Naibu Waziri wa Afya Dkt Ndugulile: Ni marufuku Hospitali kushikilia maiti kwa kile kinachotajwa hadi pale gharama za matibabu yake zitakapolipwa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Serikali imepiga Marufuku Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati zote nchini kushikilia maiti kudai fedha iliyotumika katika matibabu.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa afya Dk. Faustine Ndugulile wakati akiwa ziarani katika Kata ya Kileo mkoani Kilimanjaro.

Hatua hiyo ya Serikali inakuja siku chache baada ya Mbunge wa CHADEMA Jospeh Mbilinyi kuitaka Serikali kuacha tabia kwani si ya kibinadamu.

Sugu alisema kitendo hicho sio cha kibinadamu na ni kuwanyima haki ndugu zake.

=====

MARUFUKU HOSPITALI KUSHIKILIA MAITI " -DKT NDUGULILE

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amepiga marufuku hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kote nchini kushikilia maiti kwa kile kinachotajwa hadi pale gharama za matibabu yake zitakapolipwa.

Dkt Ndugulile ametoa tamko hilo wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha Afya cha Kileo na kusikiliza kero za wananchi wa kata ya Kileo.

Chanzo: Clouds Media

1581579903278.png


Pia, soma:


 
Da! hapo CHADEMA watasema sana kuwa bila wao serikali isingetoa hiyo tozo mbona ni hoja ya muda mrefu sana hiyo ilikuwa haijatolewa maamuzi tu.
 
Kiukweli hivyo nikudhalilisha maiti, ni bora kuwe na utaratibu wa namna ya kurecover hizo hela, ni bora mshikilie shamba la marehemu kuliko maiti yake.
 
Hivi haya malalamiko ya watu kudaiwa mpaka kufikia kushindwa kukomboa Milo ya wapendwa wao mahospitalini wakaishia kufanya ibada nyumbani na kumshukuru Mungu hayakusikika miaka yote yamesikika mwaka wa uchaguzi?
Bibie unafikri mambo yote yanaweza kufanyika kwa wakati mmoja? hli ndo muda wake umefika acha kuliweka kuwa la kisiasa.
 
Kiukweli hivyo nikudhalilisha maiti, ni bora kuwe na utaratibu wa namna ya kurecover hizo hela, ni bora mshikilie shamba la marehemu kuliko maiti yake.
Hata kushikiria mali ya marehemu bado ni aibu kwa serikali hapo ndipo inatakiwa ionekane nguvu ya serikali kumsaidia mwananchi.
 
Hivi haya malalamiko ya watu kudaiwa mpaka kufikia kushindwa kukomboa miili ya wapendwa wao mahospitalini wakaishia kufanya ibada nyumbani na kumshukuru Mungu hayakusikika miaka yote yamesikika mwaka wa uchaguzi?
Kwahiyo mwaka wa uchaguzi shughuli zote za uongozi zisimame!?
 
Yani kuna watu ni bora kwao waendelee kuwa na matatizo ambayo yatawafanya waendelee kuilalamikia serikali na kuliko kulitatua hilo tatizo ambako akose la kulalamika,yani kifupi wabongo washazoea matatizo yao na ni kama burudani tu kwao kulalamika lalamika wanachukizwa na CCM kuliko na matatizo yanasababishwa na CCM.
 
Haya ndiyo mambo (matamko ya kisiasa) yanayokwamisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ktk nchi yetu na pengine nchi nyingi za dunia ya tatu.

Kwanini kuingilia utendaji wa taasisi kwa kuingiza siasa? Kama ni Sera ya taasisi watu kulipia, why intervene it simply because of the political reasons?

Hii inaweza hata kupelekea hata taasisi mwisho wake kushindwa kujiendesha na kujisimamia kwa sababu inakuwa imeshindwa kukusanya maduhuli yake.

Mimi nasema hili kwa sbb nina hakika serikali haizihudumii hospitali zetu za umma kifedha kwa 100% sawasawa tu na shule za umma kiasi ambacho kumepelekea huduma zitolewazo ktk taasisi hizi kuwa duni zisizo na ubora wala viwango vibavyotakiwa!
 
Back
Top Bottom