Mh. Nchambi mbunge wa CCM amdhalilisha Mh. Salome Makamba. Spika Ndugai hakuchukua hatua. Je, sababu ni mfumo dume, au chuki za itikadi za vyama?

Hii imetokea wakati wa mjadala kuhusu bajeti ya Wizara ya Madini.

Kulitokea kupishana hoja kati ya Mh. Suleiman Nchambi na Mh.Salome Makamba.

Hawa wote ni wabunge toka mkoa wa Shinyanga. Mh. Nchambi na mbunge wa Kishapu, na Mh. Makamba ni mbunge wa viti maalum.

Katika kutetea hoja yake Mh. Suleiman Nchambi alimdhalilisha Mh. Salome Makamba kwa kudai kuwa almasi iliyopatika huko Kishapu inatosha kuvaliwa ktk kiuno cha Mh.Makamba na akamburudisha mumewe.

Spika Ndugai ndiye aliyekuwa akiongoza kikao, lakini ktk hali ya kushangaza hakuchukua hatua yoyote ile.

Binafsi siamini kama Mbunge yeyote wa CDM angetoa lugha ya namna hiyo angeachwa bila kuchukuliwa hatua na mwenyekiti wa kikao, Naibu Spika, au Spika.

Unaweza kusikiliza hapa chini kuanzia dakika 4:59



cc Salary Slip , Erythrocyte , Kalamu1 , Nguruvi3

Karma is real!.
Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536 - JamiiForums
P
 
Hivi mbona CHADEMA hamna wabunge wa Kihindi,Kiarabu,Kirundi,Kinyarwanda?
 
Unfortunately, and inexplicably, nobody raised any stink about it. Not even Salome herself.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom