Hivi sasa wabunge waliochaguliwa wa majimbo mbali mbali wapo kwenye utekelezaji wa ahadi walizo zitoa. Mie ni mkazi wa jimbo la Kawe, na mojawapo ya ahadi aliyoahidi mbunge wa Kawe, Mh. Halima Mdee ni kuhusu ujenzi wa barabara ya msasani kwa mamwinyi amabayo hupitwa na idadi kubwa sana ya watu wanao kwenda kazini mjini.
Na kwa ahadi yake alisema ndani ya miezi 3 baada yakuchaguliwa angeishughulikia hii barabara. Ila chakushangaza, mpaka leo hii hakuna chochote na Mh. Mdee hajasema lolote zaidi ya kumuona kwenye kumbi za starehe na mjengoni.
My take : Ndio kusema Mh. Mdee ulitudanganya ili tukupe kura tu zakufanya matanuzi na kumbe ulikuwa huna uwezo wa kuijenga hiyo barabara ndani ya miezi 3? Na mpaka sasa ni ahadi gani umeisha tekeleza kwenye jimbo la kawe ?. Kweli Mheshimiwa, zimwi litujualo halituli ............
Wewe punguani kweli yaani baba zima ukakaa kabisa ukaamini kuwa mbunge atajenga barabara ndani ya miezi mitatu kwa fedha gani alizona wameshindwa kujenga barabara akina Rostam itakuwa Mhe Halima Mdee. Soma Katia utambue majukuu ya wabunge sio kujenga mabarabara
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 1977
63.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.
(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza-
(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.
wapi imetaja mbunge atawajengea wakazi wa jimbo atokalo barabara. Majukumu yaliyotajwa hapo juu yanmhitaji mbunge kusoma sana machapiho mbali mbali. ripoti na kufanya utafiti ili aweze kuismamia serikali ya kifisadi kama ya Tanzania barabara, hivyo muda wa kuleta maendelo majimboni haupo. Ni kutokana na watanzania wengi kuwa ubinafsi wa kijimbo kama wewe ndio maan serikali yetu inakosa usimamizi kwa kuwa wabunge wako busy kufanya kazi za utarishi wa kupeleka maendeleo jimbo moja moja matoek yake raslimali na utajiri wote wa Tanzania unakosa usimamizi kwa kuwa unasimamiwa na mhimili wa srikali ambao na hausimamiwi ipasavyo na mhimili wa bunge kwa kuwa wabunge wako busy na mendeleo ya kijimbo.
Hivyo mafiadi wanajitwali raslimli za Tanzania watakavyo. Kutoakana ubinfsi wa kila mtu kutaka maendeleo ya jimbo lake tu, watanzania wote tunakosa maendeleo kutokana na raslimli zetu kuibiwa.
maendelo tanzania yatapatikana pale tu watanzania watakapoacha kuwadai wabunge maendeleo ya jimbo moja moja na badala yake kudai uwajibikaji katika kuisimamia serikali ili nayo isimamie raslimali na fedha zetu ipasavyo na kubana matumizi ili kwa pamoja raslimali za kuleta maendelo ya nchi ziweze kupatikana