Mh. Mdee , zimwi litujualo halituli.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Mdee , zimwi litujualo halituli..........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GeniusBrain, Feb 3, 2012.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi sasa wabunge waliochaguliwa wa majimbo mbali mbali wapo kwenye utekelezaji wa ahadi walizo zitoa. Mie ni mkazi wa jimbo la Kawe, na mojawapo ya ahadi aliyoahidi mbunge wa Kawe, Mh. Halima Mdee ni kuhusu ujenzi wa barabara ya msasani kwa mamwinyi amabayo hupitwa na idadi kubwa sana ya watu wanao kwenda kazini mjini.

  Na kwa ahadi yake alisema ndani ya miezi 3 baada yakuchaguliwa angeishughulikia hii barabara. Ila chakushangaza, mpaka leo hii hakuna chochote na Mh. Mdee hajasema lolote zaidi ya kumuona kwenye kumbi za starehe na mjengoni.

  My take : Ndio kusema Mh. Mdee ulitudanganya ili tukupe kura tu zakufanya matanuzi na kumbe ulikuwa huna uwezo wa kuijenga hiyo barabara ndani ya miezi 3? Na mpaka sasa ni ahadi gani umeisha tekeleza kwenye jimbo la kawe ?. Kweli Mheshimiwa, zimwi litujualo halituli ............

   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Serikali inamkwamisha yeye Mdee hana fuko la mahela ya kujenga barabara kumbuka yeye sio fisadi kanakwamba anaweza toa pesa za mfukoni mwake ajenge hiyo barabara
   
 3. M

  Mpenda Haki Tanzania Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vipi wantanzania tuliodandanywa maisga bora kwa kila mtu?
   
 4. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Wewe punguani kweli yaani baba zima ukakaa kabisa ukaamini kuwa mbunge atajenga barabara ndani ya miezi mitatu kwa fedha gani alizona wameshindwa kujenga barabara akina Rostam itakuwa Mhe Halima Mdee. Soma Katia utambue majukuu ya wabunge sio kujenga mabarabara

  KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
  TANZANIA YA MWAKA 1977

  63.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.
  (2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
  (3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza-
  (a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
  (b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
  (c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
  (d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
  (e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

  wapi imetaja mbunge atawajengea wakazi wa jimbo atokalo barabara. Majukumu yaliyotajwa hapo juu yanmhitaji mbunge kusoma sana machapiho mbali mbali. ripoti na kufanya utafiti ili aweze kuismamia serikali ya kifisadi kama ya Tanzania barabara, hivyo muda wa kuleta maendelo majimboni haupo. Ni kutokana na watanzania wengi kuwa ubinafsi wa kijimbo kama wewe ndio maan serikali yetu inakosa usimamizi kwa kuwa wabunge wako busy kufanya kazi za utarishi wa kupeleka maendeleo jimbo moja moja matoek yake raslimali na utajiri wote wa Tanzania unakosa usimamizi kwa kuwa unasimamiwa na mhimili wa srikali ambao na hausimamiwi ipasavyo na mhimili wa bunge kwa kuwa wabunge wako busy na mendeleo ya kijimbo.

  Hivyo mafiadi wanajitwali raslimli za Tanzania watakavyo. Kutoakana ubinfsi wa kila mtu kutaka maendeleo ya jimbo lake tu, watanzania wote tunakosa maendeleo kutokana na raslimli zetu kuibiwa.

  maendelo tanzania yatapatikana pale tu watanzania watakapoacha kuwadai wabunge maendeleo ya jimbo moja moja na badala yake kudai uwajibikaji katika kuisimamia serikali ili nayo isimamie raslimali na fedha zetu ipasavyo na kubana matumizi ili kwa pamoja raslimali za kuleta maendelo ya nchi ziweze kupatikana
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  una uhakika hashughulikii? Au mpaka abebe kokoto kumwaga barabarani?
   
 6. Y

  Yetuwote Senior Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningekushauri uende office ya mbunge ukapate taarifa kamili ya jinsi alivyorishughulikia. Barabara kujengwa kuna hatua zake za awali.
   
 7. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kikwete kashindwa maisha bora kwa kila mtanzania na amekaa miaka sita ....pimbi wengine bana
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama yeye alijua haya aliahidi ya nini ndani ya miezi 3 na kwa kauli yake mwenyewe? huu sio utapeli sasa wakuahidi kitu ambacho huna mamlaka nacho?

