Dkt. Mpango tunaomba hiyo barabara uisogeze mpaka hapo Homboza Centre

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
3,198
5,774
Mheshimiwa Philipo Mpango tunaishukuru Serikali kwamba hatimaye barabara ya kutoka Chanika imefika zingiziwa. Yaani imeishia getini kwako mheshimiwa. Tulikuwa tunaomba angalau basi utusaidie isogezwe ili ipitilize kidogo ifike angalau hapo Homboza center ambapo daladala za kuelekea Kariakoo (Machinga complex) zinaanzia.

Maana tunapata taabu sana sana hicho kipande cha kama km 1 hivi kina mateso sana hasa pale inapokuwa inanyesha. Daladala haziendi Homboza kabisa wakati mwingine hata boda boda na bajaji zinashindwa kwenda huko.
 
Hivi imefika sehem inaitwa chanika majumba sita Nina kiwanja huko ila muda sijafika kusema kweli
Imeishia darajani pale kwa mh. Makamu wa raisi.ukivuka tu lile daraja unaingia Homboza wilaya ya kisarawe unaanza na mitope na madimbwi ya kufa mtu.
 
Mheshimiwa Philipo Mpango tunaishukuru Serikali kwamba hatimaye barabara ya kutoka Chanika imefika zingiziwa. Yaani imeishia getini kwako mheshimiwa. Tulikuwa tunaomba angalau basi utusaidie isogezwe ili ipitilize kidogo ifike angalau hapo Homboza center ambapo daladala za kuelekea Kariakoo (Machinga complex) zinaanzia.

Maana tunapata taabu sana sana hicho kipande cha kama km 1 hivi kina mateso sana hasa pale inapokuwa inanyesha. Daladala haziendi Homboza kabisa wakati mwingine hata boda boda na bajaji zinashindwa kwenda huko.
Afrika imejaa raia na viongozi wabinafsi. Viongozi wana tabia ya kupeleka huduma za muhimu hadi wanapoishi beyond that mtajua wenyewe au itachukua muda sana. Wanaopata abhati ndio wanaokuwa katika uelekeo wa kuelekea kwake. Alichofanya hapo kimefanyika hata huko kwao Kigoma
 
Mheshimiwa Philipo Mpango tunaishukuru Serikali kwamba hatimaye barabara ya kutoka Chanika imefika zingiziwa. Yaani imeishia getini kwako mheshimiwa. Tulikuwa tunaomba angalau basi utusaidie isogezwe ili ipitilize kidogo ifike angalau hapo Homboza center ambapo daladala za kuelekea Kariakoo (Machinga complex) zinaanzia.

Maana tunapata taabu sana sana hicho kipande cha kama km 1 hivi kina mateso sana hasa pale inapokuwa inanyesha. Daladala haziendi Homboza kabisa wakati mwingine hata boda boda na bajaji zinashindwa kwenda huko.
Barabara ikikamilika hamtaruhusiwa kuitumia ili isiharibike mapema.
 
Na wakamilishe barabara ya kuingia zingiziwa sokoni / mnadani inatia aibu sana,yaan daladala zinashindwa kabisa kuingia sokoni wakati wa mvua

Ushuru ambao ungepatikana kwa dala dala kuingia kule ungeongeza sana mapato

Nchi hii uzembe umezidi sana
 
Sidhani kama barabara ile imeishia getini kwa Makamu, isipokuwa imeishia mpakani mwa Mkoa wa Dar es Salam na Pwani (Kisarawe DC).

Kipande cha barabara kinacholalamikiwa kipo Kata ya Msimbu, Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mkoa Pwani; na inapita kitongoji maarufu kiitwacho Majumba Sita, Homboza na kuelekea Msanga hadi kata ya Masaki.

Ninadhani sababu kuu ya kuchelewa kuwekwa lami ni za kimipaka(kimikoa) na siyo kwamba VP kajipendelea kwamba lamii iishie Chanika.

Nimewahi kuzungumza na Diwani wa Msimbu ambapo aliniambia kwamba katika miradi ya barabara inayopendekezwa katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kisarawe, hiyo barabara ni moja wapo.

Eneo la Kata ya Msimbu (Homboza) lipo ndani ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kisarawe(kata nyingine za Mji ni Kisarawe, Kiluvya, na Kazimzumbwi).

Kisarawe ipo katika harakati za kuboresha Mji wake na hivi karibuni Madiwani na Menejimenti ya Kisarawe DC walifanya ziara katika Mji Mdogo wa Korogwe, Tanga, kwa lengo la kujifunza namna bora ya kuendesha Mamalaka ya Mji.

Nimewahi kufanya kazi Kata ya Msimbu (Homboza) na nimeshuhudia adha na kero ya ile barabara, lakini bila shaka mamlaka zinafanya jitihada za kuhakikisha njia ile inapitika ukizingatia kwamba hiyo barabara ndiyo njia inayotegemewa na malori yanayochota mchanga kutoka machimbo ya Msanga Zalala na Mbezi (Mbezi ya Kisarawe-Mkuranga).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom