Mh. Naibu Waziri Kigwangalla unayajua haya? Hospitali ya Ocean Road haina dawa kwa miezi 6

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,558
25,324
Dr. Kigwangala ana dhamana ya ubunge na uwaziri kwa uwakilishi na utumishi wa umma, toka ateuliwe kuwa waziri shughuli zake zinazooneka dhahiri ni ushiriki wake kwenye mitandao ya kijamii.

Sio nia ya uzi huu kuuchambua ushiriki wa Dr. Kigwangala kwenye mitandao ya kijamii, bali kama kipambanuzi kwenye matatizo yaliyo kwenye wizara aliyo na dhamana nayo.

Dr. Kigwangala unajua kuwa hospitali pekee nchini kwa magonjwa ya saratani (cancer) Ocean Road haina dawa kwa zaidi ya miezi 6 sasa?
Kuna haja gani ya kukimbizana na kujibizana na akina dokta Mwaka huoni badala yake umepaswa usimamie upatikanaji wa dawa pale ocean road hospital?

Kwa spirit ile ile aliyoitumia kumjibu dokta mwaka kuwa hakusoma nae ajitokeze hapa hapa ajitetee kwa tuhuma za kufanya kazi (tangible) chini ya kiwango.

Naomba kuwasilisha.
 
Dr. Kigwangala njoo kipande hii ukanushe au kuthibitisha habari ya dawa ocean road na chanjo nchini inasemekana hakuna,
Kwanini usingiziwe??
 
Nilitarajia Mh. Atakuwa amejitokeza na kujibu hoja, kumbe anamuonea dokta mwaka pekee.
 
Dr. Kigwangala njoo kipande hii ukanushe au kuthibitisha habari ya dawa ocean road na chanjo nchini inasemekana hakuna,
Kwanini usingiziwe??
Hayo yanamuhusu Ummy Mwalimu ambae kwa sasa yupo busy sana kuhakikisha KY haziuzwi tena madukani kwahiyo wenye saratani wasubiri. Mh. Kigwangalla yeye kipaumbele chake ni Mganga wa jadi Mwaka, mpaka ahakikishe kammaliza kuweni na hakika hamtaona tena roll call wizarani au akimtetea lady JD kutukanwa na Gardner. This only happens in TZ.
 
Mkuu una maana hatajitokeza kujibu???!
 
Hayo yanamuhusu Ummy Mwalimu ambae kwa sasa yupo busy sana kuhakikisha KY haziuzwi tena madukani kwahiyo wenye saratani wasubiri. Mh. Kigwangalla yeye kipaumbele chake ni Mganga wa jadi Mwaka, mpaka ahakikishe kammaliza kuweni na hakika hamtaona tena roll call wizarani au akimtetea lady JD kutukanwa na Gardner. This only happens in TZ.
Hatari sana hasa unapokuwa kwenye nchi yenye changamoto nyingi kama Tanzania
 
Back
Top Bottom