MH. Mwakyembe Swala kuchimba DAWA safarini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MH. Mwakyembe Swala kuchimba DAWA safarini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by pilau, Aug 31, 2012.

 1. p

  pilau JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Amri ilitolewa ndani ya bunge la Tanzania na Mh. Mwakyembe waziri wa miundo mbinu kuwa ni marufuku kwa wenye mabasi kusimamisha magari yao njiani yakiwa na abiria porini kwa ajili ya watu kujisaidia (kuchimba dawa) wale watakaopatwa na tumbo la kuharisha na wenye kukojoa kila baada ya saa 1 watakomaje au mabasi yatatumia mifuko ya rambo????????????
   
 2. Sanja

  Sanja JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  Tarehe 1 sept ndo inaingia kumbe, haya sasa mradi huo wajasilia mali ombeni vibari vya biashara mchangie allowance za wenye meno.
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Pollonium 210 imeharibu ubongo.
   
 4. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mbona inawezekana kabisa, ni uamuzi wa busara sana. Kwa kawaida binadamu bladder inakuwa full kila baada ya masaa ma3, basi likitoka ubungo kituo cha kwanza Msamvu, cha pili ruaha mbuyuni cha tatu Makambako/ Njombe na mwisho safari inakuwa imekwisha kwa wale wa songea, Mbeya sijafika lakini baada ya kutoka makambako nadhani si zaidi ya masaa ma5
   
 5. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  kweli kabisa mkuu, ilianzia kwenye bone marrows, halafu ikapumzika kwenye ubongo. siku hizi uwezo wake wa kung'amua mambo kidogo umeanza ku-deteriorate. dah!!!  Tuendeleeni kuwaelimisha wananchi, waelimike ili waling'oe madarakani hili li-serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Watu tunatofautiana bro, wengine tukinywa hata robo glass ya maji basi unachokoza utachimba dawa zaidi ya maji uliyokunywa. Na kuna wenye matatizo kama wazee, wajawazito na watoto.Nadhani serikali kwanza ingeweka hivyo vituo na vyoo vya njiani halafu ndio wangetuletea hii habari. Watu wanaopewa tenda ya kutengeneza barabara labda watengeneze kabisa na vituo vya mapumziko.
   
 7. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Maundumula nadhani Mupirocin ameeleza vizuri kabisa kwamba kama utaratibu unawekwa na unakubaliwa ni rahisi kupanga vituo vya kusimama kwani mbona vipo tayari? - tubadilike na kuwa jamii ya wastaarabu zaidi
  kama unakwenda Mbeya mfano, sehemu zenye hotel na vyoo mbona ni nyingi? kuna chalinze, Morogoro/msamvu, mikumi, ruaha mbuyuni/aljazeela, Kitonga motel, ilula, Iringa Town, Mafinga, Makambako, na kabla ya kufika mbeya vipo vingi hapa katikati. kama utaratibu utawekwa watu watajenga mahotel na vyoo mimi sioni tatizo katika hilo cha msingi narudia tubadilike na kuwa jamii ya wastaarabu zaidi
   
 8. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Kawaida ipi unayoongelea hapa ile ya 1+1=2....!!!!????

  Hayo mahospitali yanayojengwa na specialists wa magonjwa ya figo na vibofu ni ya nini kama unawaza binadamu wa kawaida??????

  Polyuria unaiweka kundi gani for watever the reason may be a causative?????

  Alitakiwa kuweka vyoo kwanza kila baada ya umbali flan then na exceptionals kwa wenye matatizo na dharura sio kupiga marufuku tu.......kwa hili aliteleza na anatakiwa aambiwe wazi kuwa hii si sawa......waeza kuta hata kwake ana choo cha nje lakini kwa sie wapanda mabasi tutajijua............wajenge jela mpya maana hili litatufungisha wengi

  Yaani nijiharishie kwenye gari eti kisa sheria........booking ziruhusiwe huko mahabusu as anytime waeza jikuta umo
   
 9. Mhoja

  Mhoja JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Je ikitokea gari imepata hitilafu katikati ya pori ikasimama, kwa ajili ya matengenezo mafupi na abiria wakashuka ili wachimbe dawa mwakyembe atawafanyaje hao abiria?
   
 10. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Mpaka lini hii serikali yetu itakuwa inatufanya sisi tujisaidie kwa huruma ya wenye mahoteli?????
  Kama ni sheria ilitakiwa vijengwe vyoo kwanza tena vya bure na serikali yenyewe halafu ije hiyo sheria.......hebu assume siku wote wenye hoteli wamegoma na hakuna huduma......sheria itaegemea wapi??????

  Haki na wajibu jaman......au utii wa sheria bila shuruti ni kwa mwananchi tu????

  Siungi mkono hoja ya mtu kujisaidia hovyo vichakani....ila je ni kweli ukijenga vyoo visafi na kutoa elimu ya kutosha bado watu watapenda kwenda machakani ambako unajisaidia huku una hofu ya nyoka?????

  Na kuna sehemu hazifungiki kamba incase ndo umegongwa na nyoka.........!!!!!!!!
   
 11. Paul Ndugulile

  Paul Ndugulile Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nchi hii ni ya dili, wenye Mahotel ktk maeneo yaliyotangazwa na Sumatra wamecheza dili ili vipato viongezeke mfano Bus za Dar-Mza ni 10 kila kituo cha Hotel au choo cha kulipia @200mapato yataongezeka na watakao kula chakula nao watakuwa wengi, hii ni akili mkichwa!
   
 12. p

  pilau JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mimi ninahisi kuwa Mh. Mwakyembe alipotoa amri hiyo bungeni alikuwa katika hali ya kuifanya makadirio ya wizara yake yapite ni dhahiri kwamba hakulifanyia utafiti, kuzingatia wajawazito, wagonjwa, wazee nk gari kuharibika au kupata ajali porini na mambo yanayoweza kujitokeza
   
Loading...