Mh. Pinda waite CHADEMA Mkae Mzungumze

Mh. Pinda waite CHADEMA Mkae Mzungumze

Bubu Msemaovyo

Platinum Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,552
Haja ya mja hunena Muungwana ni Kitendo; wahenga walinena, sioni kama itaingia akilini kama hali hii tayari imejitokeza. Ukipata nafasi waite CHADEMA huko utapata kuwakanya kwa nguvu zote ikiwa utaona hawana sababu ya msingi. Hali hii haileti picha nzuri hata kidogo na kwa bahati mbaya wewe kama Mkuu wa Serikali macho yetu yote millioni 90 yanakuangalia wewe.

Nataka nihakikishe kuwa nimechangia mawazo mazuri kabla hujasema "Liwalo na Liwe" kauli ambayo itaashiriwa wote tuko katika vilabu vya pombe tunagombana ambapo neno hilo "Liwalo na Liwe" ni la kawaida sana.

Hakika si busara kumkanya mtoto kupitia vyombo vya habari!!!!! Waite CHADEMA kaa nao wasikilize kwa makini lazima kuna jambo limejificha katika uhasama huu wa Polisi V/S CHADEMA, siyo bure. Asante sana Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mtoto wa Mkulima kutoka Katavi.

Tata etu Kalesa!!
 
Nimjuavyo Kayanza Mizengo Pinda ni mtu wa TISS awamu tofauti tofauti.

Nina maana haoni busara nje ya kusimamia utawala ulioko madarakani bila kujali wameingiaje madarakani na wanafanya nini wakiwa kwenye mnadaraka.

TISS hawafany kitu cho chote bila idhini ya Waziri Mkuu na Rais; nina maana wanajua kinachoendelea kuliko unavyofikiria

Nimjuavyo Kayanza Mizengo Pinda ni mtu wa TISS awamu tofauti tofauti.

Ni mgeni sana katika siasa za kistaarabu na za kidemokrasia. Nina maana hata ukimchoma sikio hasikii wala haelewi kitu kiachoitwa kushindwa kwa hoja inayoamriwa na kura halali ndani ya sanduku la kura.

Nimjuavyo Kayanza Mizengo Pinda ni mtu wa TISS awamu tofauti tofauti.

Anaongoza Serikali na Bunge ambazo zimejijengea uhalali wa kutawala kwa utaratibu wa LIWALO NA LIWE. Nina maana bila kujali nchi na wananchi kwa vitendo. Yaani wanachokisema sicho wanachokitenda, na wanachokitenda sicho wanacho kisema.

Nimjuavyo Kayanza Mizengo Pinda ni mtu wa TISS awamu tofauti tofauti.

Anatoka familia ya kimaskini kwa maana ya viwango vya kumiliki mali na fursa za mali ambazo zimebadirishwa na Uwaziri Mkuu. Nina maana hawazi kutema zali la kitumbua hicho kwa kusimamia hoja mbadala zaidi ya ya utawala.

KWA BAADHI YA SABABU HIZO MUONEE HURUMA TU HUYO PINDA KWA SABABU

1. Ni muongo mzoefu si wakujadiliana naye kitu cho chote

2. Nina wasiwasi na upeo wa uelewa wake, ni vigumu kukaa meza moja na mtu wa namna hii kwa sababu hataheshimu matokeo ya kikao cho chote.

3. Ni kiongozi wa Serikali na Bunge lililoshindwa kwa udhaifu wa utawala, sasa kwa nini apewe promo asiyoistahili

Kuna fursa za busara na hekima kwa uongozi wo wote; inapofikia ni matumizi ya mabavu, kejeli kwa kutanguliza na kujilinda na vyombo vya dola ni afadhali kutumia njia mbdala. Kujihami au kupambana na mwenye haki daima itaibuka mshindi. Mwenye haki ni yule anayesimamia maadili maudhui na uwajibikaji kwa wananchi na nchi. SI PINDA AU YE YOTE NDANI YA CCM NA VYOMBO VYA DOLA.
 
kama kiongozi mwenye hekima na busara ndo angetakiwa kuonge na si kusema piga hao
 
