Mh. Pinda atetea mbio za mwenge

TinkerTailor

Member
Apr 5, 2014
15
0
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ametetea umuhimu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, akisema ni jambo kubwa lenye manufaa ambalo moja ya faida zake ni kuhimiza umuhimu wa kujitolea miongoni mwa wananchi katika kujiletea maendeleo yao.

Aidha, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amesema mbio za Mwenge zinaeneza ujumbe wenye manufaa kwa jamii, kuliko mikutano inayofanywa na kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Waziri Mkuu Pinda alishan- gazwa na mjadala ulioibuliwa na wabunge wa upinzani bungeni jana kuona Mwenge kama suala lisilo na maana kwa taifa.

"Nimesimama kwa sababu nimesikiliza mjadala hapa, naona jambo hili kubwa, linaonekana kama halina maana kwa taifa," alisema Pinda na kuongeza:"Kila mwaka, mbio za Mwenge huwa na kaulimbiu mahsusi kwa sababu Mwenge huu huwa na fursa ya ku- fika maeneo mengi hivyo kufikisha ujumbe kuhusu masuala mazito ya nchi kama elimu. Kwa hiyo, si sahihi kabisa kuona Mwenge hauna maana."

Alisema anafahamu kuwa wap- inzani wanaweza wasipendezwe sana na Mwenge kuhimiza suala la kujitolea miongoni mwa wananchi.

"Hili linaweza lisiwapendeze sana wenzetu wa upande wa pili. Mwenge unahimiza suala la kujitolea katika shughuli zao za maendeleo.

"Wananchi wanahimizwa kuenzi moyo huo na wamekuwa wakifanya hivyo katika shughuli mbalimbali za kijamii. Hili halina ukakasi hata kidogo.

"Hoja hapa imekuwa ni michango, lakini hivi Mwenge unakuja pale kwangu Kibaoni, kwa ugeni huo, unaofanya kazi nzuri, kama watu wanachanga kuku, bata, hii siyo dhambi. Wananchi wamekuwa wakarimu sana katika jambo hili," alisema Waziri Mkuu Pinda.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema), alitaka kufahamu ni kiasi gani cha fedha hutumika kwa kila wilaya kwa ajili ya mbio za Mwenge, gharama za kuuwasha na kuuzima na faida zinazopatikana.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Nkamia alisema Serikali hutenga fedha kulingana na mahitaji ya gharama halisi ya wakati husika.

Alitoa mfano wa mwaka 2012, Sh milioni 650 zilitengwa kwa ajili ya kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru; ambazo kati ya hizo, Sh milioni 450 zilitumika na Wizara na Sh milioni 200 zilitumika na mkoa mwenyeji wa kilele cha mbio hizo.

Kuhusu faida, alitaja kuwa ni kuendelea kutunza historia na falsafa ya ukombozi wa taifa, kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuendelea kuenzi amani, mshikamano, upendo na zaidi kupambana na aina yoyote ile ya kuwabagua Watanzania kwa rangi, dini au makabila yao.

Pia kuendelea kuhamasisha kushiriki katika shughuli za uzal- ishaji mali na kujiletea maendeleo. Hata hivyo katika maswali ya nyongeza, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), alisema Mwenge unaongeza ugumu wa maisha kwa kuchangisha wananchi na kuwa viongozi wa mbio hizo mwaka huu wanapita kupiga propaganda ya serikali mbili na kutaka mbio hizo zifutwe.

Akijibu swali hilo, Nkamia alisisitiza kuwa Serikali haiko tayari kusitisha mbio hizo, kwani wananchi wana imani nazo na zimesaidia kudumisha umoja na amani.

Alisema Mwenge unatoa ujumbe mzuri kuliko unaotolewa na Ukawa. Mbali ya Mnyika, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), alihoji sababu za walimu kulazimishwa kuchangia mbio hizo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Uratibu na Bunge, Wil- liam Lukuvi alisema michango hiyo ni hiari na hakuna anayelazimish- wa kuchangia, na kwamba hailipii mafuta ya Mwenge wala posho za wakimbizaji.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM), yeye aliitaka Wizara ion- geze siku za kukimbizwa Mwenge wilayani Kishapu kwani una manu- faa makubwa, na Wizara imeahidi kulifanyia kazi ombi hilo huku ikipongeza hatua hiyo.

Baada ya hapo, Waziri Mkuu alitoa ufafanuzi zaidi, lakini baada ya Kipindi cha Maswali na Majibu, wabunge wa upinzani walisi- mama tena na kuomba Mwongozo kuhusu majibu hayo ya mawaziri.

Waliosimama ni Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (Chadema), Moses Machali (NCCR- Mageuzi – Kasulu Mjini) na Susan Kiwanga (Viti Maalumu – Chade- ma), wote wakieleza kuwa wananchi wanachangishwa, na baadhi yao kusoma ujumbe waliotumiwa katika simu zao za mkononi. Naibu Spika Ndugai alisema atatoa majibu ya miongozo hiyo ‘mbele ya safari.

Source: HabariLeo


BILIONI 158.8 / KWAAJILI YA MBIO ZA MWENGE!!??
2011/ 2012 BAJETI YA WIZARA YA ELIMU, BILIONI 632.
KWANINI TUSICHUKUE HIZO BILIONI 158 TUKAZIWEKA KWENYE ELIMU!

UNAHAMASISHA VILAZA WA DIVISION 0 NA WATOTO AMBAO WANAMALIZA DARASA LA SABA HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA ILI WAFANYE NINI!!!???
 

A-town

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
495
225
Pinda atetea mbio za mwenge
28/05/2014

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, jana alitetea mbio za mwenge wa uhuru kwa kusema zinahamasisha jamii ione umuhimu wa kujitolea katika shughuli za maendeleo.

