Walijifanya kutoa ahadi kwamba wataianzisha wakadhani Tz ya leo ni ile ya nyuma sasa linawatokea puani, walizoea tutajenga madaraja, tutajenga lami alafu wasipojenga kinachofuata ni kuwaambia wananchi maneno ya kupendeza kwamba "upembuzi yakinifu umefanyika na mpaka sasa wataalamu wanahangaika kuangalia namna ya kuboresha ili barabara ijengwe pana zaidi hivyo tutatekeleza katika awamu ijayo"-wanapigiwa makofi, lakini hili la kazi issue imekuwa nzito namna ya kuliundia maneno imekuwa ngumu kidogoHii ni rahisi sana kutatua kuliko lolote
Ningesimamia msimamo wa katiba
serikali haina Dini na kila dini ishughulikie mambo yake ya ibada kwa mujibu wa taratibu za kanisa au msikiti.
Ni rahisi kiasi hicho. Pinda, kikwete na ccm yao inawawia vigum kwasababu wanafanya nje ya jatiba na hivyo kuonekana wanavuruga Taifa kwa kuvunja katiba hadharani.
Kiongozi yeyote asiyeweza kuilinda, kuisimamia na kuitetea katiba yetu, huyo hatufai. Pinda hafai hata kuwa mwenyekiti a kijii kwa sababu haheshimu haki za binadamu, hajali katiba ya nchi, wala nia ya kujenga taifa imara lenye mshikamano na amani hana.
Amejidhihirisha ni namna gnai anaweza ktumiwa na itikadi yoyote kusaliti nchi na watu wake halafu asijitambue kwamba ana haribu.
Aliamuru majeshi yapige raia wasio na silaha wakitafuta haki zao kikatiba kwa mba amechoka. Leo nguvu ya kuliingiza taifa kwenye mapigano ya kidini amezitoa wapi?
Alisema eti Waziri asipokuwa mbunge hataweza kuwatumikia vizuri wananchi kwa sababu hatajua hali na mahitaji yyao sahihi ikatoa namna gnai kichwa chake kilishaacha kufikri na bila shaka anapoteza kumbukumbu zake haraka.
Amekusanya kusanya viongozi kadhaa wa dini kulazimisha maridhiano ya kadhi, pamoja na kukataa kwao akaibuka na taariga kwamba wameafiki. Hii ni tabia ya udanganyifu na ulaghai inayoangamiza taifa kwa kufanya maamuzi yasiyo sahihi yanayojengwa kwenye taarifa za kupikwa.
Ameendelea kuishauri serikali itumie ubabe katika masuala yote yenye utata kuazia kura za mitaa, BMk, unandikshwaji wa wapiga kura, kura za maoni na miswada mbali mbali inayoelekea kutusababishia shida hata kabla ya uchaguzi mkuu.
Huyu anatahili kupumzika kwa sababu amechoka. Bila hivyo, tutegemee majanga makubwa kama hli la kadhi kwenye katiba, unless watu watumienguvu kubwa kudhibiti nyendo zake.
LAKINI URAISI ASAHAU, INGAWA ANATAKIWA KUAGALIWA KWA UKARIBU SANA KWA KIPINDI HIKI CHA LALA SALAMA KWA SABBU NINAONA WAMEJIZATITI KUMALIZIA HUJUMA WALIZOZIANZA KWA TAIFA YEYE NA MKUU WAKE.
SAFARI ZA ARABUNI NINAOMBA NGUVU YA MUNGU IMFUNGIE KUANZIA SASA HADI ATAKAPOACHA UONGOZI.
KUNA WAKATI MWINGINGE Mh.Pinda huwa anapinda,hakika ktk hili alipinda na iwe funzo kwa watu wa aina yake
Hakuna waziri mkuu atayekuja kuwa rais wa Tanzania.
Tatizo la baadhi ya watanzania hupima urais kwa kigezo kimoja tena kigezo dhaifu kama mahakama ya kadhi. Hata waisilam sio wote wanashadadia mahakama ya Kadhi sembuse wakristo au hata wapagani? Suala sio kusema Pinda anaipenda hoja ya Mahakama ya Kadhi hoja ni namna gani ameishughulikia? Hata kama haijakubalika yeye binafsi kama kiongozi amelishughulikiaje.Hawezi kuacha kulishughulikia kwa sababu tu yeye sio Mwisilamu, la hasha! Yeye siyo kiongozi wa kidini ni kiongozi wa kisiasa. Kiongozi hufanyi jambo lile unalolipenda tu hata usilolipenda lakini kuna wananchi ambao wewe ni kiongozi wao wana jambo wanalolipenda wewe unawasaidiaje kufikia malengo yao. Uraisi ni mambo mengi yanayoshikana kwa pamoja (complex) Kumkataa mtu kwa sababu ya jambo moja tu Mahakama ya Kadhi na huwezi kumkubali mtu kwa sababu ya Mahakama ya Kadhi tu, tumwangalie mtu in his totallity. Kama vile watu kumjudge mtu kwa jinsi anavyotoa rushwa kwenye vikundi vya dini au kijamii. Hapana uraisi ni mchanganyiko wa sifa nyingi zikijumuishwa kwa pamoja.
Bantulile, tunaungana kuwafanyia thathmini pana viongozi wetu katika wingi na ukubwa wa mazuri na mabaya yao.
Kiongozi mtumia rushwa na fisadi, ameshajiengua wala hana nafasi ya kupimwa tena kwa uhudhriaji wake misibani, kutoa michango kwa makundi au propaganda. Kosa la ufisadi na rushwa linafunika wema na uzuri wowote wa kiongozi.