Mimi sidhani hali ilipofikia kuna haja ya kuongea na Pinda au na JK, kunahitaji msuluhishi wa kimataifa. Viongozi wa Tanzania wananuka damu
 
Wala hawezi hata kukuelewa , maana leo ameruhusu polisi kupiga raia ( bila shaka ameruhusu kuua pia ) , madaraka yanapofusha Mkuu , hawa hawaamini kama kuna Kiama , Suluhisho la haya yote ni pale tu CCM itakapokubali kushindwa ARUSHA , Hakuna muafaka wa namna ingine yoyote , Askari wanahesabika ,bunduki zinahesabika hata risasi zina idadi , lakini huwezi kuhesabu fikra au nguvu ya ukombozi ! Hakuna na haitapata kutokea POPOTE PALE Dhuluma kuishinda Haki , hata akitamka mara mia moja ile kauli yake ya LIWALO NA LIWE !
 
He has little time left...miaka mi2 tu......Walikuja na wataondoka hata kama watatuua na kututuesa, HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA
 
Mkuu mleta mada umesema kitu cha maana sana. Muda wakeutafika tu wa kuondoka. Wameondoka wengi sana hivi sasa wanalilia kurudi llakini ni ngumu. Huyu Mzee Pinda kwa kweli sometimes anakurupuka sana kuongea.
 
Haja ya mja hunena Muungwana ni Kitendo; wahenga walinena, sioni kama itaingia akilini kama hali hii tayari imejitokeza. Ukipata nafasi waite CHADEMA huko utapata kuwakanya kwa nguvu zote ikiwa utaona hawana sababu ya msingi. Hali hii haileti picha nzuri hata kidogo na kwa bahati mbaya wewe kama Mkuu wa Serikali macho yetu yote millioni 90 yanakuangalia wewe.

Nataka nihakikishe kuwa nimechangia mawazo mazuri kabla hujasema "Liwalo na Liwe" kauli ambayo itaashiriwa wote tuko katika vilabu vya pombe tunagombana ambapo neno hilo "Liwalo na Liwe" ni la kawaida sana.

Hakika si busara kumkanya mtoto kupitia vyombo vya habari!!!!! Waite CHADEMA kaa nao wasikilize kwa makini lazima kuna jambo limejificha katika uhasama huu wa Polisi V/S CHADEMA, siyo bure. Asante sana Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mtoto wa Mkulima kutoka Katavi.

Tata etu Kalesa!!

Sidhani kama kuna cha kongea au kushauriana CDM; everything is black and white, Kila kitu kiko wazi na kinaeleweka kuwa mambo yote yanayotokea yanapangwa na yanaratibiwa na yeye akiwa anajua. kwa mfuatiliaji ya hali ya siasa yetu nchini nadhani hata mtoto wa miaka mitano ataelewa kitu gani kinaendelea.
Kuna baadhi ya kauli hazileti maana kabisa kuzungumzwa na viongozi wa serikali.
 
kama kiongozi mwenye hekima na busara ndo angetakiwa kuonge na si kusema piga hao

Anazidi kudhihirish upumbavu wake kwani sikutegemea mtu kama yeye kuwa majibu ya ovyo ovyo kama hivyo nilitegemea toka kwa mwingulu na wajinga wengine ila nae kashajiweka ktk kundi moja na hawa wapumbavu
 
Mimi sidhani hali ilipofikia kuna haja ya kuongea na Pinda au na JK, kunahitaji msuluhishi wa kimataifa. Viongozi wa Tanzania wananuka damu

Na ni wengi wa maslahi ya chama kuliko ya Taifa
 
Pinda aliwahi kutoa tamko kuhusu wale wanaokamatwa na viungo vya albino kuwa akikamatwa mtu akiwa na kiungo cha albino naye auawe, wanaharakati walimjia juu akarekebisha kwa kusema "Hakuna chochote tutakachofanya nje ya sheria" clip ya maneno haya iko katika kibwagizo cha "Yaliyotokea" kinachorushwa na WAPO RADIO na Patapata cha radio hiyo. Kauli hii aliikanusha baada ya kuona ametamka kitu ambacho kingeweza kuleta athari na mauaji mengi kwa kisingizio cha "tumemkuta akiwa na kiungo cha albino"

