Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,707
- 1,729
Jana kupitia radio yake iitwayo Voice of Tabora mheshimiwa Ismail Aden Rage, mbunge wa Tabora mjini, alikuwa 'live' akiwahutubia wapiga kura wake mjini hapo. Nilimsikia akitoa pikipiki na pesa. Kilichonishangaza ni muda wa mkutano kuendelea mpaka saa moja kasorobo jioni na kumsikia mmoja kati ya wazungumzaji akilalamikia uhaba wa ulinzi (polisi) katika mkutano huo. Wana JF hebu tujadili mambo haya mawili:-
1. Nijuavyo mikutano yote mwisho saa kumi na mbili jioni, au ni ile ya uchaguzi pekee?
2. Kwa nini pawe na ulinzi hafifu wakati mikutano ya vyama mbadala ulinzi huwa mkubwa zaidi?
1. Nijuavyo mikutano yote mwisho saa kumi na mbili jioni, au ni ile ya uchaguzi pekee?
2. Kwa nini pawe na ulinzi hafifu wakati mikutano ya vyama mbadala ulinzi huwa mkubwa zaidi?