Pinda alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), aliyetaka kufutwa kwa michango ya mwenge kwa kuwa hupangiwa bajeti yake na serikali.

Pia Mnyika aliitaka serikali kupiga marufuku tabia ya wakimbiza mwenge kitaifa kutumia mbio hizo kuhamasisha muundo wa serikali mbili, jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya mbio hizo.

Akiendelea kujibu swali hilo, Pinda alisema mwenge unapokimbizwa nchi nzima husaidia kuelimisha masuala mazito ya nchi, hivyo wananchi wanapaswa kuunga mkono mbio hizo.

“Kila mwaka mwenge unapokimbizwa nchini huwa kuna kaulimbiu yake, hizi kaulimbiu ni kwa sababu mwenge ule unapita katika maeneo mengi nchini, hivyo tunatumia muda ule kuelimisha masuala mazito ya nchi.

“Hili linaweza lisiwapendeze wenzetu wa upinzani, lakini kupitia mwenge huu tunahamasisha jamii waone umuhimu wa kujitolea katika shughuli za maendeleo mbalimbali,” alisema Pinda.

Alisema ndiyo maana kila mwenge unapokimbizwa hutaja miradi itakayozinduliwa na gharama zake, ili kuhamisha moyo wa Watanzania kuenzi shughuli za kujitolea.

“Hofu ya wabunge wa upinzani ni michango. Michango hii ni hiari na siyo lazima, wananchi wenyewe wamekuwa wakijitolea sana hususan katika eneo ambalo mwenge unalala,” alisema Pinda.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, alisema serikali haina mpango wa kupiga marufuku michango ya mwenge.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (CHADEMA), alitaka kujua kiasi cha fedha kinachotumika kwa kila wilaya kwa kukimbiza mwenge.

Pia mbunge huyo alitaka kujua gharama zinazotumika katika kuuwasha na kuuzima na faida zinazopatikana kutokana na mbio za mwenge huo.

Nkamia alitoa mfano kwa mwaka 2012 kwamba jumla ya sh bilioni 158.8 zilitumika kuuwasha na kuuzima.

“Mwenge wa uhuru unaendelea kutunza historia na falsafa ya ukombozi wa taifa la Tanzania na kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuendelea kuenzi amani, mshikamano, upendo na zaidi kupambana na aina yoyote ile ya kuwabagua watanzania kwa rangi, dini ama makabila yao,” alisema Nkamia.


BILIONI 158.8 / KWAAJILI YA MBIO ZA MWENGE!!??
2011/ 2012 BAJETI YA WIZARA YA ELIMU, BILIONI 632.
KWANINI TUSICHUKUE HIZO BILIONI 158 TUKAZIWEKA KWENYE ELIMU!

UNAHAMASISHA VILAZA WA DIVISION 0 NA WATOTO AMBAO WANAMALIZA DARASA LA SABA HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA ILI WAFANYE NINI!!!???

Kati ya vitu tumekosa kama taifa ni viongozi wenye upeo mambo na kupanga vipaumbele vyenye tija na siku tukiwapata tutaishi kwenye neema kubwa:israel:
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,414
2,000
Ujamaa ni umasikini.
Tunafanya vitu visivyokuwa na mantiki wala tija kwa taifa. Mfano hai ni hizi mbio za mwenge.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,299
2,000
Aidha, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amesema mbio za Mwenge zinaeneza ujumbe wenye manufaa kwa jamii, kuliko mikutano inayofanywa na kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Aisee.......
 

samvande2002

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
414
195
Ujamaa ni umasikini.
Tunafanya vitu visivyokuwa na mantiki wala tija kwa taifa. Mfano hai ni hizi mbio za mwenge.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk


ni aibu kwa taifa; yani tunazichoma kodi za wananchi moto kupitia mbio za mwenge? aibu; au kuna cha juu??..
 

Usoka.one

JF-Expert Member
Nov 20, 2013
773
250
Tunafanya mambo kwa mazoea, ni kero aisee

Mwenge ni uchawi na kule ndani kuna kijiti toka kwa mungu wa kizanaki.Kuna mtumishi aliombea watu ambao wamewahi kushika mwenge zililipuka pepo balaa huku zikiwapindisha wahusika mikono.Chezea uchawi wa chama kubwa wewe!!
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,414
2,000
Mwenge ni uchawi na kule ndani kuna kijiti toka kwa mungu wa kizanaki.Kuna mtumishi aliombea watu ambao wamewahi kushika mwenge zililipuka pepo balaa huku zikiwapindisha wahusika mikono.Chezea uchawi wa chama kubwa wewe!!

Ulishawahi kukiona hiko kijiti??
 

mzeelapa

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
1,077
1,500
Wanauliza mwenge wa Uhuru wa Tanzania mbona hawaulizi mwenge wa Olimpiki? Mbona hawaulizi kifimbo cha malkia, mbona hawaulizi kombe la dunia? Vyote hivi vinazunguka dunia nzima na wapinzani hawalisemei?
Ndege wote waimbe, akiimba bundi ooh uchuro...!!!
 

aloycious

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
5,823
2,000
Mwenge ni upuuzi. Ni miongoni mwa ya kijinga tuliyorithi toka kwa Mwalimu. Uwekwe makumbusho pale basi.
 

samvande2002

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
414
195
Wanauliza mwenge wa Uhuru wa Tanzania mbona hawaulizi mwenge wa Olimpiki? Mbona hawaulizi kifimbo cha malkia, mbona hawaulizi kombe la dunia? Vyote hivi vinazunguka dunia nzima na wapinzani hawalisemei?
Ndege wote waimbe, akiimba bundi ooh uchuro...!!!

kifimbo cha malkia kinakula PAYE yako??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom