Mh Rais, hili la machinga kuzagaa katika miji mbalimbali halitaifikisha nchi mbali kiuchumi

heavyload

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
919
525
Hili swala la machinga kuzagaa kila penye upenyo katika miji mbalimbali halitaifikisha nchi hii mbali kiuchumi.

Tuchukue mfano wa nchi kama Rwanda ambayo umekuwa na utaratibu mzuri wa kuwatengea machinga wao mahali maalum kufanya shughuli zao.

Hata hivyo kitaalam utaratibu huu utachangia kushuka kwa makusanyo ya kodi na ushuru mbalimbali na hivyo kupelekea kudorora hata kwa ustawi wa maisha ya watu katika nyanja zote.
 
Tatizo serikali maeneo inayoyatenga si rafiki kwa biashara za machinga kwa mfano, machinga complx ya Karume, serikali inachotakiwa ni kuendeleza maeneo yenye tija c kuwapeleka sehem Zisizo na mzunguko watarud tu sehemu zao hata ukiwaondoa kwa Mabomu.
 
Hizo bidhaa wauzazo hadi kuwafikia machinga huwa zimepitia mlolongo wa kodi mbalimbali zaidi ya moja,bidhaa au material ikipita bandarini inalipiwa kodi,ikifika dukani kodi,ikiingia na kutoka kiwandani ,pia wanapokuwa na kipato wanakuwa na uwezo wa kulipa kodi( indirect tax).
 
Hizo bidhaa wauzazo hadi kuwafikia machinga huwa zimepitia mlolongo wa kodi mbalimbali zaidi ya moja,bidhaa au material ikipita bandarini inalipiwa kodi,ikifika dukani kodi,ikiingia na kutoka kiwandani ,pia wanapokuwa na kipato wanakuwa na uwezo wa kulipa kodi( indirect tax).
Mkuu wewe inaonekana ni machinga ila wenye maduka wanaelewa namaanisha nini hapo
 
Mfano; kwa Dsm, Kama serikali kwa utafiti inaona Kariakoo ndio eneo la Machinga wanapendelea zaidi; Iingie gharama kufunga vimtaa fulani pale, then Machinga waende hapo, waache main road ipitike vizuri...pia madukani kule kuwe wazi waachiwe wenye maduka ili wateja wawe huru kutembelea maduka kwa maduka bila bughuza za wamachinga..maaana wengine wao sio machinga wa kweli...wezi na vibaka tu....Pale ubungo litafutwe eneo pia karibu na pale wapajenge pawe wazi sio jengo kama la machinga...wawe huru kumwaga bidhaa zao na kuondoka nazo...ili waache kutundika nguo na kumwaga katika njia za pembeni na hivyo wapita njia na magari kupata tabu...pia kuharibu sura ya mji...
 
Back
Top Bottom