Mh.Membe aiteka Kanda ya Ziwa.

Mh.Membe aiteka Kanda ya Ziwa.

This is too low for membe. Kuwalipia tiketi za ndege wachumia tumbo Ally Salum Hapi na Paul makonda na kujifanya wakazi wa mwanza ili kupata attention ya kanda ya ziwa ni kufilisika kisiasa.
Mkuu unashangaa low ya mwandishi kwani memmbe mwenyewe unamwonaje
 
Upotoshaji mkubwa huu. Eti kaiteka Mwanza? Mie niko Mwanza hata taarifa zake sina, na sio mimi tuu. Umesema wasanii kumbe hao wa Dar?
Acheni utoto, hata wanaompokea mbunge wao Wenje huwa na msisimko kulilo huo wa kujipa moyo ili mgawiwe fedha za ufisadi. Njaa msiiendekeze sana
 
akija lowassa hapo mwanza mitaa yote itafungwa.

Membe ni cha mtoto kwa gwiji la siasa za tz mzee wa kutenda lowassa.

Ni nadra sana kwa wanasiasa nchini kukubalika kwa kiasi kikubwa mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na ushindani mkubwa wa kisiasa nchini hususani ndani ya Chama Cha Mapinduzi.Ila Mh.Bernard Kamillius Membe kwake imekuwa tofauti.

Jana akiwa ameongozana na kundi la marafiki zake,wafuasi wake na wanachama wa Ccm alizuru jiji la Mwanza saa moja usiku na kulakiwa na maelfu ya wasanii wa filamu,muziki na wananchi wa kila rika waliokuwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kumkaribisha kwa upendo mkubwa jijini Mwanza.

Halikuwa jambo dogo,kila aliyekuwepo hakuamini kilichotokea.Mh.Membe ana wafuasi ambao hata yeye hakuweza kuelewa wametokea wapi.Kila mmoja alitaka kuongea naye,kumshika mkono au kupiga naye picha.Chama cha waendesha bodaboda mkoa wa Mwanza walijitolea pikipiki zao bure kuongoza msafara wa kumlaki Mh.Membe.

Wananchi walikuwa wakiimba;"Membe jembeee,Membe oteshwa,Membe usitusahau wakazi wa Mwanza tunakuunga mkono".

Ilikuwa ni kama Mandela amezuru jiji la Mwanza.Historia imeandikwa rasmi,na huu ni mwanzo tu.Kilio cha wasanii kimesikika kutokana na kiu yao kubwa ya kuwa karibu na Mh.Membe na kusaidiwa matatizo yao yanayosibu tasnia ya filamu.


Wasanii walioongoza msafara wa kumpokea Mh.Membe wote wana ushawishi mkubwa nchini kama vile Mjomba Mpoto,Steven Mengele Nyerere,Adam Melele"Swebe Santana Nunda",Blandina Chagula"Johari",Wastara Juma,Cathy Rupia na Kulwa Kikumba almaarufu kama Dude.

Mh.Membe alikuwa kaalikwa kuzindua filamu iitwayo I Love Mwanza ikiyoandikwa na Adam Melele almaarufu kama Swebe Santana Nunda.Mh.Membe kaahidi neema kwa wasanii nchini.Kakubali kuwa baba wa hiari wa wasanii wote wa filamu nchini.

Mh.Membe pia katika msafara waje aliungana na Mh.Lazaro Nyalando,Mnec Christopher Mwita Gachuma,Paul Christian Makonda na Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Waziri Rajab.

Jana Mh.Membe baada ya kuizindua filamu hii ya I Love Mwanza rasmi leo atakuwa Ccm Kirumba akikamilisha ratiba ya tamasha kubwa kuhusu sanaa kwa wakazi wa jiji la Mwanza.Wote mnakaribishwa!

Imetolewa na:
Friends Of Hon.Membe
 
Huyo Membe anajisumbua tu,sisi kanda ya ziwa tumemwomba Magufuli apeleke jina,labda kamati kuu imuengue.
 
Membe ana fit ktk wizara aliyo nayo, hakika hilo halina ubishi lkn ktk Ukuu wa nchi yetu bado hajaiva vya kutosha.

Sema uwezo hana lakini kusema jiwe litaiva ni kosa na haiwezi kutokea,Membe ni kama jiwe mkuu haliwezi kuiva kwa nafasi ya urais
 
Huyo Membe anajisumbua tu,sisi kanda ya ziwa tumemwomba Magufuli apeleke jina,labda kamati kuu imuengue.

Magufuli is a ministerial material not presidential material. Then he's incapable of internal CCM politics.... Master wao yupo kiboko ya wote gwiji la siasa Tanzania. Jiwe kuu la pembeni
 
Huyo Makonda ndo yule nilisikia kaiba simu bunge la katiba?
miniko hapa mwnza sijaona hekaheka yoyote !!
 
Badala ya kuzunguka na wataalamu wa mambo ya uchumi,biashara na kilimo ili wamsaidie kuelewa kiini cha matatizo yanayowakabili Watanzania wa tabaka la kati na la chini yeye anazunguka na wasanii?Another Kikwete in the making. Nahisi Ikulu itaendelea kuwa kijiwe cha wasanii wa bongo movie na bongo flava as long as Membe will be the next man to hold the throne.
We can't afford to have another celebrity President in the White House, We need real leaders not wanna be Presidents like the one we have in the White House right now! Sad thing is,There is enough small minded Tanzanians who will actually vote for him.
 
Sijaona umati hapo zaidi naona mijitu miwili tu tena mifisadi sasa sijui ndo umati hio.

attachment.php
 
Back
Top Bottom