Kwa uchambuzi wangu inaonekana vijana walioko CCM wanaona mbali kuliko wazee wao na hii inaondoa status quo ya waasisi kiasi kwamba wazee wanaona vijana wanakosa adabu na kuaza kutumia mbinu chafu kuwanyamazisha.
CCM wako vijana ambao wameamua kutolalia godoro lenye chawa la CCM ya akina Kingunge na wameamua kuwa na mtazamo tofauti na hivyo kuonekana kuwa chukizo kwa wazee. Akina January Makamba, Filikunjombe, Lazaru Nyalandu, Selukamba na wengine wanaonekana kuwa na msimamo ambao utawakera sana CCM kiasi cha kutaka kuwapiga vita na kuzima nyota yao ya kisiasa.
Ninawashauri hawa vijana kuondoka na kujiunga na sisi tulioamua kuingia katika mapambano ya kidemokrasia kuikomboa nchi yetu. Milya amenza na wengine(Nyalandu, Januari Makamba, Filikunjombe, Selukamba) msipate kigugumizi karibuni tujenge upya taifa la kizalendo CCM iko kwenye steep downfall!!!!