Kiongozi mwandamizi wa serikali kama Pinda ajue hata akicheka kicheko mbele ya msiba ni hotuba tayari kwa jamii. Maneno atamkayo huwa ni "DECREE" kwa njia moja au nyingine. Mizengo Pinda ukiwa na hasira bora utoe machozi kuliko kutamka kauli za kuhatarisha maisha ya sisi Watanzania.
 
serikali ya tanzania iliyokuwa na uhalali wa kuwaambia majirani zake wakae wazungumze na wapinzani ni zamani.....
Weewe unamwambia kagame azungumze na wapinzani,,...wakati hapa nyumbani mnashindwa kukaa kuzungumza na watu wa mtwara .....mnashindwa kuzungumza na chadema ....mnapata wapi moral authority kuwaambia wengine?

Pinda ni waziri mkuu mzembe ...,mjinga...na poweless kuliko wote waliopata kutokea ...mnafiki namba moja....mla rushwa wa bei nafuuu........

Watu wa arusha akiwaletea ujinga watamuumbua ...wanazo siri zake ........corrupt anahongwa hadi suti ....atawaambia nini watu huyu kilaza!!!!! Failure..
 
Pinda asichofikilia mbele, chama kikianguka kila mtu anabeba mzigo wake, leo hii anafanya haya kuwafurahisha mabwana zake, siku hiyo atasimama kizimbani peke yake kutetea damu alizo shiriki kumwaga. hapo ndiyo jasho litakuwa likmtamba mgongoni likimshuka mpaka chini kufuata uti wa mgongo.
Picha ya yule mtoto mdogo wa kike aliye pigwa bomu bado hainitoki akilini, hawa jamaa na walaaniwe tu.
 
mimi nasema chadema wasikosee ...wawapeleke hawa the hague haraka sana sana...ushahidi wa leo wa uvunjaji wa katiba na agizo la serikali kupiga kupiga !!!! Uunganishwe kwenye kesi ya the hague....
Leo nimechukia sana ....namna pinda alivyojibu maswali irresponsibly

VIONGOZI WETU WA JUU WANAHITAJI IMPECHMENT .......KABISA....NADHANI WANAUGUA MAGONJWA AMBAYO SASA YAMEFIKIA HATUA YA KULA UBONGO
 
JK ni mwepesi kutoa ushauri kwa Kagame kuhusu yanayoendelea nchini Rwanda lakini anashindwa kukifanya kile ambacho kinafanana na alichomshauri Kagame kufanya.....Only GENIUS CAN DO THAT.
Kitaeleweka tu.
 
Haja ya mja hunena Muungwana ni Kitendo; wahenga walinena, sioni kama itaingia akilini kama hali hii tayari imejitokeza. Ukipata nafasi waite CHADEMA huko utapata kuwakanya kwa nguvu zote ikiwa utaona hawana sababu ya msingi. Hali hii haileti picha nzuri hata kidogo na kwa bahati mbaya wewe kama Mkuu wa Serikali macho yetu yote millioni 90 yanakuangalia wewe.

Nataka nihakikishe kuwa nimechangia mawazo mazuri kabla hujasema "Liwalo na Liwe" kauli ambayo itaashiriwa wote tuko katika vilabu vya pombe tunagombana ambapo neno hilo "Liwalo na Liwe" ni la kawaida sana.

Hakika si busara kumkanya mtoto kupitia vyombo vya habari!!!!! Waite CHADEMA kaa nao wasikilize kwa makini lazima kuna jambo limejificha katika uhasama huu wa Polisi V/S CHADEMA, siyo bure. Asante sana Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mtoto wa Mkulima kutoka Katavi.

Tata etu Kalesa!!

2015 kuna kazi ya kufanya uchaguzi sahihi.
 
Ni wanafiki wa hali ya juu kutaka kujionyesha katika jumuiya ya Mataifa kwamba wanapenda mazungumzo ili kupunguza au kuondoa migogoro katika nchi mbali mbali za Afrika wakati hapa nchini wanafanya tofauti na mahubiri yao.

Back
Top Bottom