizi hao lakini hawataki kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola.Mh.Rais mgogoro wa uvamizi Shamba la Mh.Sumaye serikali yako inaujua kupitia Mkuu wa wilaya Kinondoni ambaye sasa in MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Makonda.Bw. Makonda badala ya kuwatoa wavamizi kwenye maeneo ya wamiliki kisheria amekuwa anawahakiki wavamizi.Mh.Magufuli wavamizi hawa wasipochukuliwa hatua za kisheria ili kukomesha uhalifu huu unakuwa Kwa kasi huenda yakatokea mauaji makubwa ya kutisha kati ya wavamizi Na wenye maeneo.Mh.Magufuli nchi yako INA Sheria tunaomba utuokoe sisi wenye maeneo Yetu tunaoyamiliki kihalali Na pia viongozi wa mitaa Na Diwani wa mabwepande ndio chanzo za uvamizi kwani maeneo yanayovamiwa hata wao wanapewa.Sheria ichukue mkondo wake.
 
Back
Top Bottom