Kiongozi anayesaliti katiba, anasaliti uma. Hata angejaribu kujitabasamisha namna gani huyo hafai kuongoza umma kwa sababu hatasimamia maslahi ya umma.
Ninakubaliana na wewe kabisa kwamba kiongozi ni mdau wa masuala yote yanahusu jamii anayoiongoza na anapaswa kuyashughulikia. Tatizo linakuja namna gani anashughulikia? Kujaribu kuvuruga amani ya nchi kinyume na misingi ya katiba na utaifa eti unashughulikia tatizo la kundi moja? Unashughulikia tatizo la kundi moja kwa gharama ya uhai wa taifa? Hapo ndipo sifa ya Pinda ilipoondoka na mahakama yake ya kadhi.
Hivi leo wafanyabiashara wanagoma kulipa kodi, halafu kiongozi anaanza kushirikiana nao kuboresha mgomo ili kodi walipe wafanyakazi peke yao. Ni sahihi? Kwamba kwa kuwa hawataki basi atafute lugha ya kuwashawishi wafanyakazi wakubali klipa kodi peke yao kuwaridhisha wafanya biashara waiogoma? Hapana ndugu. Huo si uongozi.
Migogor yote inatatuliwa kwa kurejea kwenye constitution. Hivi kulikuwa na haja gani Pinga kulazimisha hasi muswada wa kuvuanja sheria za nchi na kuvuruga amani? Hajui kama katiba inasemaje? Huyu Pinda na wenziye wa ccm (wanafiki wachache), wangekuwa wakweli, na wana uchungu na taifa, walishindwa nini kuwapa elimu ya uraia na katiba hao waliotka dini yao iwe ya seriakli? Kilichowafanya hadi waingize kwenye ilani ni nini kama si unafiki, na woga wa kuitetea katiba ya Jamhuri?
Hapo ndipo Pinda na ccm fisadi, wamethibitisha hawawezi ama kwa hiyari ama kwa mfumo wa chama chao, ama kwa kundi dogo lenye nia ovu na taifa, kuitetea na kuisimamia katiba na hivyo hatuhitaji tena kuwapima kwa vitu vingine ingawa hata hivo yak mengi sana waliyopwaya.
Kwa ufupi, Mahakama ya kaedhi alivyoishughulikiapinda, hafai kuwa kiongozi wa umma.
Lowasa kwa wizi, rushwa , ufisadi na uwongo uwongo wake wa kuhadaa, hafai kuwa kiongozi wa umma na hatuna sababu ya kuwaupima kwa namna nyingine kwa sababu makosa yana constitute major constitutional offences na actually wanastahili kushitakiwa.
Hatuhitaji watu wenye usafi wa kutafutiza kwenye nafasi zoe za uongozi.
Hope umenielewa kiongozi.
Pinda alifaa kuwa waziri mkuu wa mashambani au wakulima wa nyanya chungu
Kwa ujumla serikali ya awamu ya nne iliendekeza suala la udini sana.
Hata ajira za watu mhimu mf Mnikulu, Mawaziri, Usalama, RPCs, na washauri mhimu wa serikali ili lazimu kuwa Waislam. Bila siri hawa jamaa wengi hawajasoma!!
TCRA mnisamehe leo, naomba muanze tarehe 1 July, 2015. Ila ukweli kwa gharama yoyote ni lazima usemwe na ujulikane.
Unaposema waislam hawajasoma uweke na takwimu,
tuwekee idadi yao kiujumla,idad ya waliosoma na wasiosoma.
Na pia tupatie idadi ya wasio waislam kwa ujumla,na idad ya waliosoma na wasiosoma.Then tufanye analysis
Kusifia kama wakristo wamesoma,then kwenye kashfa za wizo serikalin wao ndo wengi ni ujuha.Haya Mtoto wa Mkulima kasoma mbona anavurunda?AG wa Mkapa,ma-AG QA JK WOTE WAKRISTO NA HAPA WANACHAMBWA KUWA NI EMPTY HEADS,ILA WAO HAMUWASEMI KWA DINI ZAO,AKINA S@ad@ mnawajadili kwa dini zao.Hapo hakuna u-great thinker mdau
Silaha ni moja tu nayo ni kuliaHoja ya mahakama ya kadhi tumeiona jinsi ilivyoibua hisia kali na hali ya sintofahamu ktk jamii.Ilipelekea Mh.Mtikila kuwahi mahakamani kuipinga isizungumzwe bungeni.
Maaskofu na watu wasio na maslahi na mahakama ya kadhi,waliipinga kwa hoja na hata kuionya serikali isithubutu kuinzisha mahakama hiyo.
Waziri mkuu na mwanasheria mkuu waliikomalia na kushawishi sana kuwa haina madhara endapo ikijadiliwa na hata kupelekea kuanzishwa kwa mahakama hiyo ya kadhi.Huenda ilikua janja ya nyani kula indi bichi ili kushawishi kundi linalodai mahakama hiyo na kupata kuungwa mkono kwa mambo fulani yanayotakwa na wapenda madaraka.
Sasa ni wazi kuwa mswada wa mahakama ya kadhi umetoswa baada ya kuona jinsi hali ya hewa ilivotaka kuchafuka huko bungeni na baadaye ingekua huku uswazi(MUNGU aepushie mbali)
Hivyo,endapo Mh.Pinda alitaka kuwafurahisha waislamu,sijui sasa atawaambia nini? Na huko kwa wakristo nako sijui atawaeleza nini? Atagombea urais kweli,au amejikaanga kwa mafuta yake mwenyewe?
Wanasiasa huwa hawana aibu,ngoja tumsubiri !