Mh. Ngeleja nina wasiwasi na kauli yako.

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
635
Nimekuelewa mh. kwa kauli yako ya kuitaka EWURA kuwakamata wafanyabiashara ya mafuta waliogoma kuuza mafuta kuwanyang'anya leseni na kuwafikisha mahakamani kwa kuwa kitendo walichofanya ni kuhujumu nchi. Kwa juu juu kauli yako inaweza kuonena inamvuto na maslahi kwa wananchi. Binafsi mimi siiamini kabisa hii kauli yako, kwa kuwa hujatoa majibu ya maswali yanayoniumiza kichwa:
1. Kwanza mh. sijaelewa siku zote hizo ulikuwa wapi wanachi wanavyoendelea kupata tabu.
2. Pili, nilimsikia mkurugenzi wa EWURA akisema kwamba hakuna mgomo kwenye vituo vya mafuta ilhali anaona watu wanavyohangaika na vidumu barabarani, mh. hujasena utamchukulia hatua gani kiongozi huyu.
3. Mkuu hujasema wewe una mkakati gani wa kupambana na wafanya biashara hawa wakati unafahamu fika kwamba kwa sasa serikali haina ubavu wa kuwadhibiti wafanyabiashara. Mfano mzuri ni bei ya sukari na kauli ya rais & waziri mkuu.

4. Mheshimiwa, umeridhika na zigo mliowatupia watanzania walio wengi kutokana na kuwapadishia bei ya mafuta ya taa. Mh. unafahamu kabisa kwamba kitendo hiki ni hujuma kwa watanzania iliyotokana na udhaifu wenu kwa kushindwa kudhibiti uchakachuaji, ilhali unajua fika kwamba hilo ni jukumu lenu sio la wanachi wa kawaida. Leo nitakuamini vipi kama kweli unaguswa na adha anayopata mtanzania wa kawaida inayotokana na mabadiliko ya bei za mafuta?

Yapo mengi ya kusema mheshimiwa, ila kwa kuanzia tu ningependa kuona unatoa majibu ya hoja hizo ili japo raia wa kawaida tuamini tuamini kama kweli kauli yako imetoka rohoni kweli.
 
Hopeless ngeleja. Tupa kapuni huyo, mwache ale naye aondoke waje wengine
 
ngeleja tumemchoka siku nyingi mara ngapi anakuwa na kauli za ajabu ajab kuhusu umeme umesahau hata wanamagamba wenzie walishindwa kuvumilia uozo wake wakataa bajeti yake ilijaa madudu? Infact cjui anafanya nn
 
Back
Top Bottom