Mh.Mnyika hii si sawa

Mh.Mnyika hii si sawa

Tatizo ni kwamba kwa kila tukio linalohusisha Mtu kufa au kuumia ndivyo Watu wengi wanavyozidi kujiuliza Maswali kama kweli Wapinzani wapo kwa ajili ya kuwatetea au vinginenvyo, haya mambo hayataki jazba, kitu cha mwisho ambacho Wapinzani wanahitaji sasa hivi ni wananchi kupoteza Imani kwao, na hiyo Imani itazidi kutoweka kila pale Mtanzania anapopoteza Maisha, bila sababu! Tiini Mamlaka iliyopo, basi hata Mungu atawabariki huko mbeleni kwa maana imeandikwa!

wanauliwa na polisi mkuu,hembu polisi wakae pembeni wasindikize maandamano tuone kama kuna mtu ataumia au kujikwaa.polisi wakitumia nguvu mtu anakufa
 
Maandamano nihaki yetu hatuwezi kusubiri mpaka 2015 kwani nch sasa ishakua kichwa cha mwenda wazimu,wanao tuongoza hawajitambui wala hawajiamini

Maandamao ni haki yetu, lakini pia Serikali ina haki na uwezo ya kuyaruhusu au kutoyaruhusu, kwa jinsi inavyoona inafaa!
 
Umeona itv saa 12,wakazi wa makongo wanauziwa maji sh 300 kwa ndoo.sasa kama hutaki tuandamane tupe maji safi na salama

kwa hiyo mkiandamana kesho hiyo hiyo mabomba yooote yataanza kutoa maji sio?hivi kama tatizo ni serikali kwa nini tusitafute namna ya kuhamasisha raia watumie njia za kisheria kuirestisha in pisi?kwa mfano jimbo la ubungo tunahamasishana asipite hata diwani mmoja uchaguzi ujao na pengine manispaa ya kinondoni.after then tukishamiliki halimashauri tunaendesha mambo kitaalamu zaidi na kwa kuangalia vipaumbele.ninachomaanisha ni kuwa,kwa nini tuendeshe harakati badala ya kujipanga tuondoe tatizo kuu?wakitatua tatizo kabla ya uchaguzi ujao si watakuwa wamegain na sisi tumepoteza even if watakuwa wametekeleza kwa shinikizo letu?si watasema serikali imefanya?
 
Maandamano nihaki yetu hatuwezi kusubiri mpaka 2015 kwani nch sasa ishakua kichwa cha mwenda wazimu,wanao tuongoza hawajitambui wala hawajiamini
 
Naelewa machungu yako, lakini hayabadilishi ukweli kwamba Mamlaka iliyopo imechaguliwa na Watanzania kwa wingi wao, wenye maji na wasio na maji, wenye umeme na wasio na umeme, Maskini na Matajiri hivyo wote kwa ujumla wetu hatuna budi kuitii, ndio demokrasia yenyewe hiyo, na kama tunaona haitutendei haki tuna uwezo wa kuibadilisha 2015 na kuweka Mamlaka ambayo itafanya yale yanayotupendeza, ila kwa sasa hatuna jinsi!

Isitoshe hata Wapinzani nao siku moja watapewa Mamlaka ya kuongoza na Watz, ninaweza kukuhakishia sio 100% yetu tutawachagua, lkn kwa kuwa wengi watakuwa wamewachagua wengine tuliobaki tutakuwa hatuna budi pia kutii Mamlaka watakayokuwa nayo, sasa kama kila mtu akisema kwa kuwa hapendezwi na maamuzi ya Mamlaka iliyochaguliwa kihalali aandame hata kama Mamlaka imemkataza, pia wao watashindwa kuongoza, na watatumia njia zilezile ambazo Mamlaka ya sasa hivi inatumia, hakuna jipya Dunia hii tumeona Afrika Kusini, ANC wanatumia jeshi lile lile na mbinu zile zile kuuwa watu walewale waliokuwa wanawapigania miaka yote!

Demokrasia ni ngumu sana!

Rais na Serikali za Tunisia, Misri, Libya na Syria walichaguliwa ki-halali na ki-katiba zao, lakini nguvu ya umma iliwapiga au inawapiga chini. Bila kumwagika damu hakuna ukombozi wa walalahoi! Na kwa hapa TZ damu ishamwagika na itaendelea kumwagika hadi ghadhabu ya Mungu (kwa kupitia nguvu ya umma) itakapowaondoa hata hao waliowekwa madarakani na Umma huo huo, katiba hii hii na Mungu huyo huyo. Waliomwaga damu (hata kama wako hai au wamekufa) mbona ni wengi tu! Ulimboka, Kibanda, Mwangosi, Kijana wa Morogoro, Mauaji ya Arusha, Mtwara, Mbeya, etc...Vox Populi Vox Dei.
 
Unaogopa maandamano kweli vijana bado hamjui lolote kuhusu maisha na haki zenu za msingi,hata kutetea haki zako unaogopa?ipo siku utany`ang`anywa hata kiatu na hutaweza kujitetea,maendeleo hayawezi kupatikana kwa kusubiri huruma ya ccm wewe umetoka nchi gani? mali asili na huduma za msingi kwa binadamu ni haki ya kwanza unatakiwa uipate hata kwa ncha ya upanga si kulia lia na uoga ka kunguru,serikali ya ccm wanaweza kukuwekea bomba moja kati ya watu elfu moja utakapo hoji utaambiwa subiri miaka mitano mingine wakati wa kampeni!wakati ni huu dai haki yako kama mlipa kodi dai kwa nguvu zote!
 
Mheshimiwa Mnyika tunakupenda kwasababu una mchango mkubwa kwa nchi yetu, mi nachoshauri ni kwamba hayo maandamano yasitishwe na hivyo vipengele polisi walivyotolea makosa vvifuatwe na kuwaomba hao polisi wawaelekeze maandamano yapite njia gani kwa hapa mjini coz wanasingizia shughuli kwenye barabara ya morogoro zitakwama
kwani hawaelewi kwamba sehemu nyingi duniani zinazotokea maandamano shughuli nyingi husitishwa?
ni jambo la kawaida sana kwasababu maslahi ya wananchi yanatakiwa kujaliwa
na hawawezi kuonyesha kilichopo moyoni mpaka waandamane
kwa hiyo Polisi Kenyela waonyeshe waandamanaji waanzie wapi na waishie wapi sio kuleta visingizio na kujibu maswali ambayo waziri mhusika anatakiwa kuyatolea maelezo
 
Back
Top Bottom