   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jibu hoja ya Mdee , hujajibu chochote hapo. Haya jibu sasa

   
 10. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Siutambui Uelewa wa Huyu Mtoa Hoja!! Anafikiri kuwa Tanzania Bado Ina wajinga wengi wa kudanganywa na kudandia Hoja za Hovyo!!
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hawana majibu yoyote na Mh. Mdee mwenyewe hata ofisini hayupo

   
 12. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Si ndio utaratibu uliwekwa na waasisi wa taifa hili, ukitaka kumfurahisah mtanzania mdanganye, Ukimwambia ukweli kama nilivyosema hapo juu hataki kusikia na anakuchukia.
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Huyu mleta mada atakuwa amelishwa pollonium 220, ambayo ukiimeza tu unachanganyikiwa na kuanzisha thread za ajabuajabu!, maana tokea jana anajitahidi sana kuanzisha thread zisizo na mashiko...!

  Ofisi ya Mbunge iko wazi muda wote, na ina wafanyakazi hata kama ukimkosa Mbunge!..kwanini umwogope Mdee?
  Nilitegemea kwa msomi kama wewe umuulize swali lako ofisini kwake, na uje na kauli atakayokujibu hapa, na si kulalama pasipo substance!...huh!
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Failed. Hujajibu hoja , jibu hoja. Acha kupoteza rasilimali muda

   
 15. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hakuna barabara inayojengwa kwa miezi mitatu ikakamilika. Nadhani ndugu yangu hukumuelewa Mh Mdee, alisema ndani ya miezi mitatu ataanza kulishughulikia, lakini si baada ya miezi mitatu barabara itaanza kujengwa. Sasa kama unavyojua wenye jukumu la kujenga ni serikali, na unajua hali ya serikali yetu kwa sasa, ni muflisi, kwa hiyo hata Mh ajitahidi namna gani serikali haina pesa jamani.

  Upuuzi wa namna hii ndio magamba walitumia kupotosha ahadi ya Dr Slaa wakati wa kampeni kuhusu Uandikaji wa katiba mpya pindi atakapopewa dhamana ya kuongoza nchi hii. Alisema akiingia Ikulu ndani ya miezi mitatu ataanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya; magamba bila aibu wanauambia umma kuwa Dr Slaa alisema baada ya miezi mitatu katiba mpya itakuwa tayari.

  Tututmie zaidi akili.
   
 16. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu,lazima tutambue ilo
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Failed. Hujajibu hoja, haya jibu hoja sasa kwa mantiki na mtiririko paka jike

   
 18. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #18
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  GB nikupe pole kwanza si kwa sababu ya ahadi ambazo Mbunge bado hajazitekeleza ila kwa majibu ya humu ndani baada ya kusema hivyo ni kweli kwamba wakati mwingine kuna maneno ya kisiasa ambayo mtu kama wewe au mwingine awaye yeyote unaweza ukayasikia ila yasikuingie akilini vizuri kwa kuamini kuwa utekelezaji wake hauwezi kuwa hivyo ambavyo mtoa ahadi anasema, kwa kutambua hilo mi nadhani labda ungeendelea kuvuta subira na kuendelea kuwasiliana na Mbunge wako kwa kumkumbusha kila mara kwa mara juu ya ahadi yake hiyo.

  Bahati nzuri Mbunge wako ni mtu msomi na mwelewa hivyo nadhani for the time being endelea kuwa na approach nzuri na vile vile usipende kumlaumu kwa kila akifanyacho na kwa maisha yake ya kawaida manake yeye kwenda sehemu za starehe kwangu haimaanishi kuwa hela anazozitumia ndizo hizo ambazo angejengea barabara as a human being she deserve to have fun with others, tena afadhali ya Mdee huku kwetu kuna ahadi ambazo alizotoa Mbunge nadhani mpaka Yesu arudi ndo zinaweza kuanza kufikiwa amebaki kubatizwa jina la Rais wa maandamano.

  Patient mind conquers all........ Kuwa na subira
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Unajua wakati wakuomba kura Mh. Mdee aliyasema hayo ndani ya miezi 3 barabara itakuwa tayari, na sie tukampa kura kwa hilo, kumbe ilikuwa kanyaboya. Hatimae tunaumia sisi aisee kwa ahadi hewa ya Mdee.

   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Well said . Yes, maisha yake binafsi wakati mwingine yanaweza kuathiri utendaji wake , ww unafikiri anakwenda kumbi za starehe mpaka saa 10 usiku unategemea kesho yake atakuwa yuko active kuwatumikia wananchi kweli ?.

   
Loading...